Fahamu kitakachotokea kwa mwili wako iwapo utakufa katika anga za juu

Chanzo cha picha, Getty Images
Safari za kujiburudisha anga za mbali ni jambo linalowezekana na siku zinakuja ambapo tutasafiri kwenda sayari zingine kwa likizo au kuishi.
Kampuni ya biashara ya safari za anga za mbali Blue Origin tayari imeanza kupeleea wateja anga za mbali, huku Elon Musk akiwa na matumaini ya kujenga kituo katika sayari ya Mars kwa kutumia kampuni yake ya SpaceX.
Hii inamaanisha kuwa tunahitaji kuanza kufikiria kuhusu itakuwa vipi kuishi anga za mbali na pia ni kipi kitatokeaiwapo mtu atafia huko.
Mtu anapofariki hapa duniani mwili wake hupitia awamu kadhaa za kuoza.
Kwanza damu inaacha kuzunguka na inaanza kukusanyika kwenye viungo vya chini katika kile kinachofahamika kama livor mortis.
Mwili hupata baridi na misuli huwa migumu kwa sababu ya mrundikano wa kile kinaitwa calcium kwenye misuli. Hii hali inafahamika kama rigor mortis.
Kisha vimeng'enya, aina fulani ya protini huchochea mabadiliko ya kemikali na kusababisha seli kupasuka.
Wakati huo bakteria kweney matumbo yetu huvuja na kusambaa kwenda mwili wote. Kisha zinakula nyama nyororo na gesi zinazotoka husababisha mwili kufura.
Rigor mortis hupita huku misuli ikiharibiwa, harufu kali mbaya hutoka, na nyama nyororo uharibiwa.
Kuoza kwa njia tofauti.

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini kifo nje ya mipaka yetu kitakuwa vipi?
Mvuto au gravity kwenye sayari zingine unaweza kuathiri livor mortis. Kutokuwep kwa mvuto anaga za mbali waweza kuzuia damu kukusanyika kwenye viungo vya chini.
Kwenye mavazi yanayovaliwa wakati wa safari za anga za mbali rigor mortis yaweza pia kutokea.
Bakteria wa matumbo wanaweza kula nyama nyororo lakini bakteri hizi zinahita oksijeni kuweza kufanya kazi kisawa sawa na hivyo ukosefu wake unawea kuchelewesha mchakato huo.
Vijidudu udongoni husababisha kuoza kwa hivyo ikiwa mazingira sio salama kwa vijidudu kama vile ukame mkali, yaweza kusababisha nyama nyororo kubaki.
Aina nyingine ya mifupa
Kuoza katika mazingira tofauti na ya dunia yaweza kusabaisha mazingia ya nje kushawishi muonekano kwa vitu kama mifupa kuwa tofauti.
Wakati tuko hai mifupa pia huwa na uhai iliyo na vitu kama mishiba ya damu, collagen na pia Crystalline.
Kwa kawaida vitu hizi huoza kwa hivyo mifupa tunayoiona kwenye makavazi huwa ni mabaki ya isokaboni.

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini kwenye mchanga wenye asidi, ambao tunaweza kupata kwenye sayari zingine, inaweza kuwa ni kinyume na mabaki ya yasio kaboni yanaweza kutoweka yakaacha nyuma nyama nyororo.
Sababu za mazingira
Mazingira katika sayari zingine hayajabadilika kuweza kutupa mili yetu kwa njia inayohitajika. Wadudu na wanyama wanyanganyi hawapatikani huko.
Lakini hali kama ya jangwa hivi iliyo sayari ya Mars inaweza kusababisha nyama nyororo kukauka na labda vitu vinavyopeperushwa na upepo vinaweza kuharibu mifupa kwa njia sawa na ile tunayoiona hapa duniani.
Joto pia ni sababu kuu ya kuoza
Huko mwezini kwa mfano joto inaweza kuwa kati ya nyusi joto 120C na 170C. Huko miili inaweza kuonyesha dalili za mabadiliko yanayosababishwa na joto na baridi kali.
Lakini nafikiri mabaki bado yataonekana kama binadamu kwa sababu kuozoa kabisa sawa na kunakotokea dunani hakutakuwepo.













