Vita vya Ukraine: Changamoto za kuwafunza marubani ndege za kivita za F-16

Washirika wa Magharibi wanatarajiwa kutangaza mpango wa kutoa mafunzo kwa marubani wa Ukraine ili kuendesha ndege za kivita zilizotengezwa Marekani za F-16, wataka pokutana Brussels leo.
Lakini bado haiko wazi ni nchi gani zitakuwa tayari kutoa ndege hizo, kwa idadi ngapi na lini!
Kuipa Ukraine F-16 halitokuwa suluhisho wala kuwa jambo rahisi, anasema mkuu wa kikosi cha anga cha Norway, Meja – generali Rold Folland, anasema itachukua muda kwa Ukraine kuweza kuendesha ndege hizo ambazo zina mifumo migumu.
Tulikutana katika uwanja mkubwa wa mazoezi ya anga ya kijeshi huko Norway, yakikusanya nchi nyingine, Finland na Sweden. Yanajumuisha ndege 150, idadi kubwa kuliko ndege zote walizonazo Ukraine.
Generali Folland anasema, mafunzo hayo ni namna ya kuimiliki anga, ili kujiepusha na mapambano ya kizamani ya kivita, kama hali ilivyo Ukraine.
Kuwa na udhibiti wa anga kunahitaji kiwango kikubwa cha ujuzi, na Ukraine haina ujuzi huo. Hata kuipata F-16 ndogo bado itakua changamoto kubwa.
Ilimchukua Pulse, rubani kutoka Belgium miaka mitatu kuimudu kikamilifu F-16. Tumetakiwa kutumia jina lake ambalo sio rasmi. Ametuonesha ndege yake ya F-16, iliyotengenezwa miaka ya 1970, kabla yeye hajazaliwa.
“Inapaa kwa uhuru,” anasema. “Ila kuipaisha ndio eneo rahisi zaidi. Mambo mengine ndio magumu.”
Inajumuisha kujifunza kushughulika na rada, hisia na silaha. Ukraine ambayo kwa sasa ina marubani wengi kuliko ndege, inatumai kufupisha mafunzo yawe ya miezi mitatu.
Pulse anaiona sababu ya ndege hizo kupelekwa Ukraine. “Hilo ni muhimu,” anasema Pulse, “kwa sababu unaweza kutumia silaha yoyote kutoka ghala na Nato kwa ndege hii.”
Huku akionesha silaha katika ndege yake ya F-16; makombora ya kufyatua angani kuharibu ndege za adui na mabomu ya kushambulia ardhini.
Lakini kuna swali la namna ya kuzitunza ndege hizi. Kikosi cha Anga cha Norway, kama vilivyo vikosi vingine vya Ulaya, vimehamia kwenye ndege za kisasa ziadi F-35. Kwa kuzingatia hilo, maanake F-16 zitakuwa zinapatikana kwa ajili ya Ukraine.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Katika kambi ya kikosi cha anga ya Orland, wanatumia ndege mbili za F-16 kutoa mafunzo kwa mainjinia wa ndege hizo. Mafunzo yanachukua mwaka au ziadi kwa fundi mwandamizi.
“Huwezi tu kutoa ndege na kusema nenda,” Kanali Martin Tesli, kamanda wa kamba hiyo na rubani wa zamani wa F-16 anasema.
Anasema, utaratibu ni mrefu, vifaa vya ukarabati, programu na silaha. Ila pia anaelewa uhitaji wa kukiboresha kikosi cha Ukraine kuondokana na ndege kongwe za tangu utawala wa Kisoviet.
“Huko mbeleni, ikiwa hawatopewa ndege nyingine, hawatokuwa na uwezo wa kulinda anga yao."
Justin Bronk kutoka Royal United Services Institute, anasema Ukraine bila shaka inahitaji msaada wa wakandarasikutoka Ulaya ili kuzifanya ndege hizo ziendelee kufanya kazi. Swali lililo wazi, nchi gani iko tayari kupeleka watu wako Ukraine?
Profesa Bronk anaongeza kwamba, ni jambo la kulitarajia Urusi itashambulia kambi za kijeshi ikiwa Ulaya itapeleka ndege hizo. Jambo hilo ni hatari kwa injini moja tu ya F-16 ambayo mabaki yake yanaweza kuharibu njia ya kurukia.
Hizo ni sababu za msingi kwa nini Marekani kwa muda mrefu imesitasita kuipelekea Ukraine F-16.
Sio kuogopa mgogoro kuongezeka, lakini ni namna gani hizo ndege zitafanya kazi na namna ya kuzihudumia. Pentagon imeonya ni mchakato ugumu utakao gharimu pesa nyingi.
Luteni - Kanali Neils Van Hussen, rubani wa zamani wa F-16 wa kikosi cha anga cha Netherlands anasema, “hakuna silaha ambayo itabadili mweleko wa vita. F-16 itawezesha tu Ukraine kuendelea na vita kwa muda mrefu.”
Uhalisia wa vita hivi, hata Urusi yenyewe licha ya uwezo mkubwa wa kianga haijaweza kuidhibiti anga. Ulinzi wa ardhini unazuia Urusi kufanya hilo. Kuipa Ukraine ulinzi zaidi wa anga, itabaki kuwa kipau mbele cha Ulaya. Kuimarisha kikosi chake cha anga itakuwa ni lengo la muda mref












