'Pamoja na kushindwa kuiangamiza Ukraine, Putin amefanikiwa kuiharibu Urusi'

Chanzo cha picha, Ilya Barabanov/BBC
Katika kuadhimisha mwaka wa kwanza wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, mwandishi wa BBC Idhaa Kirusi Ilya Barabanov anaangazia mzozo ambao umeleta misukosuko katika maisha ya mamilioni ya watu, akiwemo yeye mwenyewe.
Mwanzo wa mwaka 2022 ulikumbwa na wasiwasi lakini kwa upande wangu hii haikuhusishwa na mazungumzo ya vita inayokuja. Mamluki wawili kutoka Kundi la Wagner la Yevgeny Prigozhin walikuwa wakinishtaki kwa kuwaharibia jina. Mimi na mke wangu tulijadili ikiwa tungelazimika kuondoka Urusi. Hatukujua nini kingetokea baadaye..
Kesi ya mamluki hao iliwasilishwa dhidi yangu na mwandishi mwenzangu wa Idhaa BBC Kiarabu, Nader Ibrahim,kwasababu tulifanya taarifa ya pamoja, kuangaza uwepo wa mamluki wa Urusi nchini Libya mnamo 2019-2020.
Tulionyesha uthibitisho kwamba sio tu kwamba walikuwa huko, wakipigana dhidi ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na kumuunga mkono Jenerali Khalifa Haftar, bali pia walikuwa wamefanya uhalifu wa kivita dhidi ya raia.
Kufuatia ufichuzi huo mamluki wawili tuliyokuwa tumewataja katika makala hayo waliishitaki BBC katika mahakamani huko Moscow.
Mnamo Januari 2022, kesi ilikuwa bado inaendelea na nilikuwa na wasiwasi kwamba ingeendelea mbele licha ya kuwa na msaada wa mawakili waliohitimu nisingeweza kulinda sifa yangu - au hata uhuru wangu.
Miezi sita baadaye mmoja wa walalamikaji, ambaye alidai kuwa kamwe hakuwa sehemu ya kundi la Wagner, aliuawa katika mapigano nchini Ukraine kama mamluki wa Wagner. Na wa pili alipoteza kesi yake dhidi yetu.
Licha ya hayo hatimaye niliishia kuondoka Urusi lakini kwa sababu tofauti kabisa.
Mapema Februari 2022, jeshi la Urusi lilipokuwa likiongezeka kwenye mipaka ya Ukraine na mazungumzo ya vita yakizidi kuongezeka, nilifika Kyiv ili kuripoti kuhusu hali ya wasiwasi iliyoongezeka.
Lakini moyoni bado sikuamini kwamba vita vingetokea. Niliendelea kumwambia mke wangu kwamba wiki mbili baadaye ningerudi nyumbani, huko Moscow.

Chanzo cha picha, Ilya Barabonov/BBC
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mnamo Februari 14 mimi na mwandishi mwingine wa BBC Slava Khomenko tulienda mji wa Vovchansk katika eneo Kharkiv, karibu na mpaka wa Urusi.
Siku 10 baadaye mji huo ulikuwa chini ya udhibiti wa Urusi, lakini wakati huo wakazi walipuuza uwezekano huo.
Wakati mimi na Slava tulipowashinikaza kuuambia watafanya nini endapo uvamizi utafanyika kweli, kwa kutojali walisema: "Tulinusurika mikononi mwa Wajerumani kwa njia moja au nyingine." Walizungumza juu ya Vita vya vya pili vya Dunia.
Njiani kurudi Kyiv tulisimama karibu na kibao cha kuelekeza barabara kuelekea mji wa Peremoha, kwa Kiukreni inamanisha "ushindi", kupiga picha karibu nayo.
Kwa kuwa hakuna hata mmoja wetu aliyefikiri kwamba vita vingeanza, tulifikiri hii ingetukumbusha siku hizo zilizojaa wasiwasi.
Mnamo tarehe 24 Februari niliamshwa katika chumba changu cha hoteli huko Kyiv wakati mfanyakazi aligonga mlango na kusema: "Bwana, huenda tunakabiliwa na shambulio la bomu.
Nilishuka kwenye eneo la hoteli lililotengwa kujikinga dhidi ya mabomu na jhapo nikaona jinsi watoto wa wanandoa watalii wa Uhispania walivyokuwa wakicheza ishara wazi kwamba hawana habari lililokuwa likiendelea litakuwa na athari gani.
Hawakuelewa kuwa ving'ora vilivyokuwa vikilia ni ishara ya mashambulizi ya angani na pia kwa nini hawakuweza kutoka nje.
Katika siku chache zilizofuata nilitumia muda mwingi katika nyumba ya rafiki yangu Kyiv, ambapo kundi la waandishi wa habari lilikusanyika, kubadilishana taarifa na kuzungumza.
Gorofa hiyo ilikuwa na shughuli nyingi, lakini sehemu nyingine ya Kyiv, Podil, ambayo kwa kawaida ilikuwa na watu wengi, ilisalia mahame.
Nyumba ya rafiki yangu ilikuwa na roshani inayoelekea upande wa kaskazini - tulisimama hapo, tukitazama miji ya Bucha, Hostomel na Irpin. Tuliweza kusikia kishindo cha silaha na hapo tukajua kwamba jeshi la Urusi lilikuwa likijaribu kuteka maeneo hayo.

Chanzo cha picha, Ilya Barabonov/BBC
Wiki sita baadaye, wakati majeshi ya Urusi yalipoondoka katika miji na vijiji hivyo - ikielezea uamuzi huo kama "hatua ya nia njema" - ulimwengu baadaye ulibaini uhalifu wa kivita ambao vikosi hivyo vilifanya huko.
Mamlaka ya Urusi kama ilivvyo ada yake ya muda mrefu, alidai hii ilikuwa taarifa za uwongo "zilizotungwa na huduma za usalama za nchi za magharibi".
Mwishoni mwa Februari 28 nilivuka kutoka Ukraine hadi February Moldova kupitia mtu Dniester.
Nilikuwa nishagundua kwamba itakuwa vigumu kurudi nyumbani Moscow . Baada ya kuripoti kuhusu vita vya Urusi dhidi ya Ukraine, nnelikwa naiweka katika hatari ya kukamatwa na kufungwa jela kwa miaka mingi.
Moldova ilikuwa imejaa wakimbizi wa Ukraine na wenyeji walikuwa wakifuatilia kwa makini kinachoendelea nchini humo.
Wengi walikuwa na hofu endapo vikosi vya Putin vitafika Odesa,basi nchi yao ndogo ingekuwa shabaha rahisi kwa wavamizi Warusi. Wakati huo haikuwa wazi kwamba Ukraine inaweza kukabiliana na uchokozi wa Moscow.
Nilisafiri kwa treni kutoka Moldova hadi Romania. ITreni hiyo pia ilikuwa imejaa wakimbizi.
Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne aliniuliza: "Tutarudi nyumbani hivi karibuni, sio?" Sikujua nimju nini.
Treni iliposimama kwenye stesheni, mimi na abiria mmoja tulienda kwenye gari la kuuza vinywaji tukavuta sigara pamoja kutafakari tu kinachoendelea.
"Watu hawa wote," alisema kwa masikitiko, "wakijaribu kutoroka, treni zimejaa wakimbizi. Putin nafikiri vita hivi vitamsaida nani?
Sikujua la kusema kwa hilo pia, na mwaka mmoja baadaye bado sijui la kusema














