Jinsi Urusi ilivyobadilisha masharti ya mashambulizi ya nyuklia

Chanzo cha picha, EPA
Muongozo mpya wa nyuklia, ambao Vladimir Putin aliuidhinisha mnamo Novemba 19, 2024, una vipengele na dhana kadhaa ambazo hazikuwa katika toleo la awali.
Zaidi ya hayo, kwa namna muongozo huo ulivyobadilishwa umeonekana kuleta mabadiliko maana katika vifungu vyake.
Jina rasmi la muongozo huo ni Misingi ya Sera ya Serikali ya Shirikisho la Urusi katika uwanja wa udhibiti wa Nyuklia. Toleo la awali liliidhinishwa mnamo 2020.
Waraka mpya una sura nne:
- "Masharti ya jumla", ambayo yanaelezea dhana za msingi, malengo na malengo ya kuzuia matumizi ya nyuklia.
- "Hali ya uzuiaji wa nyuklia" - Hii inaelezea kile kinachoihamasisha Urusi kutumia vikosi vya kimkakati kuzuia
- "Masharti ya mpito kwa matumizi ya silaha za nyuklia"
- "Kazi za vyombo vya serikali ya shirikisho" - sura hii ina orodha na mamlaka ya mashirika yote ya serikali yanayohusika katika kuzuia nyuklia
Mabadiliko pekee katika mafundisho mapya ni katika sura ya mwisho.
Moja ya mabadiliko muhimu zaidi ni kwamba Urusi ina haki ya kutumia silaha za nyuklia ikiwa kuna tisho kubwa kwa uhuru au uadilifu wa nchi. Hapo awali, hali kama hiyo ilikuwa "tisho dhidi ya uwepo wa serikali."
Hati ya muongozo huo mara nyingine ina maneno yasiyoeleweka, na baadhi ya vifungu vinapatikana katika maeneo tofauti.
Maneno katika waraka kama huo huenda yamewekwa katika maneno yasiyoeleweka kwa makusudi na ya kukanganya kama sehemu ya sera ya udhibiti.
Masharti ya jumla yaliyotolewa
Tofauti ya kwanza katika muongozo mpya inahusu kifungu kwamba "Shirikisho la Urusi linaziona silaha za nyuklia kama njia ya kipekee kama njia ya kuzuia, matumizi ambayo ni kipimo cha kupindukia na cha kulazimishwa."
Sasa neno "kipekee" limetoweka kwenye muongozo huo, jambo ambalo linaweza kumaanisha moja kwa moja kuwa silaha za nyuklia haziwezi kudhibitiwa. Mabadiliko haya hayaelezewi kwa njia yoyote katika waraka wote.
Mabadiliko ya pili katika sura hii ni kutengwa kutoka kwenye orodha inayoonyesha kuwa silaha za nyuklia haziwezi kuzuiwa kisheria.
Dhidi ya muungano na ushirikiano
Sura ya pili, huhusu yaliyomo katika udhibiti wa silaha hizi yenye kichwa "The Essence of Deterrence," ilipitia mabadiliko makubwa zaidi, ambapo waandishi wa muongozo huo walijaribu kuunganisha washiriki wa miungano tofauti na ushirikiano na jukumu la pamoja.
Urusi imetangaza kuwa itazingatia kama lengo la kuzuia silaha za nyuklia wanachama wote wa muungano, kwa taifa moja litakaloishambulia, pamoja na taifa ambalo litatoa eneo kwa taifa jingine, bahari au anga kushambulia Urusi.
Kifungu kingine kipya kinatishia kutumia kizuizi cha nyuklia ikiwa kutakuwa na "ukiukaji dhidi ya Urusi na taifa lolote lisilo la nyuklia, lakini kwa ushiriki au msaada wa taifa lenye nyuklia."

Chanzo cha picha, AFP
Kifungu hiki kinahusiana moja kwa moja na kuiruhusu Ukraine kutumia makombora ya Marekani dhidi ya malengo kwenye ardhi ya Urusi.
Vladimir Putin alizungumza kwanza juu ya kujiandaa kubadili muongozo mnamo Septemba, wakati kukiwa na mzozo katika serikali ya Marekani juu ya uwezekano wa kuiruhusu Ukraine kutumia makombora ya Marekani ya ATACMS dhidi ya maeneo kwenye ardhi ya Urusi.
Mnamo mwezi Novemba, Putin alitia saini muongozo mpya baada ya Ukraine kupokea ruhusa hiyo.
Hatari
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Orodha ya "hatari ambayo, kulingana na mabadiliko katika hali ya kijeshi na kisiasa na kimkakati, inaweza kuendeleza kuwa vitisho vya kijeshi" pia inajumuisha vitu kadhaa vipya.
Katika moja ya mafundisho hayo, mafundisho hayo kwa mara nyingine tena yanataja "kuundwa kwa muungano mpya au upanuzi wa miungano ya kijeshi iliyopo (blocs, muungano), na kusababisha njia ya miundombinu yao ya kijeshi kwenye mipaka ya Shirikisho la Urusi."
