Tetesi kubwa tano za soka Ulaya jioni hii (30.08.2022)

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp kuhusu kusajili kiungo anasema:

"Ni kweli, lakini muda unavyokwenda, ndio inavyozidi kuwa ngumu (kukamilisha usajili). Hatujakata tamaa. muda upo, tusipata bado ninakifurahia kikosi tulichonacho"

Frenkie de Jong wa Barecelona na Moises Caicedo wa Brighton wamekuwa wakihusishwa kutua Anfield (Klopp Presser).

Arsenal watalazimika kuingia sokoni kusaka kiungo wa kukaba baada ya Mohamed Elneny kuumia kwenye mchezo dhidi ya Fulham utakaomuweka nje kwa muda mrefu. Elneny alikuwa mbadala wa kiungo namba moja Thomas Partey ambaye naye ni majeruhi.

Fulham wanakaribia kukamilisha usajili wa winga wa zamani wa Chelsea na Arsenal Willian, kwa mkataba wa mwaka mmoja. Mbrazil huyo yuko London sasa anafanyiwa vipimo (The Athletic).

Mazungumzo yaliyo katika hatua za mwisho yanaendelea kati ya Chelsea na Barcelona kuhusu uhamisho wa Pierre Aubameyang (Romano).

Klabu za Ajax na Manchester United zimetoa taarifa rasmi kuhusu Antony: "Ajax na Manchester United zimekubaliana kuhusu uhamisho wa Antony Matheus dos Santos." Ada yake inafikia €100 million.