Fahamu msafara wa kwanza wa Putin uliokwenda kupindua Ukraine

Chanzo cha picha, BBC / Claire Jude Press
Siku tatu baada ya Urusi kuivamia Ukraine, msafara mkubwa wa magari ya kivita yenye urefu wa kilomita 15.5 ulionekana kupitia satelaiti.
Asubuhi hiyo hiyo huko Bucha, kaskazini mwa Kyiv, Volodymyr Scherbynyn mwenye umri wa miaka 67 alikuwa amesimama nje ya duka lake kuu wakati zaidi ya magari mia moja ya kijeshi ya Kirusi yalipoingia mjini.
Volodymyr na satelaiti zote mbili zilikuwa mashahidi wa mwanzo wa mpango wa Rais Vladimir Putin wa kuupindua mji mkuu wa Ukraine na kuiondoa serikali.
Kwa maneno ya kijeshi – mkakati wa kijeshi wa kuondoa uongozi.
Saa arobaini na nane baadaye, tarehe 29 Februari 2022 msafara huo ulikuwa na urefu wa kilomita 56.
Lakini badala ya kupata ushindi wa haraka, mambo yalikwamba kwa wiki kadhaa.
Kisha inaonekana kutoweka mara moja. Nini kimetokea? Na kwa nini nguvu kubwa kama hiyo ilishindwa kufika Kyiv?
Timu ya BBC ilizungumza na makumi ya mashahidi; wakiwemo wanajeshi, idara za ujasusi za kitaifa na kimataifa, raia, wabobezi na ulinzi wa eneo, ambao wote walikutana na msafara huo.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Pia ilipata ufikiaji wa ramani na nyaraka za Urusi ambazo zilitoa mwanga kuhusu mpango wa msafara huo ulikuwa nini, na kwa nini ulishindwa.
Hadithi inaanzia kwenye mpaka wa Ukraine na Belarus kaskazini.
Akitoka nje kwa ajili ya kuvuta sigara yake ya kwanza siku hiyo, Vladyslav mwenye umri wa miaka 23 kutoka Kikosi cha 80 cha Mashambulizi ya Anga cha Ukraine aliona mwanga mwingi angani usiku.
"Nakumbuka nikitazama taa zikitokea msitu mzima. Mwanzoni nilifikiri ni taa za gari. Lakini baadaye nikagundua yalikuwa [makombora ya kujiendesha yenyewe]. Walikuwa wakiturushia."
Wakiwa wamepiga kambi ndani kabisa ya msitu wa eneo lililotengwa la Chernobyl, kikosi cha Vladyslav kilikuwa katika doria wakati magari ya kwanza ya Urusi yalipovuka hadi Ukraine.
"Dunia nzima ilikuwa ikitetemeka. Je, umewahi kuwa kwenye kifaru? Hakuna sauti inayofanana na hiyo. Ni chombo chenye nguvu."
Kama inavyopangwa katika tukio la shambulio lolote, Vladyslav na wengine wa brigade ya 80 walilipua daraja linalounganisha Chernobyl na mji mkubwa uliofuata, Ivankiv.
Warusi wangelazimika kupoteza muda kujenga daraja la pantoni badala, na kumpa Vladyslav na kitengo chake wakati wa kurudi Kyiv.
"Mwanzoni nilishangaa, kwa nini hatukuwazuia huko Chernobyl? Lakini tulihitaji kujifunza kuhusu adui yetu. Hivyo ndivyo tulivyofanya."
Hii karibu na mpaka wa Belarus, Waukraine hawakuweza kuanza kupiga risasi na kuhatarisha kuanzisha mgogoro mwingine.
Kipaumbele chao kilikuwa kwanza ni kuelewa mpango wa vita wa Urusi, kabla ya kutuma wanajeshi wake vitani.
Mpango makhususi wa Putin
Kinyume na ripoti nyingi za vyombo vya habari wakati huo, msafara huo wa urefu wa maili 35 (kilomita 56) kwa kweli ilikuwa vitengo kumi tofauti vya Kirusi, kulingana na Kikosi cha Wanajeshi cha Ukraine.
Nyaraka moja ya Urusi, iliyoonekana na BBC, inaonyesha ratiba ya shambulio hilo. Baada ya kikosi cha kwanza kuvuka hadi Ukraine saa 04:00 asubuhi mnamo tarehe 24 Februari, maagizo yao yalikuwa yasonge mbele moja kwa moja hadi Kyiv ikifika saa 14:55.

