Mzozo wa Ukraine: Kwa kiasi gani dunia inategemea mafuta na gesi ya Urusi?

Employees walk at the construction site of a gas metering station, part of the pipeline link between Bulgaria and Greece near the village of the Malko Kadievo, on March 18, 2022

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Energy costs have risen since Russia's invasion of Ukraine

Urusi imesitisha usambazaji wa gesi kwenda Poland na Bulgaria baada ya nchi zote mbili kukataa kulipia usambazaji huo kwa kutumia fedha ya Urusi, rouble.

EU imesema inachukulia hatua hiyo ya Urusi kuwa ni kama aina ya usaliti.

Kwa namna gani Urusi imeathiri biashara ya gesi?

Licha ya uvamizi wa Ukraine, Urusi imeendelea kusambaza kiasi kikubwa cha gesi kwenda nchi nyingi za Ulaya. Hata hivyo, baada ya mataifa ya Magharibi kuiwekea Urusi vikwazo vya kifedha, Rais Putin alitangaza kuwa nchi 'zisizo rafiki' zitalazimika kulipia gesi kwa sarafu ya Urusi.

Kampuni ya nishati inayomilikiwa na serikali ya Urusi ya Gazprom inasema kuwa imesitisha kupeleka gesi Poland na Bulgaria na haitaruhusu hadi hapo malipo yatakapofanywa kwa sarafu ya rouble.

Nchi nyingine nyingi za EU zinatazamiwa kukabiliwa na hatua kama hily itakapofika wakati wa malipo katikati ya mwezi Mei. Malipo kwa kutumia sarafu ya rouble yataimarisha sarafu hiyo ya Urusi na kunufaisha uchumi wake.

Nchi gani zinalipa kwa kutumia sarafu ya rouble?

Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen alionya kwamba kufuata matakwa ya Urusi kungekiuka vikwazo vya Umoja wa Ulaya na itakuwa "hatari kubwa" kwa makampuni ambayo yatafanya hivyo. Nchi za Umoja wa Ulaya zimegawanyika kuhusu ni kwa muda gani zitapunguza utegemezi wa nishati ya Urusi.

Kampuni za gesi katika baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya zikiwemo Ujerumani, Hungary na Slovakia zimekubali kulipia gesi kwa euro kupitia benki ya Urusi ya Gazprombank, ambayo itabadilisha malipo hayo kuwa roubles. Gazeti la Financial Times limeripoti kuwa makampuni ya gesi nchini Austria na Italia pia yanapanga kufungua akaunti kwenye benki ya Gazprombank.

EU ilisema wiki iliyopita kwamba ikiwa wanunuzi wa gesi ya Urusi wanaweza kukamilisha malipo kwa euro na kupata uthibitisho wa hili kabla ya ubadilishaji wowote kuwa roubles kufanyika, hiyo haitakiuka vikwazo. Hata hivyo kuna maoni tofauti miongoni mwa nchi kuhusu jinsi ya kutafsiri mwongozo wake wa awali, na wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya wamesema wanataka ufafanuzi zaidi kuhusu suala hilo.

Kiwango gani cha gesi kinachosambazwa na Urusi kwenda Ulaya?

Mwaka 2019, Urusi ilichangia 41% ya uagizaji wa gesi asilia wa EU.

Ikiwa usambazaji wa gesi ya Urusi kwenda Ulaya ungesityisshwa, Italia na Ujerumani zingekuwa hatarini zaidi kwani zinaagiza gesi nyingi zaidi kutoka Urusi.

Russia gas exports

Urusi huchangia 5% ya usambazaji wa gesi nchini Uingereza, na Marekani haiagizi gesi yoyote kutoka Urusi.Urusi inasambaza gesi Ulaya kupitia mabomba makuu kadhaa. Gesi hiyo inakusanywa katika vituo vya hifadhi vya kanda, na kisha kusambazwa katika bara zima.

Kuna mbadala mwingine wa gesi ya Urusi?

Bulgaria inasema inatazamia kuongeza uagizaji wa gesi kutoka Azerbaijan, pamoja na kuingia mikataba na nchi za Uturuki na Ugiriki. Naibu waziri wa mambo ya nje wa Poland aliiambia BBC kuwa yapo "machaguo mengine ya kupata gesi kutoka kwa washirika wengine," ikiwa ni pamoja na Marekani na mataifa ya Ghuba.

Ulaya inaweza kuwageukia wasafirishaji wa gesi wengine waliopo kama vile Qatar, Algeria au Nigeria, lakini kuna vikwazo vya utekelezaji vya kupanua uzalishaji haraka.Marekani imekubali kusafirisha mita za ujazo bilioni 15 za gesi asilia iliyosafishwa (LNG) hadi Ulaya mwishoni mwa mwaka huu.

wind turbine

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, The EU hopes to massively boost its use of renewable energy, including wind power

EU imependekeza mpango wa kuifanya Ulaya kutotegemea nishati ghafi ya Urusi kabla ya 2030 - ikiwa ni pamoja na kuna na vyanzop vingi vya kupata gesi.

Je,vikwazo gani vimewekwa kwenye gesi na mafuta ya Urusi?

Marekani imetangaza kupiga marufuku kabisa uagizaji wa mafuta, gesi na makaa ya mawe kutoka Urusi.Uingereza itayaondoa mafuta ya Urusi mwishoni mwa mwaka huu na EU inapunguza uagizaji wa gesi kwa kiwango cha theluthi mbili.

Urusi imeonya kupiga marufuku mafuta yake kutasababisha "matokeo mabaya kwa soko la kimataifa".

Licha ya vikwazo kadhaa, tangu kuanza kwa vita Urusi imeongeza karibu mara mbili ya mapato yake kutokana na kuuza mafuta kwa nchi za Umoja wa Ulaya, kulingana na Kituo cha Utafiti wa Nishati na Hewa Safi, huku bei ya mafuta na gesi ikipanda.

Je, Urusi inasafirisha mafuta kiasi gani?

Urusi ni nchi ya tatu kwa uzalishaji wa mafuta duniani, baada ya Marekani na Saudi Arabia.

Oil producers top 10

Kabla ya kutangazwa kwa vikwazo, kati ya mapipa milioni tano ya mafuta yasiyosafishwa ambayo inauza nje kila siku, zaidi ya nusu ya mafuta hayo yalipelekwa Ulaya.

Uagizaji wa mafuta kutoka Urusi ulichangia 8% ya jumla ya mahitaji ya mafuta ya Uingereza na 3% ya mahitaji ya mafuta ya Marekani.

Vipi kuhusu mafuta mbadala?

Mchambuzi wa utafiti Ben McWilliams anasema ni rahisi kupata wasambazaji mbadala wa mafuta kuliko gesi, kwa sababu wakati wengine wanatoka Urusi, "pia kuna usafirishaji mwingi kutoka mahali pengine".

Baadhi ya wanachama wa IEA wametoa sawa na mapipa milioni 120 kutoka kwa hifadhi ya mafuta - ambayo ni kiwango kikubwa zaidi katika historia yake.Rais wa Marekani Joe Biden aliamuru kutolewa kwa kiasi kikubwa kwa mafuta kutoka kwa akiba ya Marekani katika juhudi za kupunguza gharama ya juu ya mafuta.

Marekani pia inataka Saudi Arabia kuongeza uzalishaji wake wa mafuta na inaangalia kulegeza vikwazo kwa mafuta ya Venezuela.

Reality Check branding