Teknolojia ya Akili Mnemba (AI), inadumaza ubunifu katika muziki’ - Kimambo, Mtayarishaji wa Muziki

.
Maelezo ya video, Teknolojia ya Akili Mnemba (AI), inadumaza ubunifu katika muziki’ - Kimambo

Teknolojia ya Akili Mnemba (AI) ni teknolojia inayokuwa kwa kasi duniani huku ikianza kukita mizizi katika uzalishaji wa muziki kwa wanamuziki wa nchi za Magharibi.

Kupitia teknolojia ya AI mtu anaweza kuomba atungiwe mashairi kuhusiana na mada husika na kuiamrisha kompyuta kusuka mdundo na kukamilisha wimbo bila Msanii yoyote kuhusika.

Mwandishi wa BBC Frank Mavura amezungumza na John Kimambo, muandaaji wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania anayeona hatari ya teknolojia hii katika ubunifu kwa wazalishaji wa muziki.