Chanzo cha picha, BBC / Claire Jude Press
Shambulio hilo lilitegemea sana mambo mawili - usiri na kasi.
Kulingana na Taasisi ya Huduma ya Kifalme, kwa kuficha mipango juu ya shambulio la mji mkuu, idadi ya wanajeshi wa Urusi wanaweza kuzidi vikosi vya Kiukreni kwa 12: 1 kaskazini mwa Kyiv.
Hata hivyo, usiri wa Putin ulikuja kwa gharama. Udanganyifu wake ndio uliofanikiwa zaidi, hata makamanda wake wengi hawakuwa wamearifiwa amri hiyo hadi saa 24 kabla ya uvamizi.
Kwa kiwango cha mbinu, hii iliwaacha katika hatari. Walikosa chakula, mafuta na ramani. Hawakuwa na zana sahihi za mawasiliano. Hawakuwa na silaha za kutosha. Pia hawakuwa wamejiandaa vizuri kwa hali ya hewa ya msimu wa baridi.
Wakiwa wamevaa mavazi ambayo hayaendani na msimu wa baridi huku wakiwa wamezungukwa na theluji, Warusi moja kwa moja walijipata ndani ya matope.
Raia walio karibu na Ivankiv wanaelezea kwamba wanajeshi wa Urusi waliwaambia wakulima wa Ukraine wawasaidie kuvuta vifaru vyao vilivyokuwa vimekwama kwenye matope.
Magari ya Urusi yalihitaji kutumia barabara za lami ili kuepuka dhiki ile na kuwalazimisha maelfu yao kukusanyika katika eneo moja.
Lakini kwa ukosefu wa mawasiliano kati ya vikosi vya wanajeshi, mara moja walianza kukusanyika katika eneo moja.
Kama mtaalam mmoja wa kijeshi alivyosema, "Hutakiwi kusafiri katika eneo la aadui kwa kutumia msafara mrefu. Hapana."
Umoja kwa ajili ya adui
Wakiwa wamekwama kaskazini mwa Kyiv na kukosa chakula na mafuta, Warusi pia walikuwa wamemdharau adui yao.
Kwa siku tatu Volodymyr Scherbynyn na wenzake waliojitolea, wengi wao wakiwa wastaafu, walikuwa wamejitayarisha kwa ajili ya kuwasili kwa msafara huo katika mji wao wa nyumbani wa Bucha.
Wakiwa wamejihami kwa bunduki ya rashasha kati ya 12, wakaaji wa eneo hilo waliondoa vibao vyovyote barabarani vyakuelekeza watu nj, wakaweka vituo vya ukaguzi, na kuandaa mamia ya mabomu ya petroli.
Na hatimaye, Jumapili asubuhi vifaru vya Urusi vikaingia mjini.

Chanzo cha picha, BBC / Claire Jude Press
Kwa takriban dakika thelathini, Volodymr na kitengo chake walipiga vifaru kwa kutumia kile kidogo walichokuwa nacho.
"Tulichoma moto magari mawili na kupunguza kasi ya msafara mzima," anasema Volodymyr.
Lakini baada ya hapo wakaanza kulipiza kisasi.
"Walipotuona tukirusha chupa walifyatua risasi," anasema Maksym Shkoropar mwenye umri wa miaka 30. "Nilikuwa muuza baa. Sikuwa na mafunzo yoyote ya kijeshi."
Kufikia mwisho wa nusu saa hivi, kila mmoja wa kitengo cha Volodymyr alikuwa amepigwa risasi na kukimbizwa hospitalini.
Lakini hata kutoka kwenye ghuba ya wagonjwa, Volodymr aliendelea kupigana.
Kupokea na kukagua msafara wa raia kutoka kote Mkoa wa Kyiv na kuwaita katika mamlaka ya Ukraine.
Upande mwingine wa vita alikuwa naibu gavana wa eneo la Irpin mwenye umri wa miaka 23, Roman Pohorilyl.

