Marekani kumpeleka mwanamke wa kwanza mwezini kufikia 2024

Chanzo cha picha, NASA
Shirika la Marekani la anga za juu (Nasa) limetangaza rasmi mpango wake wa kurejea tena mwezini utakaogharimu dola bilioni 28b ifikapo mwaka 2024.
Kama sehemu ya mpango unaojulikana kama Artemis, Nasa itawapeleka mwanaume na mwanamke mwezini kwa mara ya kwanza tangu binadamu kufika huko mwaka 1972.
Lakini mpango huo utategemea na iwapo bunge la Marekani litaidhinisha jumla ya dola bilioni 3.2 za kununua vifaa vitakavyotumiwa katika safari hiyo.
Wanaanga watasafiri kwenye chombo kilicho na muundo wa maalum kinachofahamika kama Orion na ambacho kitarushwa angani kupitia roketi itakayotumia mfumo unayojulikana kama SLS.
Akizungumza mnamo mwezi Septemba tarehe 21, msimamizi wa Nasa Jim Bridenstine alisema: "Dola bilioni 28 zitatumiwa kugharamia shughuli zitakazohusiana na safari hiyo katika kipindi cha miaka minne kufadhili mpango wa Artemis kwenda mwezini.
Ufadhili wa SLS, ufadhili wa Orion, binadamu watakaotumia chombo hicho kwenda mwezini - vyote hivyo ni vitu vitakavyokuwa vimejumuishwa kwenye mpango wa Artemis ."
Lakini alifafanua kuwa: "Bajeti iliyowasilishwa mbele ya mikutano yote miwili ya bunge kwa sasa inajumuisha dola bilioni 3.2 ya mwaka 2021 itagharamia mfumo utakawapeleka binadamu mwezini.
Ni muhimu sana tupate fedha hizo, dola bilioni hizo 3.2."

Chanzo cha picha, Lockheed Martin
Bunge la Wawakilishi nchini Marekani limepitisha mswada wa kupatia shirika hilo dola milioni 600 kwenda mwezini.
Lakini Nasa inahitaji fedha zaidi kutengeza chombo kamili kitakachotumika kwa safari hiyo.
Bw. Bridenstine aliongeza kusema: "Kwamba tunalishukuru sana bunge kwa hatua hiyo, lakini tumetathmini bajeti yetu tukaonelea umuhimu wa kufadhili mfumo utakaotumiwa na binadamu - na hizo dola milioni 600 zitatumika katika mchakato huo. Pia ni keeling tunaomba kupewa dola bilioni 3.2 kwa jumla."
Mwezi Julai mwaka 2019 Bw. Bridenstine aliambia kite cha habari cha CNN kwamba mwanamke wa kwanza atazuru mwezini mwaka 2024 na atakuwa "mtu atakayethibitishwa, mtu aliyesafiri, mtu ambaye tayari atakuwa amefika katika kituo cha kimataifa cha angani".
Pia alisema atakuwa mtu ambaye tayari ni mtaalamu wa anga za mbali.

Chanzo cha picha, NASA
Alipoulizwa kuhusu ni lini watawachagua wanaanga watakaoendesha Artemis, Mkuu wa Nasa alisema anatumai uamuzi huo utafikiwa angalau miaka miwili kabla ya kufanyika kwa safari ya kwanza.
Hatahivyo, alisema: "Nathan ni muhimu tuanze kwa kubaini mapema timu ya Artemis… kwasababu itawapa msukumo watakaohusika."
Kwa kuwapeleka tena wanaanga mwezini, Ikulu ya White House inataka Marekani iongoze upya utaalamu wake katika masuala ya sayansi ya manga za juu.
Pia kuna mipango ya mipango pia ya kutoa amana yenye thamani ya barafu ya maji kutoka kwa ncha ya Kusini. Vitu hivyo vinaweza kutumiwa kutengeza mafuta ya rocket mwezini - kwa gharama ya chini ya kubeba kutoka duniani - kutumika kama msingi wa uchumi mwezini.
Lakini Makamu wa Rais Mike Pence pia ameelezea hofu yake kuhusu azma ya China kujiandaa kwenda mwezini. Mwezi Januari 2019, nchi hiyo ya mashariki mwa bara Asia ilikuwa ya kwanza kusafirisha roboti karibu na mwezi. Nchi hiyo sasa inajiandaa kuwasilisha sampuli ya vitu walivyopata mwezini katika maabara ya Ardhini.
Imekuwa ikitengeneza chombo cha angani cha kizazi kijacho cha wanaanga wa China ambacho huenda kikafika umbali wa mwezini.
Japo China haiko katika mpango wa kufika huko mwaka 2024, huenda ikapiga hatua kubwa kufikia lengo hilo mongo huu.
Hati mpya ya Nasa inaelezea awamu ya kwanza ya mango wa Marekani, unaojumuisha kusafirisha chombo hadi mwezini bila kuwepo kwa binadamu- unaofahamika kama Artemis-1 - msimu wa vuli wa mwaka 2021.

Chanzo cha picha, NASA
Mkuu wa Nasa wa chombo cha angani kitakachotumiwa na binadamu katika safari hiyo Kathy Lueders amesema kuwa Artemis-1 itafanyiwa majaribio kwa mwezi mmoja kwa kutumia mifumo yote muhimu.
Alisema chombo cha mwigo kitapunguza hatari ya Artemis-2 kuanguka, majaribio ambayo yatarejelewa katika na wanaanga kabla ya safari ya kwenda mwezini.
Ujuzi mpya imeongezewa safari hii - ikiwa ni pamoja na ukaribu wa mtambo wa kuendesha chombo hicho.
Muda mfupi baada chambo cha Orion kutengana na scheme ya juu ya roketi ya SLS- inayofahamika kama kituo cha mpito kinachoandaa chombo kuanza awamu nyingine ya safari - wanaanga wataendesha wenyewe chombo na kuondoka katika kituo hicho.
Hatua hiyo itatathmini ubora wa chombo cha Orion, utendakazi wake katika mtambo wa kompyuta utakaoielekeza mwezini.
Artemis-3 itakuwa maradi wa kwanza kuwapeleka wataalamu wa anga za juu hadi mwezini tangu kufanyika kwa safari nyingine kama hiyo-Apollo 17, karibu miaka 48 iliyopita.
Nasa imetoa dola millioni 967 kwa makampuni kadhaa kufanyia kazi muundo wa chombo kitakachotumiwa kuwapeleka katika safari hiyo.
Baada ya mwongo mmoja, mpango wa Nasa kutambua kituo cha kambi ya Artemis, utajumuishwa katika miundo mbinu utakaotumiwa kwa mudu mrefu kenda mwezini.
Ikilinganishwa na Artemis, mpango wa Apollo wa mwaka 1960 na 70 iligharimu karibu dola bilioni 250 mfumko wa bei ukijumuishwa kwa kuzingatia thamani ya dola ya Marekani
Hata hivyo, dola bilioni 28 zitakazotumiwa katika mpango huu mpya hazijumuishi fedha ambazo tayari zimetumika kuunda kifaa cha Orion na roketi yenye mfumo wa kutua mwezini.












