Upinzani ni hatari nchini Urusi lakini wanaharakati hawajakata tamaa

tt

Chanzo cha picha, SHUTTERSTOCK

    • Author, Sarah Rainsford
    • Nafasi, Mwandishi wa BBC Ulaya Masharikii

Kufuatia kifo cha kiongozi wa upinzani wa Urusi Alexei Navalny, mfungwa mwingine wa kisiasa anajaribu kuweka hai matumaini ya mabadiliko - hata kutoka gerezani.

"Uhuru unagharimu sana," mwanaharakati wa upinzani Vladimir Kara-Murza aliwahi kuniandikia akiwa katika gereza la Urusi.

Alikuwa akimnukuu mshauri wake wa kisiasa, Boris Nemtsov, ambaye aliuawa mnamo 2015 huko Moscow - karibu na Kremlin.

Sasa mpinzani mkubwa wa Rais wa Urusi Vladimir Putin, Alexei Navalny, amekufa.

Gharama ya upinzani wa kisiasa haijawahi kuwa ya juu katika Urusi ya kisasa.

Hofu ya kuchukuliwa hatua iko juu kiasi kwamba kifo cha Navalny hakikusababisha maandamano makubwa. Mamia ya watu walizuiliwa kwa ajili tu ya kuweka maua kwa heshima yake.

Lakini Bw Kara-Murza ahajakata tamaa katika harakati hizo au matumaini yake.

Wiki hii aliwataka wafuasi wa upinzani "kuongeza bidii zaidi" kufikia kile ambacho Navalny na Nemtsov walipigania: nafasi ya kuishi katika nchi huru.

Alifanya mwenyewe, zamani sana. "Bei ya kuongea ni kubwa," mwanaharakati aliniandikia, mara tu baada ya kukamatwa mnamo 2022.

"Lakini ukimya haukubaliki."

Wanaume wenye ujasiri

Mwanaharakati wa upinzani Vladimir Kara-Murza amehukumiwa kifungo cha miaka 25 kwa kosa la uhaini

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mwanaharakati wa upinzani Vladimir Kara-Murza amehukumiwa kifungo cha miaka 25 kwa kosa la uhaini
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Alexei Navalny, ambaye alikuwa na umri wa miaka 47, na Vladimir Kara-Murza, 42, ni wanaume tofauti sana.

Navalny alikuwa mtu wa watu katika jamii, mzungumzaji mwenye mvuto huku badhi ya watu wakimtaja kuwa mtu aliyezaliwa na kipaji cha uongozi.

Bw Kara-Murza ni msomi anayezungumza kwa upole - mshawishi wa nyuma ya pazia kuliko mzungumzaji katika mkusanyanyiko wa watu.

Yeye sio jina tajika nchini Urusi hata sasa.

Lakini wote wawili walikuwa na mtazamo sawa na imani kwamba Urusi ya Putin haikuwa ya milele na kwamba uhuru wa kisiasa uliwezekana.

Wakati Navalny alipotoa video inayofichua ufisadi katika ngazi ya juu ya mamlaka, Bw Kara-Murza alishawishi serikali za Magharibi kuweka vikwazo kulenga mali za maafisa na fedha zilizofichwa nje ya nchi.

Wote wawili wamelipia pakubwa hatua hiyo.

Mnamo 2015, miaka mitano kabla ya Navalny kushambuliwa nkwa sumu ya neva, Bw Kara-Murza alianguka na kuzimia.

Miaka miwili baadaye, ilitokea tena. Vipimo nchini Marekani vilithibitisha kwamba alikuwa amepewa sumu.

Lakini hakusita kuelezea mawazo yake, ambayo ni pamoja na kushutumu uvamizi wa Bw Putin nchini Ukraine.

Mwaka jana, Bw Kara-Murza alihukumiwa kifungo cha miaka 25 kwa uhaini - ingawa hati ya mashtaka haikuorodhesha chochote isipokuwa shughuli za amani za upinzani.

Kurejea Urusi

Wakati Alexei Navalny alimoamua kurudi Urusi mnamo 2021 baada ya jaribio la mauaji dhidi yake, wengine walimshagaa.

Wapinzani ambao wameamua kuishi uhamishoni badala ya kufungwa wanahoji kuwa kujitolea bila matarajio ya mabadiliko ni bure.

Navalny alifikiria tofauti.

"Ikiwa imani yako ina thamani ya kitu, unapaswa kuwa tayari kusimamia kitu hicho. Na ikiwa ni lazima, jitolee muhanga," aliandika muda mfupi kabla ya kifo chake tarehe 16 Februari.

Vladimir Kara-Murza, sawa na Navalny, ana mke na watoto. Pia ana haki ya makazi nchini Marekani na pasipoti ya Uingereza. Lakini hakusita kamwe kurudi Urusi.

“Sikuhisi nilikuwa na haki ya kuendelea na shughuli yangu ya kisiasa, kuwashawishi watu wengine kuchukua hatua, huku nikiwa nimekaa salama mahali pengine,” Bw Kara-Murza alimuandikia mwandishi wa BBC mnamo 2022, tayari nikiwa gerezani.

