Tetesi za soka Jumamosi: Man Utd wanafikiria kumnunua Delap

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Ipswich Town Liam Delap, 21, ikiwa hawataweza kumsajili mshambuliaji wa Sporting na Uswidi Viktor Gyokeres, 26, au mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 26, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Galatasaray. (GiveMeSport)
Manchester City wamedhamiria kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao na wameelekeza macho yao kwa kiungo wa kati wa Atalanta na Brazil Ederson mwenye umri wa miaka 25. (Fichajes )
Mshambuliaji wa Brazil Vinicius Jr, 24, yuko kwenye mazungumzo na Real Madrid ili kuongeza mkataba wake katika klabu hiyo, ingawa makubaliano hayajakamilika. (Relevo)

Chanzo cha picha, Getty Images
Borussia Dortmund huenda ikalazimika kumuuza winga Muingereza Jamie Gittens, 20, ambaye analengwa na Liverpool, Manchester United na Chelsea, ikiwa hawatafuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao. (Caught Offside)
Kiungo wa kati wa Crystal Palace na Uingereza Adam Wharton, 21, na kiungo wa kati wa Southampton Muingereza Tyler Dibling, 18, ndio wanaolengwa na Tottenham. (Football Transfers)
Everton itajaribu kumsajili mshambuliaji wa West Bromwich Albion mwenye umri wa miaka 21 Tom Fellows tena msimu wa joto. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
The Toffees pia wanahisi wanahitaji kuimarisha kikosi katika karibu kila eneo na wameanza kubainisha malengo yao ya msimu wa joto. (i Sport)
Tottenham itazingatia mustakabali wa Ange Postecoglou kama meneja ikiwa watashindwa kuifunga Aston Villa katika Kombe la FA wikendi hii. (NipeSport)















