Waafrika, Waarabu au Amazigh? Mgogoro wa utambulisho wa Morocco

Shabirki wa soka wa Morocc

Chanzo cha picha, Reuters

Katika mfululizo wetu wa barua kutoka kwa waandishi wa habari wa Kiafrika, Magdi Abdelhadi anaangalia jinsi soka ilivyozua mzozo kuhusu utambulisho wa Morocco.

Ni sawa kusema kwamba Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka huu limekumbwa na utata kuliko mashindano mengine hapo awali.

Kuanzia kwa uamuzi wa kutatanisha wa kuipa Qatar fursa ya kuandaa michuano hiyo licha ya rekodi yake mbaya ya haki za binadamu hadi dakika ya mwisho kabisa ambapo Amir wa Qatar alimvisha vazi la Kiarabu gwiji wa soka wa Argentina, Lionel Messi, alipokuwa karibu kunyanyua Kombe la Dunia siku ya Jumapili.

Lakini kuna mzozo mmoja ambao ulivutia umakini mdogo au haukuangaziwa kabisa nje ya Afrika Kaskazini.

Ilianza kwa swali rahisi: unaielezeaje timu ya Morocco, Atlas Lions, ambayo iliishangaza dunia nzima kwa mchezo wake wa hali ya juu - ikikaidi uwezekano wa kuwashinda vigogo kama vile Uhispania na Ureno?

Timu ya "kwanza ya Kiarabu" au "Kiafrika" kufika nusu fainali?

Kiutamaduni Wamorocco wengi wanajiona kuwa Waarabu zaidi kuliko Waafrika - na baadhi ya Waafrika Kusini mwa Jangwa la Sahara nchini Morocco wanalalamikia kwambali uwepo wa mitazamo ya kibaguzi.

Lakini maoni ya winga wa Morocco Sofiane Boufal baada ya ushindi wao wa Kombe la Dunia dhidi ya Uhispania yalizua mjadala kuhusu utambulisho wa bara la nchi hiyo.

Aliwashukuru "Wamorocco wote duniani kwa msaada wao, kwa watu wote wa Kiarabu, na kwa Waislamu wote. Ushindi huu ni wenu."

Baada ya kauli hiyo tata kuzua gumzo katika mitandao ya kijamii, alienda kwenye mtandao wa Instagram kuomba radhi kwa kutotaja uungwaji mkono wa bara la Afrika kwa timu hiyo - iliyosifiwa na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari aliposema Morocco "imefanya bara zima la kujivunia kwa ustadi wake".

Mashabiki wa Soka

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Morocco ilipata uungwaji mkono kutoka kwa mataifa mengine ya Afrika - ikiwa ni pamoja na umati wa watu nchini Senegal - walipomenyana na Ufaransa
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Katika chapisho hilo, Boufal aliandika: "Pia naweka wakfu ushindi kwako bila shaka. Tunajivunia kuwawakilisha ndugu zetu wote barani. PAMOJA."

Mgogoro huo unaonyesha juhudi za hivi majuzi za mfalme huyo kuhimiza uhusiano wa karibu na bara zima la Afrika.

"Afrika ni nyumbani kwangu, na ninarudi nyumbani," Mfalme Mohammed VI alisema mwaka wa 2017 wakati Morocco ilipowekwa tena kwenye Umoja wa Afrika baada ya kutokuwepo kwa miaka 30 mfululizo katika eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi.

Ukaribu huu umeruhusu uhusiano wa kibiashara kustawi, haswa na Afrika Magharibi. Lakini Morocco pia ni mwanachama wa Jumuiya ya Kiarabu - kwa hivyo ni mali ya nyanja zote mbili za kitamaduni.

Ingawa kivumishi cha "Mwafrika" kuelezea Morocco ni ukweli wa kijiografia, matumizi ya "Mwarabu" pia yamewatenganisha Wamorocco wengi ambao hawajitambui hivyo.

Morocco ina idadi kubwa ya watu wa Berbers, au Amazigh kama wanavyopendelea kuitwa - baadhi ya makadirio yanaiweka katika karibu 40% ya wakazi zaidi ya milioni 34 nchini humo.

Amazigh ni watu asilia wa Afrika Kaskazini

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Amazigh ni watu asilia wa Afrika Kaskazini

Lugha moja kuu ya Amazigh - Tamazight - sasa inatambulika kama lugha rasmi pamoja na Kiarabu. Lakini uamuzi wa kufikia hatua hii ulikumbwa na utata wa muda mrefu katika.

Mara tu baada ya Qatar kutunukiwa haki ya kuandaa Kombe la Dunia la 2022, vyombo vya habari viliweka tukio hilo kama "Ushindi kwa Uislamu na ulimwengu wa Uarabuni", kama kichwa cha habari kilivyoiweka tena mwaka wa 2010.

Mashindano yalipoanza, msamiati wa Uarabuni na Uislamu ulirgonga tena vichwa vya habari.

Katika mzozo wa kupiga marufuku pombe au matumizi ya kitambaa cha OneLove cha LGBTQ, watetezi wa Uislamu na Jumuiya ya Uarabuni walijitokeza kimasomaso kutetea Qatar, Uislamu na maadili ya jadi dhidi ya " ubeberu wa nchi za magharibi".

Lakini tukio hilo lilivyoangaziwa katika na vyombo vya habari vya Qatar kuanzia mwanzo kama "Ushindi wa Kiislamu au Waarabu", haukutambuliwa kwa kiasi kikubwa, ulizua hisia ya hasira wakati ilipokuwa sehemu ya lugha ya kutoa maoni juu ya michezo.

Kwa hivyo, Atlas Lions ilipoweka historia kwa kuwa timu ya kwanza ya wanaume kutoka Afrika na Mashariki ya Kati kufuzu kwa nusu fainali ya Kombe la Dunia, ilitajwa kuwa ni ushindi kwa mataifa ya Kiislamu na Kiarabu.

Baada ya timu zingine kutoka kanda hiyo - Tunisia, Saudi Arabia na Qatar - kuondolewa mapema katika kinyang'anyiro hicho, ilikuwa ni wazi kwamba wapenzi wa soka katika nchi jirani wangeshabikia Morocco.

Lakini baadhi ya makundi ya wanaharakati yalijaribu kuonyesha mafanikio ya Morocco kama kitu kikubwa zaidi, kiitikadi zaidi na kisiasa. Kwa hivyo, timu ya Morocco ilipewa jukumu la mshika viwango wa Uislamu na Umoja wa Uarabuni.

Hoja hii ilitiwa nguvu pale baadhi ya wachezaji wa timu ya Morocco waliposherehekea mafanikio yao kwa kupeperusha bendera ya Palestina uwanjani.

Hatua hiyo iliwakasirisha baadhi ya watu eneo la katika Afrika Kaskazini, hasa Wamorocco ambao hawaungi mkono itikadi hizo na mitazamo yao ya ulimwengu.

'Vita vya kitamaduni'

Katika kanda iliyodumu kwa saa moja, Mshawishi mmoja wa YouTube asiyekubalika kutoka Morocco aliwakashifu wale ambao walitaka kuingiza siasa kwenye mchezo huo na kugeuza michuano hiyo kuwa vita vya kimataifa vya utamaduni.

Ndugu Rachid pia aliwakumbusha wafuatiliaji wake 385,000 kwamba nusu ya timu ya Morocco, ikiwa ni pamoja na kocha wao, walizaliwa na kukulia Ulaya, watoto wa wahamiaji wa Morocco ambao walijifunza mchezo na kuwa wanasoka wa kulipwa huko Ulaya.

“Ukifanya uchambuzi wa chembechembe za vinasaba DNA dhdi ya timu ya Morocco utakuta wengi wao ni Amazigh, wengi wao hawaongei kiarabu, na wakifanya hivyo itakuwa ‘hawazungumzi Kiarabu sahihi’ kwa sababu walikulia katika nchi za kigeni huko ulaya," alisema.

"Morocco ni tofauti na Mashariki ya Kati, kwa sababu kimsingi ni jamii ya Waberber, Waarabu walikuja kama wageni katika Karne ya 7. Leo hii huko Morocco kuna Waarabu, Waberber, Waislamu, Wayahudi, wasioamini Mungu, wasio na dini na Wabaha'i pia kuna Washia na Wasunni."

Kwa kuzingatia mafanikio haya ya Morocco kuwa "ushindi kwa Uarabu na Uislamu ni mashambulizi dhidi ya vipengele mbalimbali vya jamii ya Morocco", aliendelea kusema.

Kwa kujibu wafuasi wa Uarabuni au Waislam wanaotaka kuteka nyara ushindi wa Morocco kwa matumizi yao wenyewe, machapisho kwenye mitandao ya kijamii yalienea kudai kuwa timu hiyo ni ya Morocco. Baadhi waliweka picha za timu hiyo zenye alama za Amazigh.

Baadhi ya mashabiki wa Morocco

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baadhi ya mashabiki wa Morocco walijifunika bendera ya Amazigh

Wakosoaji wengine walipuuza hatua ya kugeuza mchezo wa kandanda kuwa vita vya kidini au kikabila, wakisema kwamba ni jambo lisilowezekana kwamba ushindi wa Ufaransa, Brazil au Argentina unaweza kuchukuliwa kuwa ushindi wa Ukristo.

Walisema hilo lisingewezekana, kwa kuzingatia mchanganyiko wa kikabila na kidini wa baadhi ya timu za taifa za soka barani Ulaya kwa mfano.

Mzozo kuhusu utambulisho wa kweli wa timu ya Morocco ni dhihirisho la hivi punde la "vita vya kitamaduni" ambavyo vimeendelea kwa miongo kadhaa katika eneo la Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati.

Utambulisho wa kitaifa umekuwa msingi wa itikadi mbili - Uislamu na Umoja wa nchi za Kiarabu- ambazo zilitawala masuala ya kisiasa katika eneo hilo kwa miongo kadhaa.

Ingawa zilikuwa na maana wakati wa mapambano ya ukombozi wa taifa, zikitanguliza mshikamano wa kijamii badala ya uhuru wa mtu binafsi, zinaonekana kupitwa na wakati na manufaa ya masuala hayo hayana umuhimu katika ulimwengu unaozidi kuwa wa utandawazi - kama vile mzozo wa mechi ya soka unavyoonyesha wazi.