Je vita vya Putin vimefeli na je Urusi inataka nini?

.

Chanzo cha picha, Reuters

Wakati Rais Vladmir Putin alipotuma wanajeshi 200,000 nchini Ukraine tarehe 24 Februari 2022, alidhania angeingia katika mji mkuu wa Kyiv kwa siku chache na kuiangusha serikali. Lakini baada ya msururu makabiliano ya vita mpango wake wa kuivamia Ukraine umekwisha lakini vita vya Urusi havijaisha.

Je lengo la Putin lilikuwa lipi?

Hata kufikia sasa, kiongozi wa Urusi anaelezea uvamizi mkubwa zaidi wa Ulaya tangu mwisho wa Vita vya Pili vya Dunia kama "operesheni maalum ya kijeshi". Sio vita kamili ambavyo vimeshambulia raia kote Ukraine na kuwaacha zaidi ya milioni 13 kama wakimbizi nje ya nchi au wasio na makaazi ndani ya nchi yao wenyewe.

Lengo lake alilotangaza tarehe 24 Februari 2022 lilikuwa "kuizuia kijeshi na kuwaondoa wanazi na sio kuikalia kimabavu, siku chache baada ya kuunga mkono uhuru wa maeneo ya mashariki mwa Ukraine yanayokaliwa na vikosi vya maajenti wa Urusi tangu 2014.

Aliapa kuwalinda watu dhidi ya miaka minane ya uonevu na mauaji ya halaiki ya Ukraine - madai ya propaganda ya Urusi ambayo hayana msingi wowote. Alizungumza juu ya kuzuia Nato kupata nafasi nchini Ukraine, kisha akaongeza lengo lingine la kuhakikisha Ukraine haitaogemea upande wowote.

Rais Putin hakuwahi kusema hivyo kwa sauti kubwa, lakini ajenda kuu ilikuwa ni kuiangusha serikali ya rais mteule wa Ukraine. "Adui ameniteua kama mlengwa namba moja; familia yangu inalengwa namba mbili," alisema Volodymyr Zelensky. Wanajeshi wa Urusi walifanya majaribio mawili ya kuvamia makao ya rais, kulingana na mshauri wake.

Madai ya Urusi ya Wanazi kwamba Wanazi wa Ukraine wamekuwawakisababisha mauaji ya halaiki hatakuingia akilini, lakini shirika la habari la serikali ya Urusi Ria Novosti lilieleza kwamba "kuondolewa kwa Unazi ni lazima mbali na kufuta hali halisi ya sasa ya Ukraine.

Kwa miaka mingi, rais wa Urusi ameikana Ukraine kuwa nchi ya kivyake , akiandika katika insha ndefu ya 2021 kwamba "Warusi na Waukraine walikuwa watu wamoja" kuanzia mwishoni mwa Karne ya 9.

Jinsi rais Putin alivyobadili malengo yake ya kivita

Mwezi mmoja baada ya uvamizi , malengo yake ya kampeni yalipunguzwa kwa kasi baada ya kurudishwa nyuma Kyiv na Chernihiv. Lengo kuu likawa "ukombozi wa Donbas" - kwa upana akimaanisha mikoa miwili ya viwanda ya Ukraine mashariki mwa Luhansk na Donetsk.

Baada ya kulazimishwa kurudi nyuma katika eneo la Kharkiv kaskazini-mashariki na Kherson kusini, malengo ya Urusi bado hayajabadilika, lakini imeonyesha mafanikio kidogo katika kuyafikia.

Mabadiliko hayo kwenye uwanja wa vita yalimsukuma kiongozi wa Urusi kutwaa majimbo manne ya Ukraine Septemba iliyopita, bila ya kuwa na udhibiti kamili wa yoyote kati yao: Sio Luhansk au Donetsk upande wa mashariki, wala Kherson au Zaporizhzhia upande wa kusini.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Malengo ya vita ya Putin

Rais Putin alilazimishwa kutafuta wanajeshi wa ziada kwa mara ya kwanza tangu Vita vya Pili vya Dunia, ingawa usajili huo wa maaskari ulitengengewa askari wa akiba wapatao 300,000.

Vita vya mvutano sasa vinaendelea kwenye mstari wa mbele wa kilomita 850 (maili 530) na ushindi wa Urusi ni mdogo na ni nadra. Kilichokusudiwa kuwa operesheni ya haraka sasa ni vita vya muda mrefu ambavyo viongozi wa Magharibi wamedhamiria Ukraine inapaswa kushinda.

