Vita vya Ukraine: Kwanini vifaru vinaonekana muhimu katika vita hivi kuliko silaha nyingine?

Faisal Titumir, BBC News Bangla, Dhaka

Ukraine

Chanzo cha picha, Huw Evans Picture Agency

Vifaru vya "Leopard 2" au "Mwan Abrams" vinajadiliwa sana kwa sasa katika vita vya Urusi na Ukraine.

Kifaru cha kwanza cha Leopard 2 kinatengenezwa na Ujerumani, ambapo hatimaye nchi hiyo imekubali kuvipeleka Ukraine baada ya wiki kadhaa za mazungumzo na kusita kuamua.

Ndani ya saa chache baada ya kutangazwa kuwa Ujerumani itatoa vifaru 14 vya Leopard 2 kwenda Ukraine, Marekani ilisema pia itapeleka vifaru 31 vya Abrams vya M1 nchini Ukraine katika vita dhidi ya Urusi.

Akikaribisha matangazo haya mawili, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema, "Hii ni hatua muhimu katika kuelekea ushindi."

Kwa jumla, Ukraine inatarajia kupokea angalau vifaru 100 kutoka Ulaya. Ambavyo vinaaminika kuwa na jukumu muhimu katika kuokoa maeneo yaliyotwaliwa na Urusi. Lakini je ni kweli vinaweza kufanya jukumu hilo?

Leopard

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ujerumani imetangaza kupeleka vifaru 14 vya Leopard 2

Je, mizinga italeta tofauti gani?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Takriban nchi 30 zimetoa msaada wa kijeshi kwa Ukraine tangu Urusi ilipoanzisha mashambulizi yake Februari mwaka jana.

Walakini, wakati huu wote walitumia vifaru ya T-72, ambayo ilikuwa na umri wa miaka 30 kutoka enzi ya Soviet na vilikuwa tayari viko Ukraine.

Kando na hayo, Poland, Slovakia na Jamhuri ya Czech zimepeleka takriban vifaru 200 zaidi vya T-72 nchini Ukraini.

Lakini tangu vita vilipoongezeka, haswa katika miezi michache iliyopita, Rais wa Ukraine Zelensky amekuwa akizitaka nchi za Magharibi kuipa vifaru na mizinga ya kisasa. Na anadai kwamba ikiwa Ukraine itapata vifaru 300, inaweza kushinda vikosi vya Urusi na kurejesha maeneo yaliyotwaliwa.

Vifaru ni magari ya kivita, silaha nzito za kivita ambazo zinaweza kufyatua makombora kutoka umbali mrefu, na kuharibu mizinga ya adui pia.

Sasa wakati wa vita vya kukera, vifaru vya kisasa vya Leopard 2 na M1 Abrams vitaisaidia Ukraine kujenga upinzani mkali dhidi ya Urusi, anasema Syed Mahmud Ali, mtaalam wa kijeshi na profesa katika Chuo Kikuu cha Malaya huko Kuala Lumpur, Malaysia.

"Ikiwa wale watakaozitumia watafunzwa na kupewa vifaa vyote wanavyohitaji, vinaweza kutumika kuanzisha operesheni ya kukera ambayo itasambaratisha ulinzi wa Urusi."

Bwana Ali alikuwa akisema kwamba viongozi wa nchi za Magharibi wanahofia kwamba majeshi ya Urusi yatafanya mashambulizi makubwa mwishoni mwa majira ya baridi, na safari hii lengo la kuwapa vifaru ni ili Ukraine iweze kukabiliana na kurejesha eneo lililopotea kabla ya mashambulizi hayo.

Kwa hiyo, kupeleka vifaru Ukraine kwa wakati huu ni muhimu kulingana na maoni ya kisiasa na kijeshi.

Abrams tanks

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marekani imetangaza kupeleka vifaru 31 ana ya Abrams

Kiasi gani cha vifaru Ukraine inapokea na lini?

Ukraine haipati vifaru 300 ambavyo inadai inahitaji ili kushinda vita. Lakini mwandishi wa BBC, Jonathan Beal, anafikiri kwamba ikiwa hata vifaru 100 kutoka nchi za Magharibi vitaifikia Ukraine - inaweza kuleta mabadiliko makubwa katika uwanja wa vita.

