TUAMBIE SIMULIZI YAKO: Je, maisha yako yameathiriwa vipi na kupanda kwa bei ya vyakula?
Familia kote ulimwenguni zinapambana na hali ya kupanda kwa gharama za maisha na watu milioni 71 katika nchi zinazoendelea wanaangukia katika umaskini kutokana na kupanda kwa bei, kwa mujibu wa UN.
Bei za vyakula na uhaba wa chakula vinalazimisha familia kutokula milo mitatu, kutumia viungo vya chakula vya bei rahisi na kuzorotesha afya zao za kimwili na kiakili.
Je, wewe au familia yako mmeathiriwa moja kwa moja na kupanda kwa gharama za chakula? Tuambie jinsi maisha yako yalivyobadilika - ikiwa simulizi yako itachaguliwa, mmoja wa wanahabari wetu anaweza kuwasiliana nawe hivi karibuni.