Jinsi ya kutunza macho yako

.

Chanzo cha picha, Getty image

Kwa watu ambao hawana shida ya macho, huduma ya macho labda ndio jambo la mwisho kufikiria.

"Tunatumia macho yetu kuanzia dakika yanapokuwa wazi hadi yanapofunga. Yanatufanyia kazi kama mioyo yetu," anasema Sarah Maling, kutoka Chuo cha Royal cha Ophthalmologists.

"Lakini tunapokimbia, mioyo yetu hupiga kwa kasi na hatimaye tunapunguza kasi. Tofauti na moyo, hatuachi kutazama kwa sababu tu macho yetu yamechoka." "Na mara chache huwa tunafikiria kuhusu kuyafuatilia."

.

Chanzo cha picha, Lucy Owen/BBC

Mwandishi wa BBC Lucy Owen ameandika makala kuhusu macho yake kuokolewa alipokuwa akifanyiwa uchunguzi wa kawaida.

Lucy amekuwa akivaa lenzi tangu akiwa na umri wa miaka 16. Sasa akiwa na umri wa miaka 50, aligundua mwezi Juni kwamba alianza kupata mwanga mweupe mara kwa mara kwenye jicho lake la kulia.

"Haikutokea hivyo mara nyingi, labda mara moja au mbili kwa siku, na ingawa ilinigusa kama jambo lisilo la kawaida, sikukimbilia kuchunguzwa.

"Huku nikiwa karibu kutimiza umri wa miaka 52, nilitazama macho yangu na kufikiria itakuwa ni furaha ya kuwa mkubwa."

Anasema hakuwa ametembelea daktari wa macho mara kwa mara kama alivyopaswa kufanya na mara nyingi alisahau uchunguzi wa kila mwaka.

Lakini huku hali hiyo ikiendelea, hatimaye alichunguzwa macho yake na ndipo daktari wa macho alipogundua retina ya jicho lake la kulia ilikuwa katika harakati za kujiondoa na kwamba miale hiyo ilikuwa ni ishara.

.

Chanzo cha picha, Lucy Owen/BBC

Lucy alifanyiwa upasuaji wa dharura kwenye jicho lake la kulia. Operesheni hiyo ilichukua kama dakika 40. Alilazimika kuwa ndani na nje ya hospitali kwa masaa machache.

"Ilinibidi kutumia wiki iliyofuata nikiwa nimelala upande mmoja, na kisha ukawa mchezo wa kusubiri uwezo wangu wa kuona kurudi katika hali ya kawaida."

Kuona kwake kuliboreka hatua kwa hatua katika miezi iliyofuata.

Na sasa amerudi kazini.

"Ninachoweza kufikiria sasa jinsi gani nilivyo kuwa na bahati. Kwenda kwa daktari wa macho na wao kuchukua hatua ya haraka ndio kuliniokoa."

.

Chanzo cha picha, Getty Image

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Lakini upatikanaji wa wataalam wa huduma ya macho na huduma bora za afya ya macho kama zile Lucy Owen alizopata huenda zisipatikane kwa watu katika nchi maskini zaidi.

Peter Holland anaamini kuwa kuna haja ya mipango na sera za kitaifa kuhusu afya ya macho na matunzo, hasa katika nchi zenye kipato cha chini hadi cha kati.

Holland anasema: "Kwa kuongezea, tutakuwa na nia ya kuhakikisha kuwa afya ya macho inajumuishwa katika mipango ya afya ya kitaifa, lakini pia imejumuishwa ipasavyo katika sera ya afya ili kuwezesha upatikanaji wa rasilimali unazohitaji."

Takriban watu bilioni 2.2 duniani kote wana matatizo ya kuona au upofu, huku zaidi ya bilioni 1.1 wakiteseka kutokana na kasoro zinazoweza kuzuilika au zisizotibiwa, kulingana na ripoti ya 2023 ya Shirika la Kazi Duniani (ILO).

"Bila ya uwekezaji mkubwa katika hatua za kuzuia, idadi hii inakadiriwa kuongezeka, hasa katika nchi za kipato cha chini na cha kati, na katika jumuiya za kiasili na jamii za mbali."

.

Chanzo cha picha, getty image

Hatari za macho mahali pa kazi ni pamoja na, kulingana na ripoti, kuangalia wigo wa mwanga unaoonekana na usioonekana kama mionzi ya UV "ambayo inaweza kusababisha mtoto wa jicho" kwa wafanyikazi.

Hivyo, kazi imekuwa sababu kuu ya tatu ya hali zinazohusiana na matatizo ya macho.

Ripoti hiyo pia inasema: "Zana zinazofaa za ulinzi zinahitajika kwa wafanyakazi walio katika hatari ya kiwewe cha mitambo, kama vile chembechembe zinazoruka [ambazo] hugonga au kupenya kwenye jicho kwa mwendo wa kasi na/au kwa joto la juu."

Na mwisho kabisa, pia kuna tatizo la kipekee kwa wafanyikazi wa kisasa: shida ya macho ya skrini ya kompyuta.

"Watu mara nyingi hudumisha umbali tuli kati ya macho yao na skrini, na kusababisha misuli ya macho kudumisha mkunjo usiobadilika," ripoti hiyo inasema.

"Tabia hizi za matumizi ya kompyuta zinaweza kusababisha matatizo yanayohusiana na macho na kuona."

Jinsi ya kutunza macho yako bila gharama ya ziada:

Fanya uchunguzi wa macho ili kuangalia afya ya macho yako

Ikiwa kuna tofauti yoyote muhimu kati ya macho yako, hiyo inaweza kuwa ishara kwako kuwa una tatizo

Ikiwa una watoto chini ya umri wa miaka saba na huna uwezo wa kupata huduma ya macho, unaweza kumwambia atazame mbali kwa macho yote mawili

Unaweza kupata matatizo kama vile amblyopia, ambayo ni kupungua kwa uwezo wa kuona kwa watoto, na kutafuta usaidizi

Kumbuka kitu muhimu kwa afya ya macho ni namna ya kuzuia matatizo

Vidokezo vya namna ya kutunza macho kutoka kwa Sarah Maling, Chuo cha Royal cha Ophthalmologists