Fahamu ni kwanini Marekani, Urusi na India zinashauku kubwa ya kwenda mwezini

అమెరికా, భారత్, రష్యా సహా అనేక దేశాలు లూనార్ స్పేస్ రేస్‌లో భాగం కానున్నాయి

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Nchi nyingi, ikiwemo Marekani, India na Urusi, zitashiriki katika mbio za anga za mbali za kuelekea mwezini

Hakuna chombo hata kimoja cha safari za anga za mbali kilichotua mwezini mwaka uliopita. Lakini, tunaendelea kusikia habari kuhusu mwezi. Nchi nyingi na makampuni yanajiandaa kwa kupatwa kwa mwezi mwaka huu.

NASA itazindua mpango wake wa Artemis mwaka huu kama sehemu ya hili, mwanaanga wa kike atatua kwenye mwezi kwa mara ya kwanza. Aidha, mipango iko mbioni kutuma zana muhimu za kufanya utafiti wa muda mrefu juu ya mwezi. Hizi zitatumiwa na wanaanga wa siku zijazo.

Kufuatia hilo kambi ya Artemis itajengwa ili kuweka wanaanga mwezini. Kituo cha anga pia kinatayarishwa ambacho wanaanga wanaokwenda kwenye mwezi wanaweza kusimama.

Nyumba ya kisasa ya itaundwa hapa ambapo uchunguzi ambao haujawahi kufanywa wa mwezi unaweza kufanywa kutoka hapo. Pia itatusaidia kutua kwenye sayari ya Mars siku zijazo.

Ni nchi gani zinafanya mipango ya programu hii?

India, Japan, Urusi, Korea Kusini na Umoja wa Falme za Kiarabu(UAE) pia zitazindua safari zao za kwenda mwezi mwaka huu.

Kando na haya, nchi zingine na kampuni za kibinafsi pia zitapeleka vyombo vyao kwenye mzunguko wa dunia mwaka huu.

Nyingi ya hizi ni safari zisizo na rubani. Roketi hizo hubeba vifaa vinavyohitajika ili kuishi mwezini. Kwa hivyo nafasi ipo kwa wanadamu kuweka vituo kwenye mwezi kwa muongo mmoja.

Hili sio lengo kuu la programu hizi lakini hii ni hatua ya kwanza katika mpango wa kutua kwenye sayari ya Mars.

Aina mpya ya mashindano ya programau za safari za anga za mbali zinatarajiwa kuanza mwaka huu, huku nchi nyingi zaidi zikitarajiwa kushiriki, alisema Dkt Joy Linhart, mtaalamu wa anga katika Chuo Kikuu cha Bristol nchini Uingereza.

Orion ship

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Orion ship

NASA 'Artemis-One', 'Capstone

NASA imefanya mradi huu kabambe kwa lengo la kuwatuma wanadamu kwenye mwezi ifikapo 2025. Hata hivyo, huo sio mwisho wake, ikiwa itafanikiwa, itakuwa hatua ya kwanza kuelekea lengo kubwa zaidi.

Chombo cha 'Moonikin' kitatumwa kwa mwezi kama sehemu ya program ya 'Artemis-One'. Kupitia hii vazi la kutumiwa kwa safari hii infanyiwa majaribio ambalo litavaliwa na wanaanga watakaokwenda mwezini kama sehemu ya programu hii.

Safari hiyo itazinduliwa na mfumo wa NASA wenye nguvu zaidi wa kurusha roketi (SLS). Itabeba chombo cha Orion hadi mwezini.

Chombo cha kwanza cha angani cha Capstone kitarushwa ifikapo Machi 2022 kama sehemu ya programu ya Artemis.

India hapo awali ilituma chombo cha Chandrayaan kwenye ardhi ya mwezi lakini program hii ilifeli. Shirika la Utafiti wa Anga la India (ISRO) linapanga kuzindua programu kwa jina Chandrayaan-3 mwezini tena mwaka huu.

Programu ya Chandrayaan-3, ikiwa ni pamoja na chombo cha anga, rover na lander, inatarajiwa kurushwa kwenda mwezini baadaye mwaka huu.

Darubini
Maelezo ya picha, Darubini ya anga za mbali -Web telescope

Mpango wa kutua kwenye sayari ya Mars

Taarifa zilizokusanywa na programu ya Artemi zitatumika kujenga kituo anga za mbali. NASA ilieleza kuwa kitakuwa kituo cha nje kinachojengwa karibu na mwezi.

Ikiwa yote yataenda kulingana na mpango, NASA itatuma wanadamu kwenye mwezi kupitia programu ya Artemis-3 ifikapo 2025.

Kurudi mwezini ni sawa na hatua kubwa katika utafiti wa angani, anasema Dk. Hannah Sergeant, mwanasayansi wa sayari katika Chuo Kikuu cha Central Florida nchini Marekani.

"Kituo hicho cha NASA kitakuwa na jukumu muhimu katika uchunguzi wa anga za mbali. Kitasaidia kuweka kituo cha anga za juu karibu na mwezi, na kuweka njia ya kutua kwa siku zijazo kwenye sayari ya Mars," alisema.

