Kwa nini Urusi inachoma gesi ya hadi dola milioni 10 kwa siku huku bei ya nishati ikipanda?

Gesi

Chanzo cha picha, OPERNICUS SENTINEL/SENTINEL HUB/PIERRE MARKUSE

Gharama ya nishati barani Ulaya inapoongezeka, Urusi inateketeza kiasi kikubwa cha gesi asilia, kulingana na uchambuzi ulioonekana na BBC.

Uchambuzi huo unaonyesha kuwa kiwanda cha gesi cha Urusi karibu na mpaka wa Finland kinachoma gesi ya thamani ya dola milioni 10 kila siku.

Wataalamu hao wanathibitisha kuwa, miezi sita iliyopita; Kwa maneno mengine, kabla ya Moscow kuzindua uvamizi wake dhidi ya Ukraine, sehemu kubwa ya gesi hii ilisafirishwa kwenda Ujerumani.

Balozi wa Ujerumani nchini Uingereza aliiambia BBC kuwa Urusi ilikuwa inateketeza gesi hiyo, kwa sababu "haiwezi kuuzwa kwingine".

Vikwazo vya kimataifa vilivyowekwa dhidi ya Urusi, kwa msaada wa mamlaka ya Ujerumani, na uamuzi wa Umoja wa Ulaya (EU) wa kupunguza utegemezi wake kwa mauzo ya nishati ya Urusi imefanya serikali ya Vladimir Putin kushindwa kuuza gesi yote inayozalisha.

Moto usio wa kawaida

Uchambuzi wa shirika la ushauri wa nishati la Rystad Energy unaonyesha kuwa mtambo mpya wa gesi asilia ya Portovaya (LNG), kaskazini-magharibi mwa St. Petersburg, unateketeza takriban mita za ujazo(cubic metre) milioni 4.34 kwa siku.

Onyo la kwanza lilitolewa na wakazi wa Finland wanaoishi karibu na ambao walielezea kuona kwa mbali moto mkubwa usio wa kawaida.

Portovaya iko karibu na kituo cha mwanzoni mwa bomba la Nord Stream 1, ambalo husafirisha gesi chini ya bahari hadi Ujerumani.

Usambazaji wa gesi kupitia bomba hilo umesitishwa tangu katikati ya mwezi Julai.

Warusi wanahusisha hali hiyo na matatizo ya kiufundi, lakini Ujerumani inasema kuwa ni hatua ya kulipiza kisasi vikwazo walivyowekewa.

Urusi

Chanzo cha picha, ARI LAINE

Maelezo ya picha, Moto kutoka kwa mtambo wa Portovaya wa Urusi unaweza kuonekana kutoka kilomita kadhaa, kama inavyoonekana kwenye picha hii iliyopigwa na raia wa Finland.

Lakini tangu Juni, watafiti wamebainisha ongezeko kubwa la joto linalotokana na kituo hicho - kinachofikiriwa kuwa ni kutokana na kuwaka kwa gesi, uchomaji wa gesi asilia.

Ingawa kuchoma gesi ni jambo la kawaida katika viwanda vya kuchakata - kwa kawaida hufanywa kwa sababu za kiufundi au za usalama - ukubwa wa uchomaji huu umewachanganya wataalam.

‘’Sijawahi kuona mtambo wa LNG ukiwaka sana,’’ Dk Jessica McCarty, mtaalam wa data ya satelaiti kutoka Chuo Kikuu cha Miami huko Ohio.

‘’Kuanzia karibu Juni, tuliona kilele hiki kikubwa, na hakikuisha. Kimebakia kuwa juu sana,’’ aliongeza.

Hakuna wanunuzi

Balozi wa Ujerumani nchini Uingereza, Miguel Berger, aliihakikishia BBC kwamba uchomaji huo usio wa kawaida ni uthibitisho kwamba juhudi za Ulaya za kupunguza utegemezi wa gesi ya Urusi "zina athari kubwa kwa uchumi wa Urusi."

"Hawana maeneo mengine ya kuuzia gesi yao, hivyo wanalazimika kuichoma," alisema.

Kwa upande wake, Mark Davis, Mkurugenzi Mtendaji wa Capterio, kampuni inayojitolea kutafuta suluhisho la kuchoma gesi, alikubali kuwa hali hiyo ni uamuzi wa makusudi uliofanywa kwa sababu za kiutendaji.

