Wizi mkubwa wa benki uliowashangaza wapelelezi wa Scotland Yard

h

Chanzo cha picha, Gettty Images

Muda wa kusoma: Dakika 7

Ilikuwa ni mwaka 1971. Kundi la watu lilifanya wizi wa benki uliosababisha hofu kubwa katika historia.

Wafanyakazi wenye kipaji, wapole wenye uhusiano na wahalifu walipanga njama ya wizi mwishoni mwa juma wakihamasishwa na hadithi ya filamu ya Sherlock Holmes.

Walivunja chumba cha benki, ambapo pesa zilihifadhiwa salama, na kuanza kutoa pesa kutoka kwenye mamia ya masanduku ambapo pesa na vitu vya thamani vilihifadhiwa. Wakati huo huo, mtu alikuwa akisikiliza mazungumzo yao katika chumba cha kudhibiti siri cha kuhifadhia pesa kupitia redio za mazungumzo walizokuwa wakitumia.

Upande mwingine wa chumba salama, polisi wa ulinzi walikuwa wamesimama, na walihusika katika wizi huo. Hakuna mtu aliyeonekana kuingia na kuona kile kilichokuwa kinaendelea.

Jinsi gani wizi wa benki katika moja ya sehemu salama zaidi ya nchi unaweza kusababisha Lloyds Bank kutangaza kufungwa kwa muda kwa tawi lake la Baker Street huko London? Ni kwa jinsi gani hata leo kesi hiyo bado ni kesi isiyotatuliwa kabisa?

Mwezi Mei mwaka huo, mwanaume mwenye umri wa miaka 60 kwa jina Benjamin Wolfe alikodisha duka hilo.

Benjamin alikuwa na hamu ya kununua duka hilo kwani lilikuwa na milango miwili mbali na Lloyds Bank.

Kabla ya hapo, mnamo Desemba 1970, tajiri mmoja alifungua akaunti ya benki katika benki hiyo iliyopo Baker Street na kuweka £ 500 ambazo ni sawa na (£ 6,000) wakati huu.

Kisha akakodisha 'sanduku la kuweka' pesa hizo kwenye chumba cha siri cha kuhifadhia pesa..

Kama wateja wengine matajiri wa benki, mara nyingi alijaribu kupata sanduku lake la amana kwenye chumba hicho.

Tofauti na wengine, mtu huyo alihesabu urefu na upana wa chumba cha siri cha kuhifadhi pesa za benki kwa kutumia mwavuli aliobeba.

Wengine pia wamechangia kwa wizi kwa nyakati tofauti.

Katika kipindi hicho cha majira ya kiangazi , kelele za ukarabati wa barabara zilisababisha mtetemo na kulia kwa ving’ora vya tahadhari za maduka kama ishara za onyo, na watu wengi walisimamisha kwa muda kufuatia operesheni ya ving'ora hivyo.

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Walinzi waliingia benki na kukagua chumba cha kuhifadhi pesa ndani ya benki

Nani alihusika katika wizi huo?

Awali, Brinks - Matt na Brian Reeder, ambao walihusika katika wizi wa Hatton Garden, walidhaniwa kuwa walipanga wizi huo pia. Lakini hadi wakati huu maelezo kamili ya watu waliohusika katika tukio hili la wizi hayajapatikana.

Reeder, ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 84 baada ya kukutwa na mali yenye thamani ya £22m katika mfululizo wa wizi, alisema hakuhusika katika wizi wa benki.

Watu wanne, akiwemo Anthony Gavin, ambaye aliongozwa na Benjamin na Reeder, walikamatwa na kufungwa mwaka 1973 kuhusiana na wizi huo.

Watu wengine wanne, akiwemo mwanamke aliyehusika katika wizi huo, walitoroka bila kujeruhiwa.

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, SAC ilikuwa na maduka mawili mbali na benki ya bidhaa za ngozi

Uvumi na habari nyingi ambazo hazijatolewa

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mbali na utambulisho wa wezi, maswali mengi bado hayajajibiwa kuhusu ni kiasi gani kiliporwa kutoka kwa benki hii.

Inaripotiwa kuwa kati ya pauni nusu milioni na pauni milioni 3 zinaweza kuwa ziliibiwa. Leo inakadiriwa kuwa pesa zilizoibiwa zina thamani ya kati ya £ 6 milioni na £ 40 milioni.