Sio tu NASA, lakini nchi nyingi na kampuni kama India, Japan, Falme za Kiarabu zinaangazia mwezi mwaka huu. Baadhi ya programu hizi ni za utafiti, wakati zingine zikisaidia kusafirisha vifaa vinavyohitajika kwenye mwezi.

chombo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chombo cha anga za mbali kikilikaribia jua

Chombo cha India cha Chandrayaan

Rova imepangwa kutua upande wa giza wa mwezi kupitia Chandrayaan-3. Ni sehemu ambayo haijaangaziwa na mwanga wa jua kwa mabilioni ya miaka. Watafiti pia wanasema kwamba paka wanahitaji kujumuishwa katika hatua zozote za tahadhari dhidi ya virusi.

Mipango ya Japan

Mwaka huu, Japan inazindua programu mbili zinazohusiana na mwezi.

Shirika la Anga za Juu la Japan (JAXA) linajiandaa kuzindua chombo cha kwenda mwezini mwezi Aprili mwaka huu. Chombo hicho kwa jina 'Smart Lander for Investigating the Moon' (Slim), kitafanya majaribio ya teknolojia ya kutua mwezini. Kitakusanya taarifa kuhusu kreta kwenye mwezi kupitia mfumo wa utambuzi wa uso. Pia ina darubini ya anga ya juu iitwayo X-ray Imaging and Spectroscopy Mission (XRISM).

Kampuni ya Icepace ya Japan pia inajiandaa kuzindua chombo kiingine hadi mwezini baadaye mwaka huu na nyingine mwaka ujao. Chini ya programu ya 'Hakuto-R', programu hizi mbili zilipewa jina la 'Mission-I' na 'Mission-II'. Hizi ni programu zilizoundwa mahsusi kwa mwezi ambazo zitatuliwa kuchunguza uwezekano wa kuanzisha kituo kwenye mwezi.

Kampuni hiyo ilisema inaweza kuchunguza fursa za biashara huko ikiwa inaweza kujenga vituo mwezini katika siku zijazo. Baada ya program hizi mbili, itajenga mfumo wa usafirishaji mizigo kwenda mwezini kuanzia misheni ya tatu hadi ya tisa, na kisha kujenga viwanda huko.

లూనా 25

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chombo cha Luna 25

Programu za anga za mbali za Urusi na Korea Kusini

Urusi inapanga kuzindua programu yake ya Luna-25 na ile ya Korea Kusini ya Lunar Orbiter.

Shirika la safari za anga za mbali la Urusi Roscosmos limetangaza kuwa maandalizi yanaendelea kupeleka ndege aina ya Luna-25 mwezini Julai mwaka huu.

Kufuatia hili, Urusi inafanya kazi katika mipango ya kuzindua Luna-26 mnamo 2024, Luna-27 mnamo 2025, Luna-28 mnamo 2027 na 2028.

Shirika la anga za mbali la Korea Kusini 'Korea Aerospace Research Institute' litazindua 'Korea Pathfinder Lunar Orbiter' (KPLO) kwenda mwezini Agosti mwaka huu. Itakusanya habari kuhusu hali ya hewa kwenye mwezi na kusaida katika programu ya siku zijazo kwenda kwa mwezi.

Roboti za Biashara za NASA

Kando na serikali za nchi tofauti, kampuni nyingi za kibinafsi pia zinashindana kwenda mwezini.

Kampuni ya Japan iSpace ilijiunga na mbio hizo. Kampuni nyingi zinajitayarisha kushindana kutuma vifaa mwezini chini ya Huduma za NASA

Intuition Missions, iliyoko Houston, Marekani, inajiandaa kurusha vitu hadi mwezini mapema mwaka wa 2022 na roboti yenye miguu sita inayoitwa 'NOVI-C'.

Kampuni ya teknolojia ya Astrobatic yenye makao yake Pennsylvania inatarajiwa kuzindua programu mwaka huu ambapo chombo cha miguu-minne kitafanya utafiti wa kisayansi kwenye ardhi ya mwezi.

Mwezini

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, China ilivumbua nyumba ya ajabu kwenye mwezi...nyumba hii ni ya nani?na nikwanini iko pale ?

Unaweza pia kusoma:

Je, malengo ya programu hizi ni yapi?

Orion ship

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Orion ship

Dk Sajenti alieleza kuwa lengo lao kuu lilikuwa kukusanya taarifa kuhusu hali ya hewa kwenye mwezi. Ili kwamba katika siku zijazo wanadamu wataweza kuweka kutua kwenye mwezi na kujenga mfumo ambao unaweza kulinda dhidi ya upepo na vumbi ya mwezi. Pia, uwezekano wa kujenga rasilimali za maji kwenye mwezi unaweza kuchunguzwa.

చంద్రయాన్ -2

Chanzo cha picha, iSRO

"Lengo ni kufanya mipango yote muhimu kwa wanadamu kutua kwenye mwezi. Taarifa zitakazokusanywa zitatumika kupanga safari kwenda Mirihi. Inaweza kutuchukua angalau miezi sita kufika Mars," Dk. Sajenti alieleza.