Wanasayansi kuzalisha umeme kutoka maelfu ya maili kwenye anga za mbali

ESA

Chanzo cha picha, ESA

Wakuu wa masuala ya anga wanapaswa kuchunguza iwapo inawezekana kupatikana kwa umeme bila kutumia waya kutoka angani hadi kufikia mamilioni ya nyumba.

Shirika la masuala ya Anga la Ulaya wiki hii huenda likaidhinisha utafiti wa miaka mitatu ili kuona kama inawezekana kuweka mitambo ya kuvuna miale ya jua kwenye anga ya juu kwa ajili ya umeme wa jua na kama inaweza kuwa wa gharama nafuu.

Lengo la mwisho ni kuwa na satelaiti kubwa katika obiti, inayoweza kutoa kiwango sawa cha umeme kila moja kama kituo cha nguvu ya kuzalisha umeme huo.

Baraza la ESA litazingatia wazo hilo katika Makao Makuu yake ya Paris siku ya Jumanne.

Wakati mashirika kadhaa na mashirika mengine ya anga yameangalia wazo hilo, kinachojulikana kama mpango wa Solaris ungekuwa wa kwanza kuweka msingi wa mpango wa vitendo wa kuunda mfumo wa uzalishaji wa nishati mbadala unaotegemea anga ya mbali

Mpango huo ni mojawapo ya mapendekezo kadhaa yanayozingatiwa na mawaziri wa utafiti katika mkutano wa Baraza la ESA mjini Paris ambao utaamua bajeti ya awamu inayofuata ya mipango ya wakala wa anga ya juu ya uchunguzi wa anga, ufuatiliaji wa mazingira na mawasiliano.

Josef Aschbacher, ambaye ni mkurugenzi mkuu wa ESA, aliambia BBC kwamba anaamini kuwa nishati ya jua kutoka angani inaweza kuwa na ''msaada mkubwa'' wa kushughulikia uhaba wa nishati katika siku zijazo.

 ''Tunahitaji kubadilika kuwa uchumi usio na kaboni na hivyo basi kubadili njia tunayozalisha nishati na hasa kupunguza sehemu ya nishati ya mafuta katika uzalishaji wetu wa nishati," alisema.

''Kama unaweza kuifanya ukiwa angani, na nasema kama tunaweza, kwa sababu bado hatujafika, hii itakuwa nzuri sana kwa sababu ingetoa suluhisho la matatizo mengi. 

ESA

Chanzo cha picha, ESA

Nishati ya Jua inaweza kukusanywa kwa ufanisi zaidi angani kwa sababu hakuna usiku wala mawingu. Wazo hilo limekuwepo kwa zaidi ya miaka 50, lakini limekuwa gumu sana na ghali sana kutekeleza, hadi labda sasa.

ESA inatafuta fedha kutoka kwa mataifa wanachama wake kwa ajili ya mpango wa utafiti inaouita Solaris, ili kuona kama maendeleo haya yanamaanisha kuwa sasa inawezekana kutengeneza nishati ya jua iliyotenganishwa kwa uhakika na kwa bei nafuu ili kuifanya iwe na faida kiuchumi.

ESA

Chanzo cha picha, ESA

Lengo kuu la mpango wa Solaris ni kubaini kama inawezekana. Kwa kweli hii haiwezi kufanywa kwa kebo ndefu sana, kwa hivyo lazima itumwe bila waya, kwa kutumia mihimili ya microwave.

Timu ya Solaris tayari imeonyesha kuwa inawezekana kimsingi kusambaza umeme bila kutumia waya kwa usalama na kwa ufanisi. Wahandisi walituma 2 KW za nishati kwa umbali wa zaidi ya mita 30 bila waya kama sehemu ya mnamo Septemba na ikafanikiwa.

Itakuwa hatua kubwa kutuma gigawati za nguvu kutoka umbali wa zaidi ya maelfu ya maili, lakini kulingana na Jean Dominique Coste, ambaye ni meneja mkuu wa kitengo cha anga cha Airbus, inaweza kufikiwa lakini kupitia hatua nyingi ndogo ndogo.

ESA

Chanzo cha picha, ESA

Marekani, China na Japan pia zimepiga hatua katika kinyang'anyiro cha kutengeneza nishati ya jua inayotegemea anga za juu na wanatarajiwa kutangaza mipango yao wenyewe hivi karibuni.

Kando na pendekezo la ESA, nchini Uingereza, kampuni, Space Solar, imeundwa. Inalenga kuonyesha nguvu inayong'aa kutoka angani ndani ya miaka sita, na kufanya hivyo kibiashara ndani ya miaka tisa.

ESA

Tathmini ya serikali ya Uingereza, isiyotegemea mpango wa ESA, ilihitimisha kuwa inawezekana kuwa na setilaiti yenye uwezo wa kuzalisha kiwango sawa cha umeme kama kituo cha uzalishaji, karibu 2 GW, kufikia 2040, ambayo inaambatana na makadirio ya ESA yenyewe.

Lakini, kwa mujibu wa Dk Vijendran, kwa ufadhili ulioongezeka na kuungwa mkono zaidi kisiasa inaweza kufanyika ndani ya muongo mmoja, sawa na tarehe ya mwisho iliyowekwa na Rais wa Marekani John Kennedy mwaka 1961 kupeleka mwanaanga wa Marekani mwezini.