Vita vya Ukraine: Meli za Urusi zenye silaha za nyuklia zajiweka tayari ikiwa ni mara ya kwanza kwa miaka 30

Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images

Meli za jeshi la wanamaji la Urusi zimeanza kuingia katikati ya bahari zikiwa na silaha za nyuklia. Hatua hiyo ni kwa mara ya kwanza katika miaka 30 iliyopita, kwa mujibu wa taarifa toka shirika la kijasusi la Norway.

Ripoti yake ya kila mwaka, iliyotolewa Februari 13, inasema kwamba sehemu kubwa ya vikosi vya nyuklia vimewekwa kwenye manowari na meli zilizoko Kaskazini.

Kwa kuzingatia kudhoofika kwa uwezo wa kawaida wa ulinzi, umuhimu wa silaha za nyuklia kwa Urusi umeongezeka sana, waandishi wa ripoti wanaandika.

"Mbinu za Silaha za nyuklia ni tishio kubwa hasa katika matukio kadhaa ya uendeshaji ambayo nchi za NATO zinaweza kushiriki," taarifa za shirika hilo la kijasusi ilisema.

Tovuti ya Norway The Barents Observer, ikitoa maoni juu ya ripoti hiyo, ikiita hiyo dhana ni"habari za kusisimua."

"Katika nyakati za Usovieti, meli kutoka Severomorsk zilikwenda baharini na silaha za nyuklia, lakini hakujawa na ushahidi kwamba silaha za nyuklia za nguvu ndogo ziko baharini tangu wakati wa vita baridi," chapisho linasema.

Siku moja kabla, Naibu mkuu wa kijasusi wa Norway, Lars Norram, alisema Urusi itakuwa "kimabavu na kijeshi" zaidi katika miaka ijayo.

Inaendelea kutokana na ukweli kwamba propaganda na uendeshaji wa maoni ya umma katika miaka ijayo utaongezeka tu, na Moscow itatafuta uhusiano wa karibu zaidi na tawala za kimabavu duniani kote.

Nordam aliita vita ni "janga kwa Urusi", kulingana na makadirio yake, maelfu ya aksari wake wameuawa au kujeruhiwa.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi bado haijatoa maoni kuhusu ripoti hiyo kutoka shirika la kijasusi la Norway.

Meli sita

Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Silaha za nyuklia (TYAZ) ni zana ndogo za nyuklia zilizoundwa ili kulenga shabaha eneo mahususi au kulenga walipo askari wa adui kwenye uwanja wa vita au eneo karibu zaidi.

Katika meli, hizi zinaweza kubeba aina zote za silaha na makombora ya kusafirishwa kwa meli, ndege, na hata silaha za chini ya maji - torpedoes, mabomu ya kina na nanga. Wakati wa Vita Baridi, meli nyingi zilibeba silaha za nyuklia - kwa mfano, frigate class.

Nguvu ya mabomu haya ya nyuklia inaonyeshwa na jaribio la torpedo la nyuklia ya Soviet mnamo Oktoba 10, 1957. Kwa pigo moja la manowari kutoka umbali wa kilomita 10, maeneo sita ya mafunzo yaliharibiwa mara moja - meli nne manowari mbili. Majaribio sawa na hayo yalifanywa nchini Marekani.

Mnamo Mei 29, 1990, Marais wa Soviet na Marekani Mikhail Gorbachev na George W. Bush walikubaliana kupunguza silaha za nyuklia za aina hii na kupunguza utayari wao wa kupambana. Tamaa ya kupunguza TYAZ ilikuwa ya pande zote, lakini mpango huo ulichochewa zaidi na Soviet.

"Mkataba wa Makubaliano ya kiungwana"

Haja ya kurudisha silaha za nyuklia za TYAZ katika meli za Urusi ilitangazwa mnamo Agosti 2022 na mkurugenzi wa heshima wa kisayansi wa Kituo cha Nyuklia cha Sarov, Msomi Radiy Ilkaev. Kulingana na yeye, walijadili hili na kamanda mkuu wa Jeshi la Wanamaji la Urusi, Admiral Vladimir Vysotsky.

"Tuna nguvu kubwa baharini na lazima tuwe na meli zinazofaa za kulinda. Lakini kujenga meli kama hiyo, inachukua miaka 100, ni ghali sana. Wakati huo huo, tunahitaji kujilinda kwa njia zilizopo - kurudisha nyuklia ya TYAZ , pia ziko kwenye maghala, - alisema mwanataaluma huyo. Kwa nini? Wengi sasa wanasema kwamba meli zetu hazina nguvu kama ilivyokuwa zamani."

Alikumbuka kuwa uamuzi wa kupunguza silaha za nyuklia hizo ulifanywa na Rais wa Soviet Mikhail Gorbachev kwa msingi wa "makubaliano ya kiungwana" na Wamarekani.

Je, kuna silaha ngapi za nyuklia za aina hii duniani?

Kulingana na wataalam wa kujitegemea, Urusi ilikuwa na vitengo 2,000 vya silaha za nyuklia zisizo za kimkakati.

Zaidi ya 500 kati ya hizo ni za kupambana na meli, kukabiliana na manowari, makombora ya kupambana na ndege, torpedoes pamoja na makombora 250 ya nyuklia ya KR-55 "Granat".

Pia kuna mamia kadhaa ya makombora ya nyuklia ya TYAZ na mabomu ya kupigwa kwenye kina ambayo yanaweza kutumiwa kwenye anga za majini.

Marekani, kulingana na makadirio hayo hayo, ina takriban silaha 500 za kimbinu za kinyuklia - takriban mabomu 400 aina ya B-61 na makombora 100 ya baharini yenye vichwa vya nyuklia.

Kati ya nchi tano rasmi za nyuklia, ni Uingereza pekee ambayo haina silaha za kimbunu za nyuklia - ina silaha za kimkakati tu.

Ufaransa ina vichwa 60 vya kivita vinavyotumia mbinu za anga. Hakuna data iliyothibitishwa juu ya China, lakini ina zana za nyuklia za TYAZ.

Mabomu mengi ya nyuklia yalitengenezwa katika miaka ya 1950-60 na tayari yamefika ukomo kirasilimali. Kulingana na data rasmi ya Kirusi, mwanzoni mwa miaka ya 2000 silaha kadhaa za nyuklia zilihamishiwa kwenye vituo vya uhifadhi va kitaifa huku asilimia 30% ya silaha hizo zilisambaratishwa.