Kiasi kidogo sana cha fedha kilipatikana. Hakuna maelezo juu ya kile kilichotokea kwa pesa zote.

Data zote na taarifa zinazohusiana na kesi hii zinahifadhiwa katika kituo cha taifa cha uhifadhi wa hati. Taarifa hii ni siri ' ili kwamba hakuna mtu anaweza kuipata hadi mwaka 2071.

Je, ni kweli kwamba moja ya masanduku ya amana yaliyoibiwa pia yalikuwa na picha za karibu za Bintimfalme Margaret?

Kavin alishutumiwa kwa kuja na mpango huu baada ya kusoma kitabu The Red-Headed League na Sherlock Holmes.

Shujaa wa hadithi yuko kwenye chumba cha siri cha benki cha kuhifadhi pesa akisubiri wezi kufika.

Benjamin, Gavin, Reginald Tucker na Thomas Stephen wote walihusika katika wizi huu. Ni Reginald Tucker ambaye aliingia kwenye chumba cha kuhifadhi fedha cha benki na kupima nafasi nzima kwa mwavuli.

Bobby Mills na Mike Gervais pia wanaaminika kuhusika katika wizi huo, .

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Polisi wakifanya uchunguzi

Stephen alitoa vifaa muhimu kwa ajili ya wizi huu. Pia alitumia vilipuzi na kemikali ya mafuta ambayo huyeyusha chuma na oksijeni kwa ajili ya wizi huu.

Kwa miezi kadhaa walitumia muda wao kuchimba handaki la futi 40 katika eneo hili. Udongo na mawe yaliyofukuliwa kutoka kwenye mgodi wa shimo hilo yaliwekwa kwenye masanduku ya plastiki na kutolewa nje usiku wakati hakuna mtu aliyekuwa akiangalia.

Mills anaendelea kufuatilia nani yuko nje. Wakati huo, watu wengine walikuwa wameingia katika chumba cha kuhifadhia fedha.

Waliingia kwenye chumba hicho cha siri kwa kutumia mlipuko unaoitwa Kelignite.

Walifanikiwa kuingia kwa urahisi katika chumba hicho kwani kelele za mlipuko huo hazikusikika kutokana na msongamano wa magari.

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wezi walichimba handaki chini ya duka la bidhaa za ngozi

Mtu aliyesikia mazungumzo ya wezi

Wakati walipokuwa wakitekeleza wizi huo, mtu aliyekuwa akisikiliza Redio Luxembourg alikuwa akisikiliza mazungumzo yote yaliyotokea wakati wa wizi kwenye redio yake. Jina lake halisi ni Robert Rowlands.

Kwenye redio yake ya mawasiliano, alikuwa akisikiliza kila kitu ambacho wezi walikuwa wakizungumza kwenye chumba cha siri cha kuhifadhi pesa cha benki moja kwa moja.

Aliwasikia wezi wakijadili ikiwa watapumzika au la wakati moshi ukienea katika chumba cha siri kutokana na milipuko. Pia alisikia kwenye redio yake kwamba mmoja wa wezi hao aliomba chai na mkate wa sandwichi.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Robert Rowlands (kushoto) alikuwa akisikiliza moja kwa moja kile ambacho wezi walikuwa wakikisema katika chumba cha kuhifadhi pesa cha benki

Robert alikuwa amewasikia wakisema kwamba walikuwa na maelfu mengi, na kwamba walipaswa kwenda huko tena kwa mahitaji mengine. Lakini alidhani wizi huo ulikuwa unafanyika katika duka la sigara na walikuwa wakizungumzia kuhusu ni sigara ngapi walikuwa wameiba.

Aliwaeleza polisi wa eneo hilo, lakini walipuuza. Kisha Robert aliwajulisha polisi wa Scotland Yard, ambao walianza kufuatilia.

Waliamua kutumia 'gari la kufuatilia ishara ya redio za mawasiliano.

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Benki haijakubali kuhusika na wizi huu

Polisi wa Scotland Yard

"Siku iliyofuata, mameneja wa benki na wafanyakazi waliitwa kufungua benki wikendi . Polisi walioingia na walinzi walijitokeza wakiwa na uhakika kwamba hakuna uharibifu wowote uliotokea kwenye chumba hicho. Walifunga milango ya kuingilia ya benki na wezi waliosimama nyuma ya milango ya chumba cha kuhifadhi fedha walipumua kwa pumzi ya chini . Waliposikia sauuti walitambaa kupitia handaki la futi 40 ." Gazeti la Times liliripoti.

