Je, Ukraine ina uwezo wa kuzuia mabomu ya kuongozwa ya Urusi

Chanzo cha picha, VADIM SAVITSKY/RUSSIAN DEFENSE MINISTRY PRESS OFFICE/TASS
Urusi imeboresha mabomu mazito ya Usovieti, ikiyawekea moduli za upangaji na ulengaji kwa usahihi na kuunda njia rahisi kwa mabomu ya kuongozwa. Je, wanajeshi wa Ukraine wanaweza kuyazuia?
Matumizi ya mabomu ya kuongozwa ya Urusi imejulikana tangu mwaka jana. Hapo awali iliripotiwa kuwa mabomu hayo yaliundwa kwa kutumia bomu la FAB-250, ambalo lilitumiwa tangu nyakati za Usovieti. Hili ni bomu lenye mlipuko mkubwa na uzito wa takriban kilo 250 na lina takriban kilo 100 za vilipuzi.
Awali, lilitengenezwa kama bomu la kuanguka lenyewe, lakini wakati linawekewa moduli ya urekebishaji na upangaji (UMPC), linaweza kutupwa makumi ya kilomita hadi eneo linalolengwa.
Hii huruhusu kushambulia maeneo lengwa ya ardhini bila kuingia kwa mifumo ya ulinzi wa anga.
Mabomu ya kuongozwa ya Urusi yamehatarisha maeneo ya kimkakati karibu na Chasov Yar na katika eneo la Avdeevka katika mkoa wa Donetsk, Nazar Voloshin, msemaji wa Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine Khortitsa, aliiambia CNN: "Wanatupa silaha nzito bila hata kuwa karibu na laini ya mawasiliano au kuingia eneo letu la ulinzi wa anga.”
Wakati ndege zao zinafanya kazi, ni vigumu kwa ulinzi wetu kufanya kazi; wanaweza kujificha tu.”
Kulikuwa na ripoti za jeshi la Urusi kutumia mabomu yenye nguvu zaidi ya kuongozwa, kama vile FAB-500. Na mwisho wa Machi, vyombo vya habari vya Ukraine na Magharibi viliandika juu ya kushambuliwa kwa vikosi vya wanajeshi wa Ukraine karibu na Ugledar kwa bomu la tani moja na nusu ya ODAB-1500 ya kulipuka.
Mabomu kama hayo yanajulikana kama thermobaric; yaaunda wimbi la mshtuko lenye nguvu ambalo linaweza kupenya makazi na hata kwa umbali mkubwa husababisha majeraha makubwa.
Wataalam walibaini kuwa mabomu mazito ya kuongozwa, ambayo hulazimisha ndege za Urusi kupaa karibu na mstari wa mbele na kusababisha hatari ya kukaribia ulinzi wa anga.
Lakini muda mfupi baadaye, maendeleo mengine ya Urusi yakajulikana - UMBP D-30SN. Ni analogi ya bomu ya usahihi wa juu ya Marekani ya GBU-39. Kwa kuzingatia picha za bomu la anga la Urusi na mabaki yake zilizoonyeshwa na vyombo vya habari vya Ukraine, yanafanana sana kwa muonekano.

Chanzo cha picha, DEFENSE EXPRESS

Chanzo cha picha, DEFENSE EXPRESS
Na hivi ndivyo GBU-39 nne za Marekani zinavyoonekana wakati wa kusitishwa kwa utendaji wa ndege ya F-15E (picha kutoka maktaba)

