Artemis: Nasa iko tayari kuanzisha enzi mpya ya uvumbuzi katika mwezi

Chanzo cha picha, NASA
Shirika la anga za mbali la Marekani linahesabu siku kabla ya kusafirisha hadi mwezini roketi mpya itakayoelekea mwezini – ukiwa ni mfumo wa safari za anga za mbali .
SLS ni gari lenye nguvu zaidi la mwezini kuwahi kutengenezwa na Nasa, na itakuwa msingi NASA wa mradi wa Artemis unaolenga kuwarejesha watu tena katika sakafu ya mwezi baada ya miaka 50 bila mtu yeyote kwenda huko.
Roketi hiyo imepangwa kuondoka kwenye Kituo cha anga za mbali cha Kennedy saa 08:33 kwa saa za eneo (12:33 GMT; 13:33 BST) Jumatatu.
Kazi yake itakuwa ni kusukuma kifaa cha kuchukua vipimo (pad), kinachoitwa Orion, mbali na dunia.
Chombo hiki cha anga za mbali kitauzunguka mwezi kabla ya kurejea duniani kwa kasi kubwa itakayopelekea chombo hicho kupasuka ndani ya Bahari ya Pacific katika kipindi cha wiki sita.
Orion kinasafiri anga za mbali bila mhudunu yeyote ndani yake na watengenezaji wake wanafikiri kuwa iwapo kitaweza kufanya kazi kama kinavyotarajiwa basi wataalamu wa anga za mbali wataweza kupanda ndani yake kwa ajili ya msururu wa safari ngumu zaidi, wanazotarajia kuanza katika mwaka 2024.
"Kila kitu tunachokifanya na chombo hiki cha safari za anga cha Artemis tunaangalia kupitia darubini kuangalia kile kitakapokuwa na wahudumu ndani yake ," alieleza mtaalamu wa anga za mbali katika Nasa Randy Bresnik.

Shirika la angaza mbali la Marekani lina fursa kadhaa katika kipindi cha wiki ijayo za kusafirisha angazi chombo cha SLS-Orion, lakini litatakiwa kuchukua hatua za moja kwa moja.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Hali ya hewa ya Florida hubadilika mara kwa mara katika kipindi hiki cha mwaka, huku kukiwa na droruba kali zinazoambatana na radi zikipita juu ya kituo cha safari za anga za mbal cha Kennedy.
Minara ya mwangaza ya umeme imekuwa ikipigwa mara kadhaa na radi katika siku za hivi karibuni.
Mapema asubuhi ndipo hali ya hewa kwa kawaida huwa imetuliwa zaidi, jambo linalofanya kupaa kwa chombo hicho Jumatatu kuwa bora zaidi.
"Kimsingi, mwanzoni mwa safari, au baada ya saa mbili unusu asubuhi, kunakuwa na uwezekano wa kuwa na 80% ya hali nzuri ya hewa ," alisema mtaalamu wa hali ya hewa Melody Lovin.
Hatahivyo, iwapo matatizo ya kiufundi yatasukuma nyuma muda kuanza kwa safari kwa muda wa saa mbili, uwezekano wa kuwa na hali nzuri ya hewa utashuka na kuwa 60%, kwasababu kutakuwa na uwezekano wa kunyesha kwa mvua. Roketi ya anga za mbali hairuhusiwi kupaa wakati mvua inanyesha.
Watu 200,000 wanatarajiwa kujipanga kwenye fukwe na kwenye barabara ndogo zinazozingira kituo cha Kennedy, kushuhudia tukio hilo la kihistoria. Linatarajiwa kuwa tukio la kuvutia.
Mfumo wa SLS utakuwa unavuta megatani 39.1 (8.8 million pounds) za kifaa chenye muundo wa pad. Uzito huo unakaribia 15% zaidi kuliko roketi za Saturn V ambazo zilitumwa na mtaalamu wa anga za ambali zilizotumwa na Apollo ambazo zilikwenda mwezini katika miaka ya 1960 na 70.
Zikiwekwa kwa njia nyingine, injini za SLS zinaweza kuwezesha utendaji wa sawa na jeti 60 za Concorde supersonic kusafiri.

"Roketi hii itakuwa kubwa, yenye sauti kubwa zaidi na ya kufurahisha kuliko ile ambayo umewahi kuishuhudia kabla," anasema Lorna Kenna, makamu rais wa Kikundi cha safari za anga za mbali kinachofahamika kama Jacobs SpaceOperations Group, ambacho ni mkandarasi mkuu katika kituo cha anga za mbali cha Kennedy.
"Hakuna kitu chochote kinachofanana na kusikiliza sauti yake – sio kuisikia tu, bali pia kuihisi ikipita mbele yako."
Lengo la mkuu wa safari hii limefikia mwisho wake.
Wahandisi wanahofia zaidi kuona kwamba kinga ya joto ya Orion inaweza kukabiliana na hali za hewa za joto kali kitakalokabiliana nazo wakati kitakapoingia tena katika anga la dunia.
Orion kitakuja kwa kasi kubwa- ya kilomita 38,000 kwa saa (24,000mph), au mara 32 ya kasi ya sauti.
"Hata kuimarishwa kwa Kaboni ambayo hulinda vyombo vya anga ilikuwa bora kwa nyuzi joto 3,000 (1,600C)," alisema Mike Hawes, meneja wa mpango wa Orion katika kituo cha utengenezaji wa vyombo vya safari za anga za mbali cha Lockheed Martin.
"Sasa, tunakuja na zaidi ya joto la nyuzijoto 4,000 (2,200C). Tumerejea kutumia kifaa cha Apollo kinachoitwa Avcoat. Kifaa hiki kimejengwa kwa matofali kikiwa na pengo la kujazia, na kupima hilo ni kipaumbele cha juu zaidi."

Chombo hicho kinachopaa kwenda mwezini sio mafanikio makubwa kwa Nasa tu , labi kwa Shirika la anga za mbali la Ulaya (European Space Agency).
Limetoa huduma katika mfumo wa Orion.
Hiki ni kipengele cha nadra kinachosaidia kusukuma chombo katika anga za mbali. Ni msaada wa ndani wa aina yake ambao Ulaya inatumai kuwa utapelekea watu wa mataifa yake kujumuishwa katika safari zijazo za kuelekea mwezini.
Safari za kusafiri kwa kutumia Artemis IX kwa sasa zinapangwa.
Itakapofikiwa hatua hiyo lazima kutakuw ana wakazi na magari yanayosafiri kweney mwezi yatakayokuwa yanatumiwa na wataalamu wa anga za mbali.
Lakini hatimaye, Artemis inaonekana kama imeweza kuwawezesha watu kufika katika sayari ya Mars.
"Ratiba ya hilo ilipangwa na Rais Obama. Alisema kufikia mwaka 2033," alikumbuka Afisa utawala wa Nasa Bill Nelson.
"Kila utawala uliofuata umekuwa ukiunga mkono mpango huo na muda uliopangwakwamba sasa ninafahamishwa kuwa hilo litafanikiwa katika miaka ya mwisho ya 2030, labda 2040."

Chanzo cha picha, ©2022 MAXAR TECHNOLOGIES















