Vita vya Ukraine: Jinsi mzozo huo unavyoleta mpasuko wa familia nchini Urusi

Uliana at her brother Vanya's funeral

Chanzo cha picha, Anastasia Popova

Maelezo ya picha, Uliana akiwa kwenye mazishi ya kaka yake Vanya

Mwigizaji huyo mwenye umri wa miaka 37 anahudhuria mazishi ya Vanya, mwanajeshi wa Urusi aliyeuawa vitani nchini Ukraine. "Walisema alikufa shujaa," anasema Uliana wa Vanya mwenye umri wa miaka 23. "Niliwaza, 'Ina maana gani, kuwa shujaa?' Ni upuuzi. Sitaki shujaa aliyefariki kama kaka yangu."

Lakini babake Boris, ingawa pia alikuwa na huzuni, anajivunia kwamba mtoto wake Vanya alifariki akipigania nchi yake.

Maoni yake ni kwamba mzozo huo ni vita dhidi ya "serikali inayotangaza ufashisti".

Madai haya yanaunga mkono maneno ya Rais wa Urusi Vladimir Putin, ambaye anasema anasaidia kuondoa ushawishi wa Ukraine na kwamba serikali yake imefanya mauaji ya halaiki - madai ambayo hakuna ushahidi wowote.

"Kabla hii haijatokea kwa Vanya, hatukuwahi kuzungumzia vita," anasema Uliana akielezea uhusiano wake na baba yake. "Lakini baada ya kufariki tulikuwa na vita vikali kuhusu hilo."

Uliana discussing the war in Ukraine with her father Boris

Chanzo cha picha, Anastasia Popova

Maelezo ya picha, Uliana akizungumzia vita vya Ukraine na baba yake Boris

Katika filamu mpya ya BBC Storyville, baba na binti wanajadili vita - mazungumzo yanayofanyika katika familia nyingi nchini Urusi leo.

Ni vigumu kupata picha kamili ya jinsi watu nchini humo wanavyohisi kuhusu uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, kutokana na sheria inayoharamisha maoni yoyote yanayodhaniwa kuwa yanadhalilisha jeshi, au ambayo yanarejelea hatua ya kijeshi kama vita badala ya "operesheni maalum ya kijeshi."

Lakini utafiti uliochapishwa mnamo Novemba 2022 na kikundi huru cha utafiti cha Urusi ulionyesha kuwa inagawanya vizazi - 75% ya waliohojiwa wenye umri wa miaka 40 na zaidi walisema wanaunga mkono vita, ikilinganishwa na 62% ya wale wenye umri wa miaka 18-24.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Msanii wa filamu wa Urusi Anastasia Popova anasema hili lilimkera mwenyewe kwa mtazamo alipokuwa akisafiri kote nchini humo kurekodi filamu hiyo.

"Nilishuhudia tofauti nyingi zikijitokeza kati ya familia. Watoto wao wengi walikuwa dhidi ya vita, na wazazi wao - kizazi kilicholelewa wakati wa Muungano wa Sovieti, ambao walitazama televisheni [ya serikali] mchana na usiku - waliunga mkono vita. Nina tofauti sawa na hiyo katika familia yangu," anaongeza, akisema baba yake anaunga mkono hatua ya kijeshi.

Kutegemea runinga ya serikali kwa habari kunamaanisha kuamini simulizi rasmi ya serikali ya Urusi siku baada ya siku.

Uliana, na watu wengine wa rika lake, wana uwezekano mkubwa wa kupata habari zao kutoka kwa vyombo vingine, kama vile YouTube na mitandao ya kijamii.

"'Samahani' siwezi kuelezea huzuni ninayohisi ndani yangu," anasema Uliana.

Anasema vita vimebadilisha watu.

"Ninatazama watu kwenye vituo vya treni [huko Moscow]. Wanasoma habari, kisha wanaangalia pembeni. Wameacha kutazamana machoni."

Popova anasisitiza kuwa nje ya miji mikubwa, uungaji mkono vita ni mkubwa sana, bila kujali idadi ya watu.

Anasema hii ilionekana wazi alipokuwa akirekodi mazishi ya Vanya katika kijiji chao cha Arkhangelskoe, kilomita 97 nje ya Moscow.

Uliana speaks of this moment of recognition too.

Pia, Uliana anazungumzia kipindi hicho.

"Nilipokuwa nikiwatazama watu hao, ilinijia kwamba waliamini kabisa maneno waliyokuwa wakisema," anasema, "[ambayo yalikuwa ni] Vanya alikufa kama shujaa, mzalendo wa kweli ambaye alitetea nchi yake.

"Najua kuna kitu hakiko sawa. Nani tunapaswa kumuokoa huko? Wavulana wetu wanakufa kwa nini? Sikuwahi kufikiria maishani mwangu kwamba kaka yangu angeletwa kwangu akiwa kwenye jeneza la zinki."

Vanya alikuwa mdogo wa ndugu wanne, na mtoto wa kiume wa pekee.

"Alikuwa mtoto aliyependwa," Uliana anasema.

"Alikuwa amepata malezi na mafundisho mengi," Boris anaelezea.