"Mara nyingi waendeshaji wanasitasita kufunga mitambo kwa kuhofia kuwa itakuwa vigumu kiufundi au ghali kuanzisha, na pengine huenda wanazingatia hilo," aliiambia BBC.

Urusu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uchomaji wa gesi ni jambo la kawaida katika mitambo ya kusafisha mafuta, kama inavyoonekana kwenye picha hii, lakini kile kimekuwa kikifanyika katika mtambo huu Urusi si cha kawaida sana, kulingana na wataalam.

Dhana nyingine inaashiria kuwa mwako wa gesi unaweza kutokana na matatizo ya kiufundi katika kushughulikia kiasi kikubwa cha mafuta ambacho kilitumwa kupitia bomba la gesi la Nord Stream 1.

Kampuni ya Urusi ya Gazprom ingejaribu kutumia mafuta kutengeneza LNG katika mtambo mpya, lakini huenda ilikabiliwa na changamoto ya kuishughulikia ndiposa imeamua kuichoma.

"Aina hii ya uchomaji moto kwa muda mrefu inaweza kumaanisha wanakosa baadhi ya vifaa," alisema Esa Vakkilainen, profesa wa uhandisi wa masuala ya nishati katika Chuo Kikuu cha LUT nchini Finland.

"Kwa sababu ya vikwazo vya biashara, Urusi haiwezi kutengeneza vali za ubora wa hali juu ambazo zinahitajika katika usindikaji wa mafuta na gesi. Kwa hiyo huenda wana vali zilizovunjika na hawawezi kuzibadilisha," alisema.

Maonyesho ya uwezo

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mwenge mkubwa wa moto ambao raia wa Finland wanaweza kuona kutoka upande wao wa mpaka pia umekuwa onyesho la nguvu ya Urusi.

"Ingawa sababu halisi za kuwaka kwa moto huo hazijulikani, eneo la moto huo ni ukumbusho unaonyesha utawala wa Urusi katika masoko ya nishati ya Ulaya," alisema Sindre Knutsson wa Rystad Energy.

"Hakna ishara wazi zaidi ya hii: Urusi inaweza kupunguza bei ya nishati hata kesho. Hii ni gesi ambayo vinginevyo ingesafirishwa kupitia Nord Stream 1 au njia nyingine mbadala," alisema.

Bei ya nishati ya kimataifa imekuwa ikipanda baada ya amri ya kutotoka nje iliyowekwa ili kudhibiti maambukizi ya Covid-19 na baadaye kurejelewa kwa shughuli za kiuchumi kwa mkumbo.

Sehemu nyingi za kazi, tasnia na burudani ghafla zilihitaji nguvu zaidi kwa wakati mmoja, na kuweka shinikizo ambalo halijawahi kufanywa kwa wauzaji.

Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine ulisababisha kupanda tena kwa bei, ambayo ilichangiwa na vikwazo vlivyowekwa na Marekani, Umoja wa Ulaya (EU) dhidi ya Moscow kulipiza kisasi kwa uchokozi dhidi ya jirani yake.

Serikali za Ulaya zimetumia miezi michache iliyopita kutaka kupunguza utegemezi wao wa nishati kwa Urusi, ambayo hadi wakati huo ilitoa 40% ya gesi inayotumiwa na EU.

Bei za vyanzo mbadala vya gesi zimepanda, na baadhi ya nchi za EU, kama vile Ujerumani na Uhispania, zinachukua hatua za kuokoa nishati.

Pigo kwa mazingira

Mazingira

Chanzo cha picha, Getty Images

Wanasayansi pia wana wasiwasi juu ya athari kuchoma gesi ya mazingira, haswa kiasi kikubwa cha kaboni na mashizi inayotengeneza, ambayo inaweza kuzidisha kuyeyuka kwa theluji ya barafu ya Arctic.

Kulingana na watafiti, kuchoma ni bora zaidi kuliko kutoa methane tu, ambayo ni kiungo kikuu cha gesi, na ni mchangiaji mkuu hali joto.

Lakini pamoja na kutoa takriban tani 9,000 za gesi chafu kila siku uchomaji wa gesi una madhara mengine makubwa.

Mkaa mweusi ni jina linalopewa chembe za mashizi ambazo hutolewa na mwako usio kamili wa nishati kama vile gesi asilia.

"Carbon nyeusi inayotolewa kaskazini huwekwa kwenye theluji na barafu, ambayo huharakisha kuyeyuka," alisema Profesa Matthew Johnson wa Chuo Kikuu cha Carleton nchini Canada.