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
GBU-39 ni moja tu ya familia kubwa ya mabomu ya angani na JDAM (hii ni sawa na UMPC), na moja ya nyepesi - kilo 130, hata hivyo, idadi kubwa ya hii inamilikiwa na kichwa kombora chenye mlipuko mkubwa.
Kulingana na GBU-39 na kombora la M270 na M142 HIMARS, bomu la kipenyo kidogo (GLSDB) liliundwa ambalo linaweza kurushwa kutoka kwa mifumo ya makombora ya ardhini.
Silaha kama hizo zilitolewa kwa Ukraine, lakini hakukuwa na ripoti za matumizi yao makubwa kutoka kwa pande zote zinazopigana.
Raia pia huandika juu ya kujumuisha katika analog ya Urusi ya GBU-39 na injini ya turbojet ya nje na tanki ya mafuta, ambayo inawezesha kuizindua sio tu kutoka kwa ndege, lakini pia kutoka kwa mifumo mingi ya roketi ya Tornado-S.
GBU-39 ni moja tu ya familia kubwa ya mabomu ya angani na JDAM (hii ni sawa na UMPC), na moja ya nyepesi - kilo 130, hata hivyo, idadi kubwa ya hii inamilikiwa na kichwa kombora chenye mlipuko mkubwa.
Kulingana na GBU-39 na kombora la M270 na M142 HIMARS, bomu la kipenyo kidogo (GLSDB) liliundwa ambalo linaweza kurushwa kutoka kwa mifumo ya makombora ya ardhini.
Silaha kama hizo zilitolewa kwa Ukraine, lakini hakukuwa na ripoti za matumizi yao makubwa kutoka kwa pande zote zinazopigana.
Raia pia huandika juu ya kujumuisha katika analog ya Urusi ya GBU-39 na injini ya turbojet ya nje na tanki ya mafuta, ambayo inawezesha kuizindua sio tu kutoka kwa ndege, lakini pia kutoka kwa mifumo mingi ya roketi ya Tornado-S.
Na ingawa hakukuwa na habari rasmi juu ya utumiaji wa mabomu ya kuteleza ya Kirusi kutoka kwa mifumo ya ardhini, hakuna sababu ya kuondoa uwezekano kama huo. Inapaswa kuzingatiwa kuwa ikiwa kinu ziada hutumiwa, umbali wa bomu lenye kuongozwa inaweza kuwa kilomita 100 au zaidi.
Hii inatumika popote – ama ardhi au angani.

Chanzo cha picha, EPA
Kwa nini mabomu ya kuongozwa hayawezi kudunguliwa?
Kama wataalam wa ulinzi wa anga wanavyosema, huwezi kuangusha kitu kinachoanguka. Kwa kweli, kauli hii ni ya kweli ya kile katika lugha ya jeshi inaitwa "cast iron" - mabomu ya kuanguka yenyewe. Kwa upande wa mabomu ya kuelekezwa, hii sio kweli kabisa - ikilinganishwa na ganda la bomu, ni kubwa kabisa, ina mbawa na vidhibiti, na katika maendeleo mapya, ina kiongeza kasi. Hilo sio bomu kabisa, lakini nusu-bomu, nusu-roketi; na, inapaa, ambayo ina maana kwamba kinadharia inaweza kudunguliwa. Lakini ni vigumu sana.
Kwanza kabisa, ukilenga kitu kama hicho halibaki hewani kwa muda mrefu. Kasi yake ya awali ni sawa na kasi ya ndege ya kivita, kwa kawaida moja na nusu hadi Mach mbili, inawezekana kuwa ina kasi, kwa hiyo, ina umbali wa kilomita 60 kwa kilicho lengwa kwa dakika moja au mbili. Ni vigumu kuona kwenye skrini za rada. Inaweza kubadilika – sio kama kombora la kusafiri au droni, lakini kwa kuzingatia mambo mawili ya kwanza, hii ni shida kubwa ya ziada kwa ulinzi wa anga.
Uwezekano wa kushambulia shabaha kama hiyo kwa kombora moja la kuzuia ni mdogo; kadhaa yanahitajika, na sio rahisi. Kwa kuzingatia kwamba Urusi ina hifadhi kubwa ya mabomu ya angani ambayo yanaweza kubadilishwa kuwa mabomu ya kuongozwa, kutumia makombora ya gharama kubwa juu yao sio ghali tu, bali pia ni hatari. Ikiwa ulinzi wa anga wa Ukraine una uhaba wa mabomu, Urusi inaweza kukamata anga na kuanza kudondosha mabomu ya kawaida, ambayo yataanguka bure, hii itakuwa janga kwa Wanajeshi wa Ukraine.