Alikwenda "Shule ya sanaa, shule ya muziki, michezo ... nilimuwezesha kila kitu nilichotamani kwake."

Baada ya kuondoka nyumbani, Vanya alijiunga na taasisi ya fasihi huko Moscow kusoma uandishi wa ubunifu na pia aliigiza katika maeneo mbali mbali ikiwa ni pamoja na ukumbi wa michezo wa Bolshoi.

Boris anasema hii ilisababisha huzuni kubwa kwa Vanya, ambaye alipendana na msichana ambaye hakutaka kuolewa.

"Huu ni ulimwengu wa maonyesho. Kwa maoni yake binafsi kuhusu maisha na vigezo vyake vya maadili. Badala ya maadili ya familia, kumeanzishwa mahusiano ya wazi kati ya wanaume na wanawake," anasema Boris.

Vanya

Chanzo cha picha, Ivan

Maelezo ya picha, Vanya alihusika sana katika sanaa ya Moscow kabla ya kujiunga na jeshi

Uliana anasema Vanya alionekana kuwa na furaha sana kwenye ukumbi wa michezo, lakini baba yake alisema kwamba ilizua aina fulani ya matatizo kwa mtoto wake.

"Hakuridhika na maoni yao juu ya ulimwengu, kwamba wao daima wama mtazamo hasi juu ya Urusi; kwamba Warusi sio chochote kwao; kwamba mababu zao, historia nzima ya Urusi imezingirwa na upuuzi mtupu. Anaelewa kuwa yeye hayuko hivyo. Tulizungumzia hilo na kujadiliana sasa afanye nini?"

Kwa hivyo, Boris anasema, yeye na Vanya walikubaliana kwamba ajiunge na jeshi.

"Kwa maisha katika sanaa ya ubunifu.. unahitaji uzoefu wa maisha," anasema Boris. "Unaweza kuipata wapi? Tuliamua afuate nyayo za waandishi tajika. Nalo ni jeshi."

Vanya alijiunga na jeshi kama aliyesajiliwa - na kisha, akataka majukumu mengine ya kumpa changamoto zaidi, akachukua mkataba wa jeshi.

Alikuwa mwanamaji anayeishi katika mji wa Sevastopol katika Crimea inayokaliwa na Urusi wakati Urusi ilipoanzisha mashambulizi yake makubwa katika miji kote Ukraine mnamo Februari mwaka jana. Aliambiwa apigie familia yake kuiaga kabla ya kutumwa katika mji wa bandari wa Mariupol nchini Ukraine.

"Tulizungumza kwa muda mrefu, zaidi ya saa moja," anasema Uliana.

"Alikuwa akibubujikwa na machozi machoni pake. Nikasema: 'Vanya, nionyeshe ulicho nacho hapo.' Alinionyesha bunduki ya rashasha. Kama vile alivyokuwa akinionyesha vitu vya kuchezea nilipokuwa mtoto."

Boris anaonyesha video ya Vanya aliyomtumia ujumbe. "Tunachokifanya ni sawa kabisa," Vanya anasema. "Hamjambo nyote. Nitaandika nikifika huko. Nawapensa sana."

"Hayo yalikuwa maneno yake ya mwisho," Boris anasema.

Uliana looking shocked as she talks to her father about the war

Chanzo cha picha, Anastasia Popova

Aliuawa karibu na kiwanda cha chuma cha Azovstal huko Mariupol mnamo Machi 15.

Kifo chake kilileta mtazamo tofauti kati ya Uliana na Boris juu ya vita.

Boris anamwambia Uliana kwamba yeye ni mdogo sana kukumbuka kile anachorejelea kama "ndugu" wa jamhuri za Muungano wa Sovieti. Anasema kuwa kuanguka kwa usovieti huo "kulimaliza ari ya vizazi vingi vijavyo, wakidhania kuwa Warusi walikuwa adui zao".

Lugha yake inamkumbusha Rais Putin, ambaye ameita kuanguka kwa himaya ya Soviet "janga kubwa zaidi la kisiasa la Karne ya [20th]".

Ukraine ilijitangazia uhuru muda mfupi kabla ya Muungano wa Kisovieti kusambaratika mwaka 1991.

Rais wa Urusi pia analaumu NATO na nchi za Magharibi kwa vita, ambavyo anadai vinajaribu kudhoofisha na hatimaye kuiangamiza Urusi.

Boris pia, anafuatilia simulizi.

"Katika muktadha wa leo, 'Kukataa vita' inamaanisha kitu kimoja tu," Boris anamwambia Uliana. "Inamaanisha 'Kifo kwa Warusi'. Haya ni mapambano kwa ulimwengu wa Kirusi, kwa nafsi ya Kirusi, kwa utamaduni wetu."

Uliana anasema kuwa kwa tofauti zao zote anataka kudumisha uhusiano na baba yake.

"Siwezi kwenda vitani dhidi ya baba yangu mwenyewe. Siwezi kusema 'nakuchukia kwa sababu hatukubaliani.' Ninachoweza kusema ni 'Baba, sikubaliani na wewe. Hilo ndilo ninaweza kusema.'