Kwa nini bei ya gesi duniani imepanda sana?

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Bei ya gesi Ulaya sasa iko juu mara 10 zaidi ya kiwango chao cha wastani katika muongo mmoja uliopita.

Mwezi Februari 2021 gesi ya Uingereza ilikuwa ikiuzwa kwa 38p kwa therm (kipimo cha matumizi ya gesi). Mwezi huu ilifikia 537p kwa therm. Je ni nini kinachosababisha bei hizo kuwa juu?

Ni nini kimetokea mwaka uliopita?

Bei ya nishati kote ulimwenguni ilipanda sana baada ya vizuizi vya Covid kuwekwa na uchumi uliporudi katika hali ya kawaida maeneo mengi ya kazi, viwanda na burudani yote yalikuwa yanahitaji nishati zaidi kwa wakati mmoja, na kuweka shinikizo kubwa kwa wasambazaji.

Bei ziliongezeka tena Februari mwaka huu, baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Serikali za Ulaya zilitafuta njia za kuagiza nishati kidogo kutoka Urusi, ambayo hapo awali ilikuwa inatoa 40% ya gesi iliyotumiwa katika Umoja wa Ulaya. Matokeo yake bei za vyanzo mbadala vya gesi zilipanda.

EU imeahidi kupunguza utegemezi wake kwa gesi ya Urusi na mwezi Julai nchi wanachama zilikubali kupunguza matumizi ya gesi kwa 15%.

Ujerumani, kwa mfano, ilikuwa ikiagiza 55% ya gesi yake kutoka Urusi kabla ya uvamizi wake nchini Ukraine. Sasa imeshuka hadi 35% na ina mpango wa muda mrefu wa kuacha kuagiza kutoka Urusi.

ggg

Lakini wakati huo huo kuna shinikizo la kukomesha utegemezi wa gesi ya Urusi, pia kumekuwa na hofu ya muda mfupi kwamba Urusi inaweza kuzuia zaidi au hata kusimamisha usambazaji wa gesi, ikiwa ni kulipiza kisasi kutokana na msaada wa kijeshi kwa Ukraine.

Shinikizo zaidi linakuja kutoka kwa Gazprom, mtoa huduma wa nishati nchini Urusi inayomilikiwa na serikali, ambayo imesitisha usambazaji wa gesi kwa Bulgaria, Finland, Poland, Denmark na Uholanzi kutokana na kutolipa kwa kutumia pesa ya Urusi rubles.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati mataifa ya Ulaya yanapoacha kununua gesi kutoka Urusi, yanahitaji kupunguza kwa kiasi kikubwa mauzo yao ya nje ya gesi na kuweka shinikizo zaidi kwa usambazaji wa kimataifa.

Wengi wamelazimika kutegemea soko la kimataifa la gesi ya asilia iliyoyeyushwa (LNG) ambayo inaweza kusafirishwa duniani kote kwa meli, tofauti na kupelekwa kwa njia ya mabomba.

Katika miaka ya nyuma nchi za Ulaya kwa kawaida zilinunua mabaki ya LNG kutoka nchi kama Qatar na Marekani katika majira ya kiangazi, ambayo waliweka kwenye hifadhi kwa majira ya baridi yanayofuata.

Tatizo linalowakabili mwaka huu ni kwamba nchi za Asia tayari zimetia saini kandarasi za muda mrefu za kununua LNG nyingi duniani kabla hata haijachimbwa, na hivyo kuacha kiasi kidogo kwenye soko la kimataifa.

Je, gesi inatumika kwa ajili gani?

Ulimwenguni kote, gesi nyingi huchimbwa katika nchi yake ya asili. Lakini katika maeneo mengi hiyo haitoshi na uagizaji wa bidhaa kutoka nje unahitajika, hasa wakati wa majira ya baridi.

Mara tu gesi inayoagizwa kutoka nje inapofika ilipokuwa ikienda, inauzwa kwa baadhi ya watoa huduma za nishati kwa bei ya papo hapo (ikionyesha gharama ya papo hapo na utoaji). Baadhi hununuliwa kwa bei ya baadaye iliyokubaliwa mapema kulingana na kile wanachotarajia katika miezi ijayo.

Sehemu ya gesi pia huwashwa ili kuzalisha umeme, ikimaanisha kuwa bei ya juu ya gesi pia inasukuma bili zetu za umeme.

Mnamo 2021, karibu 40% ya umeme wa Uingereza ulitolewa na gesi inayowaka.

Inyobaki hutumika kwa ajili ya joto na maji ya moto katika nyumba na biashara au kuhifadhiwa katika vituo vya kuhifadhi kwa majira ya baridi.

Je, bei zinapangwaje?

Mfumo wa kupanga bei ya gesi hutofautiana kati ya nchi na nchi. Hakuna bei moja ya kimataifa ya gesi.

Bei ya jumla ya gesi huamuliwa na kiasi gani inagharimu wasambazaji wa nishati kununua gesi kutoka kwa wazalishaji wa ndani na wa kimataifa. Bei ya gesi asilia inapanda na kushuka kulingana na mahitaji ya kimataifa.

Uvumi na hofu ya usumbufu unaokaribia pia unaweza kupandisha bei ya gesi kwenye masoko ya kimataifa. Hii inaweza kuongeza bili za gesi kwa kaya na biashara. Bili ya kawaida ya gesi ya kaya nchini Uingereza inajumuisha bei ya jumla, gharama za uendeshaji za mtoa huduma wa nishati, gharama ya utunzaji wa mtandao na kodi ikiwa ni pamoja na VAT na ushuru wa kijani.

Nani anafaidika?

Kampuni zinazochimba na kusafirisha gesi zimenufaika kutokana na ongezeko la mahitaji. Sehemu kubwa ya LNG duniani inatoka Australia, Qatar na Marekani. Gesi pia inazalishwa nchini Norway na Bahari ya Kaskazini.

Kati ya Aprili na Juni mwaka huu, Shell iliripoti faida duniani kote ya £9.4bn huku BP ikitengeneza £6.9bn, zaidi ya mara tatu ya kiasi ilichotengeneza kwa muda kama huo.