Je Ukraine kupewa ndege za kivita za F-16 kutaipa ushindi dhidi ya Urusi?

Na Katya Khinkulova

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kyiv imekuwa ikishinikiza washirika wake kutoa ndege za kisasa zaidi ili kukabiliana na mashambulizi ya Urusi

Ukraine imekuwa ikiwauliza washirika wake wa kigeni kuipa ndege za kivita tangu siku za mwanzo za uvamizi wa Urusi. Uidhinishaji wa mwisho wa Marekani kwa Denmark na Uholanzi kukabidhi baadhi ya F-16 zao huenda ukaleta mabadiliko muhimu katika jinsi vita hivi vinavyopiganwa.

Safari ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika nchi hizo mbili za Ulaya wiki iliyopita ilisababisha makubaliano kwa Ukraine kupokea, anasema, jumla ya ndege 61 - 42 kutoka Uholanzi na 19 kutoka Denmark.

Akiielezea kama "siku yenye nguvu na matunda", rais wa Ukraine alitoa shukrani nyingi kwa nchi zote mbili, na pia kwa Amerika kwa kuendelea kuunga mkono Ukraine.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe

Kama tu ilivyokuwa kwa mizinga ya Leopard hapo awali, na mifumo ya ulinzi ya anga ya Patriot kabla ya hapo, makabidhiano ya ndege za F-16 zilizotengenezwa Marekani zilitokana na mazungumzo ya muda mrefu.

Majibu ya Urusi

Mataifa yenye nguvu ya Magharibi, hasa Marekani, yamekuwa yakisita kuidhinisha makabidhiano haya, yakihofia yanaweza kusababisha makabiliano ya moja kwa moja na Urusi.

Hapo awali, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Alexander Grushko alionya kwamba nchi za Magharibi zitakabiliwa na "hatari kubwa" ikiwa zitaipatia Ukraine ndege hizo.

Balozi wa Urusi nchini Denmark, Vladimir Barbin, aliunga mkono maoni hayo siku ya Jumatatu, akiambia shirika la habari la Denmark "ukweli kwamba Denmark sasa imeamua kutoa ndege 19 za F-16 kwa Ukraine unasababisha kuongezeka kwa mzozo".

Ratiba ya utoaji wa ndege za F-16

Ukraine na wafuasi wake nje ya nchi wamekuwa wakifanya kampeni ya kukabidhiwa kwa ndege hizi kwa miezi kadhaa, wakisema kuwa ubora wa anga juu ya Urusi ndio njia pekee ya kuharakisha harakati za kuchukua tena eneo la Ukraine.

Msemaji wa Jeshi la Anga la Ukraine Yuri Ihnat alisema mwezi Mei: "Tunapokuwa na F-16, tutashinda vita hivi." Hili liliungwa mkono na wengi katika nchi za Magharibi, huku wataalam wa kijeshi wakisema kwamba kupigana vita bila msaada mkubwa wa anga kulimaanisha hasara kubwa zaidi ya wapiganaji ambayo ingeweza kuepukwa.

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen wakiwa katika ndege ya kivita ya F-16 katika uwanja wa Skrydstrup Airbase nchini Denmark, tarehe 20 Agosti 2023

Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen alieleza nia yake na mipango yake ya makabidhiano: "Lengo la utoaji huu ni kulinda Ukraine. Tunapanga kutoa ndege karibu na mwaka mpya, karibu sita kati yazo, kisha nane katika mwaka ujao na kisha nyingine tano."

Huku kukiwa na ari ya, uwasilishaji wa ndege utachukua miezi michache, kumaanisha kuwa Ukraine haitaanza kuzitumia kwa muda.

Mpango wa kutuma sehemu ya mwisho ya ndege za Denmark mwaka 2025 unapendekeza nia ya muda mrefu, ya kimkakati kwa upande wa washirika wa Ulaya wa Ukraine.

Ahadi kama hiyo ni muhimu kutokana na jinsi isivyowezekana kutabiri matokeo ya uchaguzi ujao wa rais wa Marekani.

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ndege ya F-16

F-16 ni ndege aina gani?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

F-16 inachukuliwa kuwa mojawapo ya ndege za kivita zinazotegemewa zaidi duniani.

Ikielezwa kama yenye majukumu mengi, inaweza kuwa na makombora na mabomu yanayoongozwa kwa usahihi, na inaweza kuruka kwa kasi ya 1,500mph (2,400km/h), kulingana na Jeshi la Anga la Marekani.

Uwezo wa kulenga wa F-16 utaruhusu Ukraine kushambulia vikosi vya Urusi katika hali zote za hali ya hewa na hata usiku kwa usahihi zaidi.

Ukraine inaaminika kuwa na makumi ya ndege za kivita - nyingi zikiwa ni MiG - zote zilianzia enzi ya Usovieti.

Urusi, kwa upande mwingine, hutumia ndege za kisasa zaidi ambazo zinaweza kuruka kwenye miinuko ya juu na kugundua ndege zingine kutoka mbali zaidi.