Matarajio yoyote ya Ukraine kutoegemea upande wowote sasa yamepitwa na wakati.

Rais Putin alionya mwezi Disemba kwamba vita "vinaweza kuwa mchakato mrefu", lakini kisha akaongeza baadaye kwamba lengo la Urusi "sio kuzungusha gurudumu la migogoro ya kijeshi", bali kukomesha.

Je amefanikiwa nini?

Mafanikio makubwa zaidi ambayo Rais Putin anaweza kuyadai ni kuanzisha daraja la ardhini kutoka mpaka wa Urusi hadi eneo la Crimea, ambalo lilitwaliwa kinyume na sheria mwaka 2014, hivyo hategemei tena daraja lake kwenye mkondo wa bahari wa Kerch.

Amezungumza juu ya kuliteka eneo hili, ambalo linajumuisha miji ya Mariupol na Melitopol, kama "matokeo muhimu kwa Urusi". Bahari ya Azov, ndani ya mkono wa bahari wa Kerch , "imekuwa bahari ya ndani ya Urusi", alisema, akionyesha kwamba hata Tsar Peter Mkuu wa Kirusi hakuweza kusimamia hilo

.

Chanzo cha picha, BBC and Goctay Kuraltan

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Ukraine bado wanashikilia Bakhmut huku vita vikali vikikendelea

Je ameshindwa?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mbali na kuliteka eneo moja karibu na Crimea , Vita vya Urusi vimekuwa janga kwa taifa hilo na taifa lililoshambuliwa. Kufikia sasam Urusi imepata mafanikio machache Zaidi ya kuonesha ukatili na mapungufu ya jeshi la Urusi.

Huku miji kama vile Mariupol ikiathirika vibaya, maelezo kuhusu uhalifu wa kivita yamejitokeza dhidi ya rai awa Bucha , karibu na mji mkuu wa Kyiv , na yamesababisha kuundwa kwa ripoti huru inayoishutumu Urusi kwa kuchochea mauaji ya kimbari.

Lakini ni kushindwa kwa jeshi lake ambapo kuionesha mapungufu ya Urusi.

Kurudi nyuma kwa wanajeshi 30,000 wa Urusi waliovuka mto Dnipro kutoka Kherson mnamo Novemba ilikuwa ni dhihiridho la kushindwa kimkakati.

Msafara wa kivita wa kilomita 64 (maili 40) ambao ulisimama karibu na Kyiv mwanzoni mwa vita haukufaulu.

Idadi kubwa ya vifo vya wanajeshi waliohamasishwa hivi majuzi katika shambulio la kombora la mwaka mpya la Ukraine huko Makiivka kulionesha kushindwa kwa ujasusi wa Urusi.

Kuzama kwa meli ya Urusi katika Bahari Nyeusi ya Moskva kulikuwa kushindwa kwa ulinzi, kama vile shambulio la kushangaza mnamo Oktoba 2022 ambalo lilifunga daraja la mkondo wa bahari wa Kerch kwa wiki.

Maonyo ya Urusi kwa nchi za Magharibi dhidi ya kuipatia Ukraine silaha yamepuuzwa, huku kukiwa na hakikisho la uungaji mkono wa nchi za Magharibi "kwa muda mrefu iwezekanavyo".

Silaha za kijeshi za Ukraine ziliimarishwa na makombora ya hali ya juu ya Himars na ahadi ya mizinga ya Leopard 2 ya Ujerumani.

Lakini vita hivi havijaisha. Mapambano ya Donbas yanaendelea. Urusi imeuteka mji wa Soledar mwaka huu na ina matumaini ya kuuteka mji wa mashariki wa Bakhmut kwenye barabara ya kuelekea miji muhimu ya magharibi, na kutwaa tena eneo ililopoteza msimu wa vuli uliopita.

Waangalizi wa Putin wanaamini kuwa atajaribu kupanua udhibiti wa maeneo manne ambayo ametangaza kuwa sehemu ya Urusi, sio tu huko Donbas, lakini kuelekea mji muhimu wa Zaporizhzhia.

Iwapo atahitaji, Rais Putin anaweza kuendeleza usajili wa wanajeshi Zaidi na kuongeza muda wa vita . Urusi ni nchi yenye nguvu za nyuklia na amedokeza kuwa atakuwa tayari, ikibidi, kutumia silaha za nyuklia kuilinda Urusi na kung'ang'ania ardhi ya Ukraine inayokalia kwa mabavu. "Kwa hakika tutafanya matumizi ya mifumo yote ya silaha inayopatikana kwetu. Huu sio upuuzi," alionya.