Wanaume hawa wawili, walikuwa na ujasiri mkubwa.

Sasa mmoja amekufa na mwingine amefungiwa mbali na familia yake na anaruhusiwa kupiga simu mara moja tu ndani ya miezi sita.

"Sikuzungumza naye mwenyewe kwa sababu sikutaka kuchukua wakati wa watoto," Evgenia Kara-Murza alielezea simu hiyo.

Mke wa mwanaharakati huyo aliwaruhusu watoto wake watatu kusema naye kwa dakika tano kila mmoja.

"Nilikuwa nimesimama kando yao nikiangalia saa," alisema.

Wanawake wajasiri

tt

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Yulia alisaidia sana mumewe kupona baada ya kushambuliwa kwa sumu

Wiki hii, mjane wa Navalny alirekodi taarifa ya video akiwataka wafuasi wake kutokata tamaa.

"Nataka kuishi katika Urusi huru, nataka kujenga Urusi huru," alisema Yulia Navalnaya, akiapa kuendelea na kazi ya mumewe.

Evgenia Kara-Murza alishangazwa na ujasiri wake. "Anafanya kila awezalo kupita kuzimu akiwa ameinua kichwa na anashangaza."

Lakini mke wa Bw Kara-Murza amejitwika jukumu lake mwenyewe.

Tangu kukamatwa kwake Aprili 2022, amekuwa akisafiri ulimwenguni kote, akiwashawishi maafisa wa Magharibi kumsaidia mumewe na wafungwa wengine wa kisiasa, na kukemea vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.

Uvamizi huo ni uthibitisho zaidi, kama asemavyo, wa "serikali ya kikatili" ya Putin.

Tulipozungumza, Evgenia alikuwa karibu kusafiri kuelekea Marekani kuona watoto wao. Wakati huo alikuwa akielekea London kutoa wito kwa mawaziri wa Uingereza kuimarisha juhudi zao dhidi ya Rais Vladimir Putin.

"Nataka wawe na nguvu zaidi katika juhudi za kumtoa kizuizini, na kudai uangalizi sahihi wa matibabu," alisema.

"Lakini kuifanya serikali moja kuwajali raia wake ni ngumu siku hizi."

Mateso gerezani

Bw Kara-Murza ameendelea kuteseka gerezani, kama ilivyokuwa kwa Navalny.

Mwanaharakati huyo amezuiliwa katika kizuizi cha upweke kwa miezi kadhaa na hakuruhusu kuwa na mali yoyote ya kibinafsi, hata picha za watoto wake.

Mnamo Januari, alihamishiwa kwenye gereza jipya yenye hali ngumu zaidi, kunyimwa hata vitabu vyake.

Afya yake, iliyoharibiwa na sumu, inazidi kuzorota. Shinikizo la kuachiliwa kwa Bw Kara-Murza limeongezeka tangu kifo cha Navalny.

"Uharibifu wa mishipa unaenea kwa upande wake wa kulia sasa. Ni hali mbaya ambayo inaweza kusababisha kupooza," Evgenia Kara-Murza aliniambia.

Wiki hii, alipata kumuona mume wake kwenye kiunga cha video kutoka gerezani hadi mahakama ya Moscow. Alikuwa anajaribu kupata Kamati ya Uchunguzi kumfungulia kesi ya jinai juu ya sumu yake.

Bw Kara-Murza alikuwa amevalia sare nyeusi iliyokuwa kubwa kumliko.

Lakini azimio lake lilionekana kuwa thabiti kuliko wakati mwingine wowote kwani aliwahimiza Warusi wasikate tamaa.

"Hatuna haki hiyo," alihutubia wafuasi na waandishi wachache walioruhusiwa kuingia mahakamani, na kusisitiza kuwa Urusi itakuwa huru.

"Hakuna mtu anayeweza kuzuia siku zijazo."

Nini kitakachofuata?

tt

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/SHUTTERSTOCK

Evgenia Kara-Murza alitazama kipande hicho cha video kutoka mahakamani "mara elfu".

"Nadhani anafanya jambo sahihi - na jambo kubwa," aliniambia.

"Watu wanahisi kuvunjika moyo kila uchao na maneno hayo ya kutia moyo kutoka kwa watu ambao wamekataa kukubali shinikizo na vitisho ni muhimu sana."

"Ninajivunia sana Vladimir kwa kusalia imara, licha ya mateso haya."

Evgenia anaunga mkono matumaini ya siku zijazo za mume wake, pamoja na nguvu zake.

"Cha msingi ni kuendelea na juhudi za kupigania haki na kujaribu kufanya chochote unachoweza," anasema.

"Sio kukata tamaa."

Anaonyesha mwisho wa USSR na maandamano ya watu wengi ambayo yamemtia moyo mumewe kila wakati.

"Hakukuwa na kitu - hadi fursa ya hatua kubwa ya pamoja ilipojitokeza mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990. Kisha watu wakatoka mitaani," anasema.

"Tunahitaji kufanya kila linalowezekana ili kuwa tayari kwa wakati ambapo nyufa zitajionyesha serikalini."

"Hadi wakati tutakapopata nafasi hiyo."

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi