Mwanasiasa wa Uingereza aliyedanganya kuhusu kifo chake

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati nguo za John Stonehouse zilipopatikana kwenye rundo la taka kwenye ufuo wa Miami tarehe 20 Novemba 1974, watu wengi walidhani kwamba Mbunge huyo wa Uingereza alikuwa amekufa maji alipokuwa akiogelea - hadi alipoonekana Australia akiwa hai na mwenye afya katika mkesha wa Krismasi. Makala hii ya Historia inaangazia hadithi isiyo ya kawaida ya mtu aliyekufa mara mbili.
John Stonehouse alipopanga mpango wake wa kutoweka kabisa, alikuwa mtu mwenye matatizo.
Kazi yake ya kisiasa ilikuwa imekwama, shughuli zake za kibiashara za kukwepa zilimwacha akikabiliana na uharibifu wa kifedha, alishutumiwa kuwa jasusi wa kikomunisti, na alikuwa na uhusiano wa nje ya ndoa na katibu wake.
Katika hatua iliyoigwa kutoka kwa riwaya ya Frederick Forsyth,The Day of the Jackal, Stonehouse iliiba utambulisho wa watu wawili waliokufa.
Alisafiri kwa safari ya kikazi hadi Miami ambapo alitoweka, mnamo Novemba 1974, kisha akaruka kwa ndege nyingine hadi Australia. Ujanja huo ulidumu zaidi ya mwezi mmoja. Alikuwa mfalme wa Uingereza Bwana Lucan, mkimbizi mwingine asiyejulikana ambaye alitoweka karibu wakati huo huo, ambaye angemwongoza bila kukusudia kukamatwa huko Australia.
Na Stonehouse alielezeaje matendo yake? Mbunge huyo wa Uingereza alisisitiza kwa BBC mnamo Januari 1975 kwamba alikuwa kwenye "ziara ya kutafuta ukweli, sio tu katika suala la jiografia lakini kwa hali ya ndani ya mnyama wa kisiasa".
Kwa jamii ya Uingereza mwishoni mwa miaka ya 1960, alionekana kama mtu ambaye alikuwa amefikia kila kitu maishani.
Akiwa na umri wa miaka 43 tu alikuwa mkuu wa shirika la posta, ana mke na watoto watatu na alikuwa anapigiwa upatu kuwa waziri mkuu mtarajiwa wa chama cha Leba. Alisimamia kuanzishwa kwa stempu za daraja la kwanza na la pili, lakini kwa taaluma yake ya kisiasa, jukumu hilo lilikuwa na ushawishi wowote.
Mambo yalibadilika wakati mkaidi kutoka Czechoslovakia ya kikomunisti alipodai mwaka 1969 kwamba nchi hiyo ilikuwa imemuajiri mbunge huyo kama jasusi.
Stonehouse alipinga madai hayo na kujitetea kwa Waziri Mkuu Harold Wilson, ambaye alimuamini. Madai kama hayo yalikuwa yakijitokeza sana wakati wa Vita Baridi, lakini sifa ya kisiasa ya Stonehouse iliharibiwa.
Chama cha Labour kiliposhindwa katika uchaguzi mkuu wa 1970, hakukuwa na kiti cha Stonehouse kwenye safu ya mbele ya upinzani. Baada ya kukatishwa tamaa, aliamua kutumia muda zaidi kwa masilahi yake ya kibiashara ya London - hasa huduma za kuuza nje alizokuwa ametengeneza kupitia mtandao wake wa kimataifa.
End of Soma pia:
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Aliombwa kusaidia kuanzisha Mfuko wa British Bangladesh Trust, benki ambayo ingetoa huduma kwa watu wa Kibengali nchini Uingereza.
Lakini jinsi benki hiyo ilivyokuwa ikiendeshwa baadaye ilitoa maoni muhimu kutoka kwa gazeti la Jumapili na kuvutia wachunguzi kutoka Kikosi cha kukabiliana na ulaghai na Idara ya Biashara na Viwanda huko London.