Kyiv inaamini kuwa Urusi pia inatafuta kuipindua serikali inayounga mkono Umoja wa Ulaya huko Moldova, ambako wanajeshi wa Urusi wako katika eneo lililojitenga la Transnistria linalopakana na Ukraine.

Je, Putin ameathiriwa?

Rais Putin, 70, amejaribu kujitenga na kushindwa kijeshi, lakini mamlaka yake, angalau nje ya Urusi, yamepunguzwa na anafanya safari chache nje ya mipaka yake.

Huku nyumbani, uchumi wa Urusi unaonekana kustahimili msururu wa vikwazo vya Magharibi, ingawa nakisi ya bajeti yake imeongezeka na mapato ya mafuta na gesi yameshuka sana.

Jaribio lolote la kupima umaarufu wake limejaa ugumu.

Upinzani nchini Urusi ni hatari sana, huku hukumu za jela zikitolewa kwa yeyote anayeeneza "habari bandia" kuhusu jeshi la Urusi.

Wale wanaoupinga uongozi wa Urusi ama wamekimbia au, kama ilivyokuwa kwa kiongozi mkuu wa upinzani Alexei Navalny, wametupwa gerezani.

Mabadiliko ya Ukraine kuelekea Magharibi

Mbegu za vita hivi zilipandwa mwaka 2013, pale Moscow ilipomshawishi kiongozi wa Ukraine anayeiunga mkono Urusi kufuta mapatano yaliyopangwa na Umoja wa Ulaya, na kusababisha maandamano ambayo hatimaye yalimuangusha na kupelekea Urusi kuiteka Crimea na kufanya unyakuzi wa ardhi mashariki mwa nchi hiyo. .

Miezi minne baada ya uvamizi wa Urusi 2022, EU ilitoa hadhi ya mgombea wa Ukraine na Kyiv inashinikiza kukubaliwa haraka iwezekanavyo.

Kiongozi wa muda mrefu wa Urusi pia alitamani sana kuizuia Ukraine isiingie kwenye katika shirika la Nato, lakini jaribio lake la kulaumu muungano wa kujihami wa Magharibi kwa vita ni uongo.

Sio tu kwamba Ukraine iliripotiwa kukubaliana kabla ya vita makubaliano ya muda na Urusi ya kujiondoa kutoka kwa Nato, lakini mnamo Machi, Rais Zelensky alijitolea kudumisha Ukraine kama nchi isiyofungamana na upande wowote na isiyo ya nyuklia: "Ni ukweli na lazima utambuliwe. ."

Je, Nato inalaumiwa kwa vita hivyo?

Nchi wanachama wa Nato zimezidi kutuma mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine kulinda miji yake, pamoja na mifumo ya makombora, mizinga na ndege zisizo na rubani ambazo zilisaidia kugeuza wimbi dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Lakini sio lawama kwa vita. Upanuzi wa Nato unakuja kama jibu kwa tishio la Urusi - Uswidi na Ufini ziliomba tu kujiunga kwa sababu ya uvamizi huo.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uswidi na Ufini zilipowasilisha rasmi maombi ya Nato

Kulaumu upanuzi wa Nato kuelekea mashariki ni masimulizi ya Kirusi ambayo yamepata msingi barani Ulaya. Kabla ya vita hivyo, Rais Putin aliitaka Nato kugeuza saa nyuma hadi 1997 na kuondoa vikosi vyake na miundombinu ya kijeshi kutoka Ulaya ya Kati, Ulaya Mashariki na Baltic.

Machoni mwake, nchi za Magharibi ziliahidi mwaka 1990 kwamba Nato ingepanuka "sio inchi moja kuelekea mashariki", lakini ilifanya hivyo hata hivyo. Hiyo ilikuwa kabla ya kuanguka kwa Muungano wa Sovieti, ahadi iliyotolewa kwa Rais wa Soviet Mikhail Gorbachev ilirejelea tu Ujerumani Mashariki katika muktadha wa Ujerumani iliyounganishwa tena.

Bw Gorbachev alisema baadaye kwamba "mada ya upanuzi wa Nato haikujadiliwa kamwe" wakati huo.

Nato inashikilia kuwa haikuwa na nia ya kupeleka wanajeshi wake wa kivita upande wa mashariki hadi Urusi ilipotwaa Crimea kinyume cha sheria mwaka 2014