Diogo Jota: Nyota wa Liverpool afariki katika ajali ya gari

Diogo Jota alijiunga na Liverpool kutoka Wolves mnamo 2020

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Diogo Jota alijiunga na Liverpool kutoka Wolves mnamo 2020 alijiunga na Liverpool kutoka Wolves mnamo 2020
Muda wa kusoma: Dakika 2

Mshambuliaji wa Liverpool Diogo Jota amefariki katika ajali ya barabarani akiwa na umri wa miaka 28.

Kaka yake mshambuliaji huyo wa Ureno Andre Silva pia alifariki katika ajali hiyo iliyotokea katika jimbo la Zamora nchini Uhispania.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 pia alikuwa mchezaji wa kulipwa, wa klabu ya daraja la pili ya Ureno ya Penafiel.

Gazeti la Guardia Civil limeiambia BBC Michezo kuwa Jota na kaka yake walifariki saa sita usiku siku ya Alhamisi saa za Uhispania.

Gari lao aina ya Lamborghini, liliacha njia baada ya tairi kulipulipuka na kuwaka moto.

Jota alifunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Rute Cardoso, ambaye ana watoto watatu, mwezi uliopita.

Hivi majuzi alicweka mtandaoni picha ya hafla hiyo, iliyofanyika tarehe 22 Juni.

Jota aliisaidia Liverpool kushinda taji la Ligi Kuu msimu uliopita na pia aliichezea Ureno walipoifunga Uhispania katika fainali ya Ligi ya Mataifa mwezi Juni.

"Shirikisho la Soka la Ureno (FPF) na soka yote ya Ureno imepata pigo kubwa," ilisema taarifa ya FPF.

"Diogo Jota alikuwa mtu wa ajabu, alicheza takriban mechi 50 za kimataifa, aliheshimiwa na wachezaji wenzake na wapinzani, na alikuwa mtu mwenye furaha kila wakati.

FPF imeomba shirikisho la soka barani Ulaya Uefa kutoa heshima kabla ya mchezo wa Euro ya Wanawake wa Ureno dhidi ya Uhispania siku ya Alhamisi.

Jota alianza taaluma yake na klabu ya Pacos de Ferreira kabla ya kujiunga na Atletico Madrid mnamo 2016 na aliichezea Porto kwa mkopo msimu wa 2016-17 , wakati kaka yake alipokuwa mchezaji mchanga.

"FC Porto inaomboleza," ilisomeka taarifa ya klabu.