Chanzo cha picha, Getty Images
Unawezaje kuyakabili?
Mashambulizi ya mabomu ya kuongozwa yanaweza kuzuiwa kwa kushambulia mrushaji wao. Ili kufanya hivyo, tunahitaji njia ambazo zinaweza kuangusha ndege kwa umbali mkubwa.
Tunazungumza juu ya makombora ya masafa ya kati (hadi kilomita 100) na masafa marefu (zaidi ya kilomita 100); huko Magharibi, safu kama hiyo imeainishwa kama - zaidi yae neo unaloweza kuona.
Makombora kama haya yanaweza kuwa ya ardhini au ya anga. Miongoni mwa mifumo ya chini ya ardhi ya kupambana na ndege katika huduma na kikosi cha wanajeshi wa Ukraine ni mfumo wa ulinzi wa anga wa Patriot wa Marekani (umbali wa kilomita 100), NASAMS wa Marekani na Norway-Norwe (umbali wa hadi kilomita 120), SAMP-T ya Ufaransa-Italia na makombora ya Aster-30 (umbali wa hadi kilomita 120, yaliyoboreshwa zaidi – ni hadi kilomita 150), mfumo wa ulinzi wa anga wa Usovieti S-200 (umbali wa kilomita 160-300 kulingana na aina ya kombora).

Chanzo cha picha, EPA
Kati ya makombora ya kurushwa kutoka angani, yale ya masafa marefu ni pamoja na AIM-120 AMRAAM, la kurushwa na F-16 (masafa ya kilomita 120, la kisasa linakwenda - hadi kilomita 180).
Lakini kombora la kawaida la masafa ya kati, AIM-7 (hadi kilomita 70), halifai tena kwa wabebaji wa mabomu ya kuongozwa, isipokuwa rubani wa ndege afanye makosa.
Tatizo kubwa la jeshi la Ukraine ni kwamba lina mfumo mmoja au miwili tu wa ulinzi wa anga wa masafa marefu wa ardhini, na bado hakuna ndege zilizo na makombora ya masafa marefu hata kidogo. Washirika wa Magharibi wanaahidi hivi karibuni kuipatia Kyiv F-16 na mifumo ya ziada ya ulinzi wa anga.
Mfumo wa ulinzi wa anga wa ardhini hauna uhamaji sawa na wa ndege na hulazimika kufanya kazi kwa kuvizia.
Kadiri inavyokuwa michache, ndivyo uwezekano wa kuwa mahali pazuri kwa wakati unaofaa unapungua.
Wakati huo huo, mfumo wa gharama kubwa wa ulinzi wa anga wa masafa marefu lazima ulindwe kwa uangalifu - kwa mfano, kutoka kwa mizinga au ndege zisizokuwa na rubani na kuisogeza karibu na mstari wa mbele ni hatari sana.
Kuiweka katika sehemu ya mbali ya ulinzi, katika tukio ambalo adui hushambulia nafasi za mbele, hupunguza safu ya ufanisi ya kurusha.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mara nyingi, ili kushambulia kwa uhakika, rubani anapaswa kukaribia shabaha, ambayo inamweka katika hatari ya kuwa katika safu ya ulinzi wa anga wa adui.
Kwa kuongezea, ndege za Urusi za Su-34, zinazotumiwa kurusha mabomu ya kuongozwa, pia zina silaha zenye nguvu ikiwa ni pamoja na makombora ya masafa marefu ya anga.
Lakini bado, ndege nyepesi ina kasi kubwa na ukwepaji wa haraka, na wakati wa kukutana nayo, ndege iliyobeba bomu ina nafasi ndogo sana ya mafanikio.
Ingawa, kwa kweli, mengi hutegemea ubora wa mafunzo.
Jambo jingine muhimu: kama vile Su-34 ya Urusi, F-16, pamoja na ndege ya kivita, inaweza kufanya kazi kama mshambuliaji na kushirikiana na safu nzima ya mabomu ya kuongozwa.
Na nchi za NATO zinazoisaidia Ukraine zina ndege nyingi kama hizo na mabomu.