"Ndege ya Urusi inaweza kuona mara mbili hadi tatu na rada yake kuliko ndege zetu ," Yurii Inhat, msemaji wa Kamandi ya Jeshi la Anga la Ukraine aliambia Wall Street Journal. "ndege zetu ni vipofu tu, haziwezi kuona."

Kyiv inahitaji ndege za kisasa za kivita ili kusaidia kulinda anga yake dhidi ya mashambulizi ya mara kwa mara, mabaya ya makombora ya Urusi na ndege zisizo na rubani, na kusaidia mashambulizi yake ya kukabiliana na mashambulizi ya kusini na mashariki mwa Ukraine ambayo hadi sasa yamepata matokeo machache.

Kulingana na Lockheed Martin, mtengenezaji wa kijeshi wa Marekani anayetengeneza ndege hizo, kwa sasa kuna F-16 3,000 zinazotumika katika nchi 25.

Idhini ya Washington?

Usafirishaji na uhamishaji zaidi wa ndege za F-16 unahitaji kuidhinishwa na mamlaka ya Marekani kwa kuwa zimetengenezwa huko.

Pia kuna kipengele cha kisiasa kwa kuwa Marekani ndiyo mwanachama mwenye nguvu zaidi wa Nato. Mabadiliko hayo muhimu ya sera kuelekea Ukraine hayangetokea bila idhini yake.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, alituma barua kwa mawaziri wenzake wa Denmark na Uholanzi kuunga mkono makabidhiano hayo. "Inabakia kuwa muhimu kwamba Ukraine inaweza kujilinda dhidi ya uvamizi unaoendelea wa Urusi na ukiukaji wa uhuru wake," aliandika.

Muhimu zaidi kwa Ukraine, idhini hii inaweza kufungua njia kwa ndege nyingine za kivita, zisizo za Marekani, kutolewa kwa Kyiv pia.

Kabla ya kufunga mkataba wa F-16s na Denmark na Uholanzi, Volodymyr Zelensky alitembelea Uswidi ambako alitangaza kuwa mafunzo kwa marubani wa Ukraine kuhusu jeti za Uswidi za Jas 39 Gripen yameanza, jambo ambalo linadokeza kwamba jeti nyingi zaidi zinaweza kuandaliwa.

Mafunzo kwanza

Mafunzo ya kupeperusha, kuendesha na kudumisha ndege za F-16 yatakuwa muhimu. Mpango wa kina wa mafunzo, ulioandaliwa na muungano wa nchi za Magharibi kwa ajili ya kundi teule la marubani wa kijeshi wa Ukraine, umeanza nchini Denmark.

Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Denmark Troels Poulsen ana matumaini kwamba wataona matokeo ya mafunzo haya mapema 2024.

Wafanyikazi wa usaidizi pia wanahitaji kupewa mafunzo, wakati mifumo pana ya matengenezo ya jeti inahitaji kubuniwa na kuwekwa.

th

Chanzo cha picha, Ukranian Nation TV

Maelezo ya picha, Kamanda wa Jeshi la Wanahewa la Ukraine, Luteni Jenerali Mykola Oleshchuk, aliiambia TV ya taifa ya Ukraine kwamba ndege za F-16 zitalindwa vyema.

Kamanda wa Jeshi la Anga la Ukraine, Lt Jenerali Mykola Oleshchuk, alitoa hakikisho kwenye televisheni ya taifa kwamba Ukraine ina uwezo wa kutosha wa kulinda ndege hizo, na kuzifanya kuwa "janja kwa Urusi kuwinda".

Rubani wa ndege wa Kiukreni kwa jina la vita Moonfish, ambaye anapata mafunzo ya kuruka F-16s, aliambia kituo cha televisheni kuwa uzoefu wa kupambana na kiwango cha juu cha ujuzi wa Kiingereza ni mambo muhimu katika mchakato wa uteuzi.

Alisema marubani na wafanyakazi wa kiufundi katika kundi la sasa la wafunzwa wanajua Kiingereza vizuri.

Rubani alishiriki shauku yake kwa jinsi ndege hizo mpya zinavyoendelea. "F-16, ikilinganishwa na ndege tunazosafiria sasa, ni kama simu ya rununu karibu na kitufe cha mtindo wa zamani."

Uboreshaji wa kisasa upo njiani

Mpango wa mafunzo ya muda mrefu kwa marubani wa Ukraine unatarajiwa kuhama kutoka Denmark hadi Romania, nchi ambayo hivi majuzi ilinunua ndege 32 zilizotumika za F-16 kutoka Norway, kwa mkataba wa thamani ya Euro milioni 388 ($418 milioni). Romania pia ilinunua nyingine 17 kutoka Ureno.

Bucharest iko katika harakati za kuboresha jeshi lake la anga, kuchukua nafasi ya ndege za zamani za Soviet MiG-21.

Uboreshaji pia unaendelea kwa vikosi vya anga vya Uholanzi na Denmark. Wanapotoa ndege zao za 'zamani' kwa Ukraine, wanatazamia kununua ndege za hali ya juu pia.