Maswali yaliyoibuliwa na vyombo vya habari dhidi ya Stonehouse yalimuathiri sana kiasi cha kupoteza heshima miongoni mwa wabunge wenzake.
Hali hiyo ilimfanya kuingiwa na wazo la kutafuta njia ya kujiondoa kwenye sakata hiyo. Kwanza, alighushi ombi la pasipoti kwa jina la Joseph Arthur Markham, mfanyakazi wa kiwanda ambaye alikuwa amefariki hivi majuzi katika eneo bunge lake la Walsall, katika Midlands Magharibi mwa Uingereza.
Aligeuza utambulisho huu mpya kuwa mshauri wa uuzaji nje wa globetrotting na akaunti za benki huko London, Uswizi na Melbourne. Kisha akaanzisha utambulisho mwingine kwa jina la Donald Clive Mildoon, ambaye pia alikuwa amekufa huko Walsall. Ili kusaidia kufadhili maisha haya mapya, Stonehouse alihamisha kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa biashara zake hadi kwenye akaunti kadhaa za benki.
'Utambulisho mseto'
Mnamo tarehe 20 Novemba 1974, Stonehouse alitoweka wakati, ilipokuwa, akiogelea baharini huko Miami, Florida. Mtu huyo wa miaka 49 hakuwahi tena kuonekana isipokuwa nguo alizoziacha ufukweni. Je, alikufa maji akiogelea bahari? Je, aliuawa na kutupwa ndani ya jengo lililokuwa karibu na ufukwe wa Miami? Je, alikuwa ametekwa nyara?
Mkewe Barbara hakuwa na shaka kwamba alikumbwa na ajali mbaya. Aliiambia BBC News: "Nimesikia uvumi usio wa kawaida na wote hauna msingi. Sina shaka kuwa alikufa maji kwa sababu ishara zote zinaonyesha kwamba alizama."
Huko London, polisi walikuwa na mashaka yao. Sheila Buckley, katibu na mpenzi wa siri wa Stonehouse mwenye umri wa miaka 28, aliendelea kusisitiza kwa marafiki kwamba alikuwa amekufa, lakini alijua hadithi halisi: baadhi ya nguo zake zilikuwa zimepakiwa kwenye sanduku na kusafirishwa hadi Australia mwezi mmoja kabla, alipokea simu kutoka kwake, na pia alikuwa amemtumia barua kisiri kupitia moja ya benki zake mbili za Australia.
Ilikuwa kuwa na akaunti hizo mbili za benki kwa majina tofauti, Markham na Mildoon, ambayo hatimaye iliwaelekeza polisi wa Melbourne kuanza kumfuatilia.
Wakati huo, walikuwa wakimtafuta mtu kwa jina Lord Lucan, ambaye alitoweka mnamo Novemba 8 baada ya kumuua kijakazi wa watoto wake. Hapo awali, polisi walidhani kwamba Muingereza huyo aliyeonekana akitia saini hundi zilizotiliwa shaka huenda ni yeye.
Wakati kutoweka kwa Lucan kumeendelea kuwahangaisha polisi kwa miaka 50, siri ya Stonehouse ilidumu zaidi ya mwezi mmoja. Siku ya mkesha wa Krismasi, Stonehouse alilazimika kukiri utambulisho wake halisi. Baadaye, katika makao makuu ya polisi ya Melbourne, aliuliza ikiwa angeweza kumpigia simu mke wake huko Uingereza. Ingawa hakutambua wakati huo, mazungumzo ya simu ambayo yaliangazia kisa hicho yalirekodiwa.
Alisema: "Habari mpenzi. Naam, wamebaini nilikuwa natumia utambulisho wa uongo. Ukweli ni kwamba nimekuwa nikikudanganya. Samahani kwa hilo, lakini nashukuru hatimaye yote yamekwisha." Stonehouse alishikiliwa kwa siku chache kabla ya kuunganishwa na familia yake, nchini Australia na baadaye na mpenzi wake.
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi na kuhaririwa na Yusuf Jumah












