Ukraine yarusha makombora ya masafa marefu nchini Urusi - Kremlin

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Urusi imesema Ukraine ilirusha makombora ya masafa marefu yaliyotolewa na Marekani nchini humo kwa mara ya kwanza siku ya Jumanne.

Ukraine ilitumia makombora ya Atacms katika shambulizi la eneo la Bryansk nchini Urusi asubuhi ya leo, wizara ya ulinzi mjini Moscow ilisema.

Makombora matano yalidunguliwa na moja kuharibiwa, huku vipande vyake vikisababisha moto katika kituo cha kijeshi katika eneo hilo, ilisema katika taarifa.

Matumizi ya makombora ya Marekani pia yaliripotiwa katika vyombo vya habari vya Ukraine, lakini Ukraine bado haijatoa maoni.

Katika taarifa, wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema shambuklizi hilo lilitekelezwa mwendo wa alfajiri.

Moto uliosababishwa na vifusi vilivyoanguka kutoka kwa moja ya makombora ulizimwa haraka na hakukuwa na majeruhi, ilisema.

Jeshi la Ukraine hapo awali lilithibitisha kwamba lilikuwa limeshambulia ghala la kuhifadhia silaha katika eneo la Urusi la Bryansk, lakini halikubainisha kama Atacms zilitumika.

Ilisema shambulio hilo kwenye ghala karibu kilomita 100 kutoka mpaka karibu na mji wa Karachev, lilisababisha milipuko 12 ya pili.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Vyombo vya habari vya Ukraine, vikinukuu chanzo cha kijeshi, viliripoti kuwa makombora hayo ya Marekani yametumiwa.

Wakati huo huo, mapema Jumanne, Putin aliidhinisha mabadiliko ya kanuni za nyuklia za Urusi, akiweka masharti mapya ambayo nchi yake itazingatia kutumia silaha hizo kwa mashambulizi.

Urusi inasema shambulio kutoka kwa taifa lisilo mwanachama wa nyuklia, , litachukuliwa kama shambulio la pamoja dhidi ya Urusi.

Siku ya Jumanne, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov alisema Urusi "itaendelea kutoka kwa ufahamu" kwamba makombora yanaendeshwa na "wataalam wa kijeshi wa Marekani".

"Tutachukulia hili kama sura mpya ya vita vya magharibi dhidi ya Urusi na tutachukua hatua ipasavyo," aliuambia mkutano wa waandishi wa habari katika G20 huko Rio de Janeiro.

Moscow ilisema Jumatatu kwamba mashambulizi yoyote ndani ya eneo lake na makombora ya Marekani yatasababisha "jibu linalofaa na linaloonekana".

Ukraine tayari imekuwa ikitumia Atacms katika maeneo yanayokaliwa na Warusi katika eneo lake kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Makombora hayo yanaweza kulenga shabaha kwa umbali wa hadi 300km (maili 186) na ni vigumu kuyazuia.

Kyiv sasa inaweza kushambulia zaidi Urusi kwa kutumia makombora, ikiwa ni pamoja na kuzunguka eneo la Kursk, ambako vikosi vya Ukraine vinashikilia zaidi ya kilomita za mraba 1,000 za eneo hilo.

Pia unaweza kusoma

Imetafasiriwa na Seif Abdalla