Kwanza kabisa, Uingereza ilitangaza kutuma vcifaru 14 vya Challenger 2 kwenda Kiev. ifaru hivi vya muda mrefu vina uwezo wa kushambulia kikamilifu.

Ujerumani pia ilisema itawapa vifary aina ya Leopard 14, ambavyo ni vyepesi, rahisi kutumia, haraka na hutumia mafuta kidogo.

Na Marekani inatoa vifaru 31 vya Abrams. "Kikosi cha mizinga nchini Ukraine kina vifaru 31" - alisema Rais wa Marekani Joe Biden.

Hata hivyo, kwa vile Ujerumani imekubali kutoa vifaru vya Leopard 2, hakuna tena kikwazo kwa nchi nyingine za Ulaya kutuma vifaru nchini Ukraine. Kwa sababu kuna takriban vifaru elfu 2 vya Leopard katika nchi kadhaa kote Ulaya.

Vinatengenezwa nchini Ujerumani na leseni ya kuuza nje pia iko mikononi mwao. Wakati huo huo, Poland imesema kuwa mbali na Leopard, watatuma vifaru vya ziada 50-60 vya enzi ya Soviet huko Ukraine.

Hata hivyo, bado inaweza kuchukua miezi kadhaa kwa vifaru hivi kufikia uwanja wa vita. Wataalamu wanasema Marekani itanunua vipya kutoka kwa wakandarasi binafsi na kisha kuvisafirisha. Haitawapa vifaru vyake vilivyohifadhiwa.

Vifaru vya Leopard 2 vinatarajiwa kuwasili baada ya miezi miwili hadi mitatu.

Challenger Two

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uingereza imetangaza kupeleka vifaru 14 vya Challenger Two

Changamoto zitakazoikabili Ukraine baada ya Kupata vifaru

Hakuna shaka kwamba vikosi vya Ukraine vitakuwa na nguvu zaidi ikiwa watapata vifaru iliyoahidiwa. Kadiri kasi yao ya kushambulia inavyoongezeka, ndivyo walengwa wanaongezeka. Na pia inawezekana kurudisha nyuma vikosi vya Urusi ikiwa unaweza kushambulia ipasavyo kwa kupitisha mkakati sahihi.

Hata hivyo, mtaalamu wa Samar Syed Mahmud Ali anaona changamoto kadhaa katika kufikia lengo hilo. "Tatizo moja ni kwamba silaha za kisasa ni ngumu sana, zinahitaji mafunzo ili kuziendesha ipasavyo. "Vikosi vya Ukraine vimekuwa vikiendesha vifaru vya zamani kwa muda mrefu, sasa wanapaswa kupitia mafunzo mapya."

Putin

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Putin akiwa katika mkutano kwa njia ya video kujadili kuhusu hali ya vita

Urusi inasema nini kuhusu vifaru hivi?

Urusi imejibu kwa hasira tangazo kwamba Ujerumani na Marekani zinatuma vifaru nchini Ukraine. Ikulu ya Kremlin inasema uamuzi huo utazidisha mzozo zaidi. Wataalamu pia wanaamini kwamba hatima ya mzozo wa Russia na Ukraine itajulikana kwenye uwanja wa vita, badala ya kwenye meza ya mazungumzo.

Urusi pia ina vifaru vya kisasa vyake yenyewe. Walakini, itajulikana siku zijazo ni silaha ngapi ambazo Urusi itatumia dhidi ya vifaru hivi vya hali ya juu.

Lakini Bw. Ali anaamini Urusi pia itakuwa na jibu. "Hatujaona matukio mengi hivi majuzi yakitumika ipasavyo katika mapambano dhidi ya wapinzani. Nchini Iraq, Afghanistan, vikosi hivi havikuwa na vifaru hivyo. Kwa hiyo hakuna mfano wa mashambulizi ya kukabiliana nayo. Lakini naweza kudhani kwamba Urusi ina au itakuwa na silaha za kisasa za kukabiliana na vifaru hivyo.