Mwanaume aliyeiba ndege ili kukutana na mkewe

th

Kwa miaka miwili, mwandishi wa BBC Emma Jane Kirby amekuwa akichunguza kisa cha Paul Meyer, fundi wa Marekani, ambaye alipiga moyo konde na kuiba ndege kutoka kwa Jeshi la Anga la Marekani huko Uingereza mnamo 1969, na akaruka kwa ndege hiyo hadi Virginia, kwa nia ya kukutana na mkewe.

Bw Meyra aliyekuwa mwanajesi katika Jeshi la Wanahewa la Marekani, alikuwa ndani ya ndege wakati yeye na mkewe walipofunga ndoa hivi majuzi.

Saa 2 hivi baada ya kuwa angani, ghafla alitoweka katika eneo la English Channel , asionekane tena.

th

Iligundulika kuwa alitoroka kwa sababu ya mkewe wakati sauti yake ilisikia simu ikiita.

Paul, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 23, alimwamsha mke wake, Jane Goodson, na kusema: "Mpenzi, ninaruka kwa ndege na ninarudi nyumbani."

Niliiba ndege mwenyewe

Hadithi ya Paul Meyer ilisomwa na Mholanzi Theo Van Eijck, ambaye alisema yeye mwenyewe aliiba ndege wakati akifanya kazi na jeshi. Lakini aliishi ili kuweza kusimulia hadithi hiyo

th
Maelezo ya picha, Theo Van Eijck akiwa nyumbani kwake Somerset

Baada ya Theo Van Eijck kufukuzwa kutoka mafunzo ya urubani na jeshi la wanamaji la Uholanzi mwaka wa 1964, aliiba ndege na kuipeleka Libya, aliambia BBC.

Theo Van Eijck, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 76 akiwa na mvi , aliionyesha BBC picha yake pamoja na gazeti la Uholanzi mwaka 1964 lililoandika kisa cha ajali hiyo ya ndege.

Alikuwa na umri wa miaka 21 wakati huo na alikuwa amesafiri kwa ndege hadi Benghazi, Libya.

Nini sababu ya kitendo cha Van Eijck?

th

"Yote yalianza vizuri, niliongezwa kwenye timu ya wanamaji kwa ajili ya mazoezi ya urubani, na nilikuwa na shauku kubwa ya kupanda ndege," alisema Theo Van Eijck.

Mchakato wa mafunzo umeanza na anaboreka katika misheni yake mpya.

Lakini kulingana na BBC, alitapeliwa na wakufunzi wake kwenye tafrija, ambapo aliuliza kuhusu malalamishi yao kuhusu jinsi mafunzo hayo yalivyokuwa yakiendelea na aina ya ndege waliyokuwa wakifunza.

Pia alizungumza ukweli kuhusu malalamiko yake yote na alitumaini kwamba mambo yangeboreka.

Siku iliyofuata, hata hivyo, kadi yake ya mazoezi iligongwa mhuri kuonyesha kwamba hakuwa mzuri katika kurusha ndege na kwamba alikuwa katika hatari ya kushindwa ikiwa angesafirishwa.

Alishtushwa na hatua hiyo, na moja kwa moja akahisi haikuwa ya haki.

Alijaribu kuwasilisha malalamiko yake kwa maafisa wakuu, lakini juhudi zake zilishindwa

Siku iliyofuata aliandika maneno kwenye ubao wa akionyesha hasira yake na dhuluma aliyosema ametendewa.

Tukio hilo lilimfanya akamatwe kwa siku mbili mwishoni mwa juma, lakini akatoroka gerezani.

Ilipogundulika kuwa alitoroka gerezani alisimamishwa mafunzo yote ya urubani.

"Ninatoka katika familia kubwa ya watoto 12, sote tunajua kipi ni kizuri na kipi si sahihi, na kilichofanyika kilikuwa kibaya," alisema akikumbuka wakati huo.

Akiwa amechanganyikiwa na ndoto yake iliyovunjika ya kuwa rubani, Van Eijck aliomba kuondolewa kwenye kikosi cha wanamaji, lakini ombi lake lilikataliwa mara kwa mara.

Kisha akaanza kutafuta njia ya kutoroka kutoka kwa jeshi la wanamaji.

TH

Chanzo cha picha, ANP

"Sikumwambia mtu yeyote kuhusu mipango yangu, kwani ningewaambia nisingeweza," alisema huku akitabasamu.

Kama vile Paul Meyer alivyofanya, Theo van Eijck aliamua kuiba ndege ili kujipa uhuru wake.

Alipata kitabu cha mafunzo ya urubani kutoka kwa mojawapo ya ndege za Jeshi la Anga la Netherlands, na akakificha kwenye sanduku lake.

Wakati wowote marafiki zake walipolala, au kwenda matembezini, angesoma kitabu hicho kwa siri, peke yake.

Pia alifanya urafiki na marubani waliofaulu na kuzungumza nao kuhusu jinsi ya kurusha ndege, jinsi ya kuwasha injini yake na jinsi ya kuiweka angani.

"Hakujua kwa nini nilipenda kujifunza ujuzi huu wote," alisema.

Aliogopa kwamba ikiwa angeruka kutoka Uholanzi angeenda Ujerumani Mashariki, ambayo wakati huo ilikuwa adui wa nchi yake.

Lakini siku moja bahati yake ikasimama

TH

Akikumbuka , alisema: "Walituomba baadhi yetu kufanya mazoezi na jeshi la wanamaji la Uingereza kwenye kisiwa cha Malta kwa muda wa miezi miwili, na nilifikiri kama ningeweza kufika Malta ningeweza kuruka na kwenda popote".

Alijiunga na jeshi ambalo lilikubali kwa hiari kwenda Malta kwa mafunzo.

Alifanikiwa kuteka nyara ndege ya jeshi la anga na kuruka kuelekea Libya, ikipitia Bahari ya Mediterania.

Aliondoka na alitaka kutua katika uwanja wa ndege wa Tripoli lakini wanajeshi wa Uingereza walikuwa bado wanadhibiti uwaja huo.

Hivyo akageukia Benghazi, ambapo alitua.

Theo van Eijck alifurahishwa sana na jinsi alivyotua kwenye ndege, na akafikiri kwamba walimu wake wangefurahi kumuona.

Alijasalimisha kwa jeshi la Libya, na mazungumzo kufanywa kati ya Libya na Uholanzi.

Hatimaye Theo van Eijck alikubali kurejeshwa nchini na kuhukumiwa kifungo cha miezi 12 jela kwa vitendo vyake. Badala yake iliahidiwa kwamba angeondolewa kwa heshima kutoka kwa jeshi la wanamaji.

th

Chanzo cha picha, Alamy