Tetesi za soka Ulaya: Salah kutimkia Saudi Arabia Januari

Chanzo cha picha, Getty Images
Saudi Arabia inadaiwa iko tayari kufanya chochote kinachowezekana kumleta mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 33, katika ligi yao ya Saudi Pro Januari. (Gulf News)
Antoine Semenyo, 25, mshambuliaji wa Bournemouth na Ghana, anataka kujiunga na Liverpool ikiwa ataondoka Bournemouth. (Team Talk)
Semenyo anasemekana kuwa na mashaka kuhusu kujiunga na Tottenham, huku Arsenal na Manchester City pia zikionyesha nia. (Sun)
Marc Guehi, 25, beki wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, bado anataka kuhamia Liverpool, lakini Barcelona pia wanafuatilia maendeleo yake. (Team Talk)
Aston Villa wanachunguza uwezekano wa kumsajili mshambuliaji chipukizi wa Brazil Alysson, 19, kutoka Gremio. (The Athletic)

Chanzo cha picha, Getty Images
Roma wanafanya mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Uholanzi Joshua Zirkzee, 24, mwezi Januari. (Sky Sport Italia)
Roma wanataka kumsajili Zirkzee baada ya kukatisha mkopo wa mshambuliaji wa Ireland Evan Ferguson kutoka Brighton mwezi Januari. (Gazzetta)
Manchester United wanaonyesha nia ya kumtaka beki wa kati wa Elche na Austria David Affengruber, 24. (Team Talk)
Jack Grealish, 30, kiungo wa England, anafurahia maisha Everton na anataka kuendelea kucheza chini ya kocha David Moyes. (Football Insider)
Liverpool na Chelsea wote wanamfuatilia winga wa RB Leipzig na Ivory Coast Yan Diomande, 19, ambaye anatarajiwa kugharimu kati ya €80m – €100m. (Fichajes)















