SpaceX:Wataalii wa anga za juu wavunja rekodi ya kukaa muda wa siku tatu

Chanzo cha picha, Inspiration4
Wanaanga wanne wamefanikiwa kutua salama kwenye bahari ya Atlantic baada ya kuwa kwenye anga za juu kwa takribani siku tatu.
Ikiwa ni kampuni ya kwanza binafsi, ikiwa na wananchi walioweza kuvuka nje ya Obiti ya Dunia.
Inspiration4 walitumia roketi ya SpaceX huko Florida siku ya Jumatano na na kutua kwenye ardhi ya Dunia saa 19:00 (23:00 GMT) siku ya Jumamosi.

Parachuti nne zilitua kwenye maji na boti za SpaceX ziliwafata mapema kuwaokoa.
Timu ya Insipiration4 ikiongozwa na bilionea Jared Isaacman, 38, ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa 'shift4 Payment', ndiye alikuwa kiongozi mkuu kwenye safari hiyo.
Mpaka haijulikani ni kwango gani cha fedha alichokuwa amelipia, licha ya kwamba jarida maarufu la 'Time' liliandika na kusema kuwa gharama zinaangukia dola za kimarekani 200 sawa na Euro milioni 145 kwa mmiliki wa SpaceX Bilionea Elon Musk kwa siti zote nne.
Bwana Isaacman alijumuika na watu wengine watatu asiowafahamu ambao aliwachagua -mwanajiolojia na mwana-anga wa zamani wa Nasa Sian Proctor, mwenye umri wa miaka 51;
daktari msaidizi ambaye alipona saratani ya mifupa akiwa mtoto Hayley Arceneaux, mwenye umri wa miaka 29 pamoja na Mhandisi wa data za anga na mkongwe wa Jeshi la anga Chris Sembroski, 42.
"Hii ilikuwa safari ya kushaajabisha kwetu ," bwana Isaacman alitangaza kwenye redio muda mfupi baada ya kutua. "Ndio kwanza tumeanza."
Safari hii imekuwa ya tatu kwa kampuni ya Elon Musk, kuwapeleka binadamu katika anga na kuwarudisha salama - na hatua nyingine katika soko la utalii wa anga.
"Hongereni @Inspiration4x !!!" aliandika katika kurasa yake ya tweeter mara baada ya wasafiri kutua salama.

Chanzo cha picha, Reuters
Mifumo ya kitehama katika safari hiyo ilikuwa inaongozwa na SpaceX mpaka walipotua.
Haikuruhusiwa kukikaribia kituo cha kimataifa cha Anga (ISS), Ila walipewa idhini ya kufika urefu wa 575km sawa na maili 360.
Kundi hilo lililosafiri lilipatiwa mafunzo ya miezi sita hasa kuhusu anga za juu na nje ya Dunia, wataalamu waliwapima viwango vyao vya oksijeni kwenye mfumo wa damu, usingizi pia masuala muhimu hasa mambo ya kuzingatia wakiwa safarini.
Safari hiyo imewezesha kuchangia kituo cha utafiti cha Hospitali ya Mtakatifu Jude huko Tennessee ambapo awali akiwa mdogo mmoja wa aliyekuwepo kwenye safari hiyo Hayley Arceneaux aliwahi kutibiwa hapo akiwa mtoto mdogo. Bilionea Musk, ameonesha nia yake ya kufanya biashara za anga zaidi licha ya kwamba wafanyabiashara wengine wakubwa walionesha kuvutiwa zaidi na biashara hiyo kama mabilionea Sir Richard Branson na Jeff Bezos, ambao wote walikwenda juu ya anga ya Dunia mwaka huu kwa kutumia roketi zao binafsi.
"Karibuni katika hatua ya pili ," mkurugenzi wa mpango huo Todd Ericson aliwaambia waandishi wa habari , akisema baada ya safari hii, "Safari za anga zitakuepo ."