Kwa wengine, ni "hatua za adui anayeweza kuwa na lengo la kutenga sehemu ya eneo la Shirikisho la Urusi, ikiwa ni pamoja na kuzuia upatikanaji wa mawasiliano muhimu ya usafiri."
Nchini Urusi kuna mkoa mmoja ambao umekatwa kabisa kutoka eneo la jimbo - mkoa wa Kaliningrad.
Kwa kuongezea, Crimea iliyochukuliwa, ambayo Urusi inaona kuwa eneo lake, pia inaunganishwa na eneo la Urusi kwa daraja.
Hatari mbili zaidi zilizoorodheshwa katika mafundisho ni kushindwa, uharibifu au uharibifu wa vitu hatari vya kiikolojia vya Shirikisho la Urusi (hata hivyo, maandishi hayasemi wapi yanaweza kuwa), pamoja na mazoezi makubwa karibu na mipaka ya Urusi.
Orodha ya hatari ina vitu kadhaa zaidi, ambavyo baadhi yake vimebadilishwa kidogo.
Kwa mfano, orodha ya mifumo hatari ya nafasi ni pamoja na silaha za kupambana na nyota, na "uchunguzi" wa mifumo ya ulinzi wa makombora, makombora ya masafa ya kati na mafupi, na silaha mbalimbali za kimkakati zisizo za nyuklia katika maandishi zilibadilishwa na "uwepo na kupelekwa."
Hata hivyo, baadhi ya mabadiliko madogo yanaonekana kupanua dhana kwa kiasi kikubwa. Ni jambo moja kupeleka makombora, yaani, kuwaleta kwenye nafasi, na nyingine kabisa kujenga na kuwaweka katika hifadhi.
Masharti ya matumizi
Moja ya mambo muhimu zaidi ya muongozo huo ni hali ambayo Urusi inaweza kutumia silaha za nyuklia. Masharti haya hayamaanishi kwamba yatatumika moja kwa moja chini ya masharti hayo. Lakini kwa kuyachapisha, Urusi inatangaza kuwa ina haki kufanya shambulio la nyuklia wakati inaposhambuliwa.
Kifungu kikuu cha aya hii katika toleo lililopita kilitangaza kwamba silaha za nyuklia zinaweza kutumika kujibu shambulio la nyuklia dhidi ya Urusi na washirika wake, au kwa shambulio lolote ambalo litatishia kuwepo kwa serikali.
Orodha ya masharti ya matumizi ya silaha za nyuklia katika toleo lililopita ilijumuisha vipengele vinne:
- kupokea taarifa za kuaminika kuhusu uzinduzi wa makombora ya masafa marefu yanayoshambulia Urusi na washirika wake. Hatua hii bado haijabadilika;
- matumizi ya silaha za nyuklia au aina nyingine za silaha za maangamizi dhidi ya maeneo ya Urusi au washirika wake. Maneno "dhidi ya na (au) vitu vya Shirikisho la Urusi vilivyo nje ya eneo lake" yaliongezwa kwenye kifungu hiki;
- Shambulio dhidi ya malengo muhimu nchini Urusi ambayo yatavuruga ulipizaji kisasi wa nyuklia.
- kifungu " Kutumia silaha za kawaida dhidi ya Urusi, wakati uwepo wa serikali unapotishiwa" ilibadilishwa, na kuongeza Belarus, na pia kuchukua nafasi ya "tisho la uwepo" na "tisho muhimu kwa uhuru na (au) uadilifu wa eneo". Makombora ya yanayoongozwa, ndege zisizo na rubani, makombora ya hypersonic na ndege nyingine na pale ndege au mashambulio hayo yatakapovuka mpaka wa serikali ya Shirikisho la Urusi."
Je, muongozo huu umebadilika kiasi gani?
Ilijulikana mwishoni mwa Septemba kwamba Urusi itabadilisha mafundisho yake ya nyuklia. Vladimir Putin alisema hivyo.
Alitangaza pia mabadiliko mawili - majibu ya uchokozi dhidi ya Urusi na taifa lolote lisilo la nyuklia, lakini kwa ushiriki au msaada wa taifa la nyuklia, pamoja na hali ya matumizi ya silaha za nyuklia baada ya kupokea "habari za kuaminika kuhusu uzinduzi mkubwa wa ndege au droni." Mambo haya yote mawili yalionekana katika muongozo mapya.
Mwezi Septemba, Maxim Starchak kutoka Kituo cha Sera ya Kimataifa na Ulinzi katika Chuo Kikuu cha Queen, akizungumzia uvumbuzi huo, aliiambia BBC kwamba Putin alizungumzia vifungu vipya tu kufafanua masharti ya matumizi ya silaha za nyuklia, lakini sababu za matumizi yao hazibadiliki.
"Kama hapo awali hali ya matumizi ya silaha za nyuklia ilikuwa ni shambulio la makombora ya masafa marefu, sasa hili limepanuka kwa njia zote za mashambulizi ya anga na ardhini," alisema.
"Lakini ukweli ni kwamba, hii tayari ilichukuliwa kuwa tisho lenye uwezo wa kuwa na athari mbaya kwa vikosi vya kimkakati hata chini ya muongozo wa sasa," mtaalam huyo aliongeza wakati huo.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Seif Abdalla