Chanzo cha picha, Maxar Technologies 2022
"Hatukulala kwa siku tatu. Mimi na mwenzangu tulikuwa tukiratibu simu kwenye ofisi ya baraza.
Tukipiga na kupokea simu kuhusu watu wetu pamoja na wahujumu.
Watu walikuwa wakiweka alama chini ya ardhi ili msafara ufuate."
Ni diwani wakati wa mchana, lakini pia Roman ni mtaalam wa kijasusi wakati wa usiku, anakusanya pamoja ripoti za kijasusi na zilizo kwenye mitandao ya kijamii.
"Wakiwa njiani kuelekea Kyiv, Warusi walikuwa wakichapisha video kwenye mitandao ya kijamii. Tuliweka tena video hizo ili kufichua mienendo yao. Walikuwa wakijionyesha tu, lakini kwa kufanya hivyo, walishikwa na aibu."
Lakini muhimu zaidi wakati wa shambulio la Kyiv, anasema Roman, ilikuwa hisia ya umoja kwa upande wa Ukraine.
"Kila mtu alikuwa akifanya jambo fulani. Ninakubali kwamba kulikuwa na shughuli nyingi sana katika siku hizo chache za kwanza. Lakini kulikuwa na wastaafu wanajeshi wakiwasaidia raia. Kila mtu alitaka kutetea jiji lake."
Katika miji na vijiji kote katika mkoa wa Kyiv, mamia ya mashambulizi yalifanyika dhidi ya msafara huo. Kuanzia kwa raia waliojihami na silaha za kujitengenezea nyumbani hadi askari wa miguu na silaha za kivita.
Mbinu zilizopitwa na wakati
Tofauti kabisa na Waukraine, wanajeshi wa Urusi mara kwa mara walionyesha kutokuwa na uwezo wa kufanya maamuzi madhubuti ardhini.
"Warusi wote walikuwa wamebeba masanduku makubwa ya chuma yaliyoandikwa 'siri'," anasema Vladyslav kutoka Brigade ya 80.
"Tulimkamata mmoja wakati wa kuvizia. Tulikuta ramani zao zimewekwa alama ya njia yao yote. Baada ya hapo tukajua mkakati wao wote."
Usiri wa Putin ulimaanisha kwamba makamanda wa Urusi hawakuwa na ufahamu wa mpango mpana wa vita.
Mbinu moja iliyofaulu ya Ukraine ilikuwa kulipua madaraja na mabwawa kabla ya msafara kufika, hivyo kuwalazimisha Warusi kubadili njia nyingine.
Kutegemea ramani za zamani na kwa mawasiliano duni, mara kwa mara wanajeshi wa Urusi walilemazwa na kutokuwa na uamuzi.
Picha kadhaa za satelaiti zinaonyesha magari ya Urusi yalizunguka huku na kule na wishowe kurejea pale walipoanzia.

Chanzo cha picha, BBC / Claire Jude Press
Shinikizo kutoka kwa mashambulizi ya anga ya Ukraine na vifaru, hatimaye msafara wa Urusi ulikwama nje kidogo tu ya mpaka wa jiji la Kyiv.
Kwa maelfu ya raia wanaoishi karibu na eneo ambapo wanajeshi hao walikwama walipitia matukio ya kutisha.
"Waliiba kila kitu kutoka kila mahali. Maduka," anasema Vladyslav. "Pia walitumia raia kama ngao yao."
"Nilipokuwa kwenye kituo cha ukaguzi, kutoka nyuma ya foleni za watu [wanajeshi wa Urusi] walianza kutupiga risasi. Raia walinaswa katikati ya vita hovyo," anasema Vladyslav.
Baada ya wiki nne zilizoonekana kuwa nyingi mnoo, Warusi hatimaye walianza kujiondoa.