Wafanyakazi wa benki hiyo ambao walirejea kazini siku ya Jumatatu walisema waligundua kuwa chumba cha kuhifadhi fedha hakikuwa sawa.

Kamanda wa ulinzi Robert Hundley wa Scotland Yard alisema, "Tulikosolewa na umma bila kutarajia. Walitutuhumu kwa kuwa wazembe."

Tulipoingia ndani ya benki na maafisa wa usalama, chumba cha kuhifadhi pesa kilikuwa kimefunguliwa. Lakini hakuna mtu aliyefikiria kwamba wangekuja upande mwingine wa chumba. Wapelelezi 120 walifanya kazi katika kesi hiyo.

Hundley alisema kwamba tulikuwa tunapata taarifa kuhusu watu waliohusika katika wizi huo wanaweza kuwa nani.

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waandishi wa habari wafikishwa mbele ya benki

Katika kesi hiyo, mtu mmoja baada ya mwingine alianza kunyooshewa vidole kwamba alihusika na uhalifu huu.

Polisi wa Scotland Yard waliwalaumu maafisa wa usalama kwa uzembe. Maafisa wa ulinzi walijibu kwa kuwatuhumu wafanyakazi wa Scotland Yard kwa kuhakikisha kuwa wadadisi wao 'walifanya kazi vizuri'.

Ofisi ya Posta, ilidai, ingeweza kuwakamata wezi hao kama wangechunguza simu kwa wakati.

Pia walihoji kwa nini polisi hawakuvamia duka la bidhaa za ngozi lililo karibu. Kama lingekuwa limepekuliwa vizuri, polisi wangeweza kuwapata watu wakifungua masanduku 286 ya kuhifadhia pesa na ya kuibia, walisema.

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mtaa wa Baker

Filamu ya 'The Bang Job' ya mwaka 2008 ilitokana na tukio hilo.

Njama hiyo inahusu mtu anayeitwa Michael X, mkuu wa kikundi cha silaha cha Trinidad, ambaye aliweka picha za kibinafsi za Bintimfalme Margaret kwenye sanduku la amana la benki na Idara ya Usalama ya Uingereza inajaribu kuzirejesha.

Pia kulikuwa na uvumi kuhus ushiriki wa Reader katika wizi huo. Kwahiyo, rafiki wa Reeder alikuwa ametaja kwamba Reeder alikuwa amehusika katika wizi huu na kwamba alikuwa amepata picha za kiongozi wa kisiasa akiwanyanyasa watoto katika benki.

Baadaye, Reeder alidaiwa kuacha picha hizo sakafuni ili polisi wazione. Lakini hakuna ushahidi wa kuthibitisha hilo.

Serikali imetoa ilani inayoitwa DSMA ambayo inakataza usambazaji wa habari za umma zinazohusiana na jeshi la Uingereza na huduma za ujasusi. Kutokana na sababu hii, kulikuwa na uvumi kwamba hakukuwa na habari kuhusu wizi huu katika magazeti.

Lakini taarifa kama hizo hazitolewi kuzuia kutolewa kwa habari kuhusu wizi huo ambao tayari umeishafanyika.

Kwakweli, maslahi katika suala hili yamepungua. Hata hivyo, magazeti ya kitaifa na kikanda yaliendelea kutoa taarifa kuhusu suala hilo.

Uvumi kama huo huenda ulisambaa baada ya Robert Rowlands kujaribu kutoa taarifa kwa gazeti moja kwa njia ya simu na polisi wakaichukua na kumwambia mhariri kwamba hakuruhusiwa kuitoa.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jengo la Lloyds Bank

Akikumbuka miaka hii baadaye, Rowlands alisema polisi huenda walitenda kwa njia hii ili kuficha uzembe wao.

Ni nini hasa kilichotokea mwishoni mwa wiki hii? Ni nini kwenye hati ya kurasa 800 kwenye kumbukumbu za kitaifa? Hakuna mtu anayeweza kuifikia miaka 47.

Je ni nini Lloyds Bank inasema kuhusu suala hilo?.

Iliwataka watu ambao walikuwa na akaunti za benki huko kupata bima kwa masanduku yao salama ya amana. Lakini ilikataa kuwajibika kwa wizi huo.

Hata kwa wizi mkubwa kama huo, benki ilisema, "Ni kawaida kwa wezi kupitia chumba cha chini ya jengo."

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Seif Abdalla