Vita vya Ukraine: Urusi yasitisha usambazaji wa gesi kwa Poland na Bulgaria

Chanzo cha picha, Getty Images
Kampuni ya nishati ya Urusi Gazprom imeziambia nchi za Poland na Bulgaria kuwa itaacha kutuma gesi katika nchi hizo mbili kuanzia Jumatano
Kampuni ya gesi ya taifa la Poland PGNiG ilisema kuwa imeambiwa usambazaji wote wa gesi utasitishwa kuanzia saa mbili za asubuhi kwa saa za eneo, saw ana saa kumi na mbili alfajiri kwa saa za Afrika mashariki.
Wizara ya nishati ya Bulgaria pia ilisema imefahamishwa kwamba usambazaji wa gesi utasitishwa kuanzia Jumanne.
Hii inakuja baada ya Urusi kusema kuwa ''nchi zisizo rafiki'' , lazima zianze kulipia gesi kwa sarafu ya rouble, vinginevye itakata usambazaji. Nchi zote mbeli zimekataa kulipa kwa njia hii.
PGNiG hutegemea kampuni ya Urusi ya Gazprom kwa sehemu kubwa ya gesi yake inayoagizwa kutika nje na ilinunua 53% ya mafuta yake kutoka kampuni ya Urusi katika robo ya kwanza ya mwana huu.
Ilielezea kusitishwa huko kwa usambazaji wa gesi kama ukikaji wa mkataba, na kuongeza kuwa kampuni itachukua hatua kurejesha upatikanaji tena wa gesi.
Bulgaria, ambayo hutegemea Gazpromkwa zaikdi ya 90% ya gesi yake, ilisema imechukua hatua za kutafuta vyanzo mbadala lakini hakuna masharti juu ya ununuzi wa gesi yanayopaswa kuwepo kwa sasa.
Wizara ya nishati ya nchi hiyo alisema kuwa Bulgaria iitekeleza majukumu yake chini ya mkataba wa sasa na Gazprom na kufanya malipo yote yanayohitajika.
Iliongeza kuwa mfumo wa malipo mapya uliopendekezwa na Urusi ni uvunjaji wa mkataba uliopo.
Kufuatia taarifa hizi, wizara ya hali ya hewa ya Poland imesema kuwa usambazaji wa nishati nchini humo uko salama.
Waziri wa hali ya hewa wa nchi hiyo Anna Moskwa alisema kuwa hakuna haja ya kuchukua gesi kuthoka kwenye akiba na gesi kutoka kwa wateja itakuwa ni nkuipunguza.
Naibu Waziri wa mambo ya nje wa Poland, Marcin Przydacz, alisema nchi yake imekuwa ikijiandaa kwa uwezekano wa Urusi kupunguza mauzo ya gesi kwa kutafuta wasambazaji wengine wa gesi.
"Nina uhakika kwamba tutaweza kulishugulikia hili ," aliiambia BBC.
Aliongeza kuwa kuahirishwa kwa usambazaji wa gesi kunaonyesha kuwa Moscow "sio mshirika wa kuaminika katika aina yoyote ya biashara " na akazitaka nchi nyingine za Ulaya kama Ujerumani kuunga mkono marufuku ya kuagiza nishati kutoka Urusi .
Poland tayari ilikuwa inapaka kusitisha uagizaji wa gesi kutoka Urusi ifiapo mwishoni mwa mwaka , wakati mkataba wake wa muda mrefu na Gazprom utakapomalizika.
PGNiG ilisema akiba yake ya gesi iliyopo chini ya ardhi imejaa kwa takriban 80%, na wakati kipindi cha majira ya joto kinakaribia, gesi itakayohitajika itakuwa ya nkiwango cha chini.
Poland pia ina vyanzo mbadala vya usambazaji wa gesi inayotumia, ukiwemo mfumo wa gesi asilia (LNG) katika Swinoujscie.
Tarehe 1 Mei , bomba jipya gesi nlinaloiunganisha na Lithuania pia litazinduliwa ambalo litaipatia Poland uwezo wa kupata gesi kutoka bomba la Lithuania la LNG.
Na bomba jipya linalosambaza gesi kutoka Norway,linalofahamika kama the "Baltic Pipe", litaanza kutumiwa katika mwezi Oktoba. Linatarajiwa kuwa na uwezo kamili kufikia mwishoni mwa mwaka na linaweza kuchukua nafasi ya mauzo ya gesi kutoka Urusi.

Uchambuzi
Na Adam Easton, BBC Warsaw
Kukatwa kwa usambazaji wa gesi kunamaanisha Poland haitaweza moja kwa moja kutimiza mahitaji ya gesi kutoka kwa wateja wao.
Katika miaka ya hivi karibuni, Poland ilipunguza utegemezi wake wa gesi ya Urusi na sasa inanunua gesi asilia LNG kutoka Qatar na mifumo ya mabomba inayoiunganisha na soko la Ulaya. Pia msimu wa majira ya baridi wa kupasha joto nyumba umeisha, kwahiyo itahitaji kiwango cha chini cha gesi.
Lakini usambazaji wa Gazprom ni zaidi ya nusu ya gesi yote inayoagizwa na Poland. Hilo ni shimo kubwa linalohitaji kujazwa
Na Poland sio nchi pekee ya Muungano wa Ulaya ambayo inataka kusitisha sasa ununuz wa nishati kutoka Urusi.
Kuna ushindani mkubwa katika soko la gesi ambalo tayari limekuwa dogo. Wakati msimu wa upashaji joto wa nyumba utakapoanza ten ana kuongezeka kwa mahitaji yake, Poland inaweza kukabiliwa na miezi migumu michache kupata gesi ya kutosha.
Na kama itafanya hivyo, italazimika kubana usambazaji wa gesi kwa viwanda vikubwa vinavyotumia gesi zaidi.

Usambazaji wa gesi kutoka Urusi unachangia takriban 40% ya gesi asilia ya gesi inayoagizwa na Muungano wa Ulaya.
Hatahivyo, nchi nyingi zimeahidi dkuachana na nishati hiyo ya Urusi ili kujibu uvamizi wake wa Ukraine.
Marekani imetangaza marufuku kamili dhidi ya uagizaji wa mafuta kutoka Urusi, gesi na makaa ya mawe.
Wakati huo huo, Uingereza inatarajiwa kusitisha ununuzi wa mafuta ya Urusi kufikia mwishoni mwa mwaka , huku marufuku ya gesi ikifuatia haraka iwezekanavyo, na Muungano wa Ulaya unapunguza ununuzi wa gesi kwa theruthi mbili.
Unaweza pia kusoma
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine












