Nasa yachagua kampuni ya SpaceX kutengeneza chombo cha kwenda kwenye mwezi

Human Landing System

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Mfumo wa chombo cha kwenda mwezi

Nasa imechagua kampuni ya Elon Musk ya SpaceX kutengeneza chombo kitakachomrejesha binadamu kwenye mwezi mwongo huu.

Chombo hicho kitambeba mwanadamu atakayefuata na mwanamke wa kwanza hadi kwenda kwenye mwezi kupitia mpango wa 'Artemis' wa shirika la Space.

Lengo jingine la mpango huo litakuwa kupeleka mtu wa kwanza mweusi mwezini.

Chombo hicho kipo katika roketi iliyoundwa na kampuni ya SpaceX ambacho kinafanyiwa majaribio kusini mwa Texas.

Kampuni ya SpaceX ilikuwa ikishindana dhidi ya muungano wa mashirika makubwa ya ndege pamoja na mwanzilishi wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos, pamoja na kampuni ya Dynetics iliyopo Alabama.

Thamani ya kandarasi hiyo kwa ujumla uliyopewa kampuni ya Musk n idola bilioni 2.89.

"Kwa ushindi huu, Nasa pamoja na washirika wetu tutakamilisha safari ya kwanza yenye watu kwenda kwenye mwezi karne ya 21 wakati ambapo kampuni hii inachukua hatua zaidi katika kuhakikisha usawa wa kijinsia na malengo ya muda mrefu ya kufuatilia anga la mbali," amesema Kathy Lueders, mkuu wa shirika la ufuatiliaji shughuli za binadamu anga la mbali.

"Hatua hii muhimu inamuweka mwanadamu katika uwezo endelevu wa kufuatilia shughuli za mwezini na kuangazia hata zaidi safari za mfumo wa jua ikiwemo sayari ya Mihiri yaani 'Mars'."

Astronaut on Moon

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Nasa inataka kuerejea mwezini mwongo huu, lakini mara hii inataka kupiga kambi huko

Mpango huo wa Artemis ambao ulianzishwa chini ya utawala wa Trump ulikuwa umelenga kurejea mwezini mwaka 2024. Lakini ukosefu wa pesa kuufadhili ukafanya iwe vigumu kufikiwa kwa lengo hilo.

Elon Musk amekuwa akitengeneza chombo hicho kwa miaka kadhaa. Chombo hicho kinachofanana na roketi ya enzi ya ufanisi wa kisayansi, ni muhimu katika malengo marefu ya mjasiriamali ya kupeleka watu kwenye sayari ya Mihiri.

Kwa sasa, ingawa, kitatoa huduma kama chombo cha kwenda kwenye mwezi kinachopeleka wanaanga kutoka kwenye mzunguko wa mwezi.

Kukiwa na vyumba vya kuvutia na vizuizi viwili vya hewa wanaanga watakuwa wanaweza kuondoka kwenye chombo hicho kwenda kutembea mwezini, umbali mrefu kuliko walikokwenda wanaume 12 chini ya mpango wa Apollo wa Marekani kati ya mwaka 1969 na 1972.

Miaka ya hivi karibuni, Nasa imechagua zaidi ya kampuni moja inapotaka huduma za usafiri na hilo linawapa machaguo mengi ikiwa moja wapo itashindwa.

Bill Nelson in 2018

Chanzo cha picha, JEFF MITCHELL

Maelezo ya picha, Bill Nelson - aliyeteuliwa na Rais Biden kuongoza shirika la Nasa - anajiandaa kufika mbele ya kamati ya bunge wiki ijayo

Lakini Nasa imepokea dola milioni 850 pekee kati ya dola bilioni 3.3 iliyoomba kutoka kwa bunge kutengneza chombo cha kwenda kwenye mwezi.

Katika taarifa, Bi. Lueders alisema kwamba "wakati inasalia kuwa lengo la shirika hilo kuendeleza mazingira ya ushindani katika kiwango hiki cha mradi huu", bajeti yake ya sasa inawazuia kuchagua kampuni mbili kama ilivyokuwa ikitarajiwa.

Inaaminika gharama ndio imekuwa kikwazo kikubwa; kampuni ya Space ndio ilikuwa imeweka kiwango cha chini cha pesa kati ya washindani wake watatu ambapo "pengo likiwa kubwa haswa".

Bi. Lueders amesema: "Nilidhamiria kwamba itakuwa kwa maslahi ya shirika kutengeneza chombo cha kwanza kupitia kampuni ya SpaceX."

Uamuzi huo umesababisha mabishano makali bungeni. Nasa inapitia mabadiliko ya madaraka kufuatia kuchaguliwa kwa Rais Joe Biden. Inaendeshwa na utawala wa mpito na Bwana Biden alimteu aliyekuwa seneta na mwanaanga Bill Nelson kuendesha shirika hilo - ambaye atafika katika kikao cha kuthibitishwa kwake wiki ijayo.

Starship

Chanzo cha picha, SpaceX

Maelezo ya picha, Chombo cha Starship kikirejea duniani wakati wa moja ya safari zake za majaribio

Nasa inalenga eneo la mwezi la ncha ya Kusini kwa safari yake ya kwanza ya wanaanga tangu mwaka 1972. Eneo hilo lina barafu nyingi na linaweza kubadilishwa kuwa roketi ya fyueli na kuwa na hewa kusaidia katika ujenzi wa eneo la kutua mwezini siku za usoni.

Lakini kutua katika eneo hili pia ni mtihani kwasababu pembe ya jua inatoa kivuli ambacho kinazuia vifaa kama chombo kutua.

Wahandisi watahitajika kuangalia tatizo hilo wakati wanaimarisha mipango yao ya kutua kwa chombo kwenye mwezi kwa mara ya kwanza.

Pia kuchaguliwa kwa kampuni ya SpaceX inawakilisha hatua nyengine kwa kampuni hiyo ya miaka 19 iliyoanzishwa na Musk, ambayo awali ilikumbana na ukosoaji mkubwa katika mipango yake ya kupunguza gharama ya kutengeneza chombo cha anga za mbali.

Nusra kampuni ya SpaceX ifilisike kwasababu ya ukosefu wa pesa, lakini ikaweza kuendelea na shughuli zake baada ya kupata kandarasi ya bahati kutoka Nasa mwaka 2008.

Lunar Module

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Starship is a far cry from the spindly Lunar Module used for the Apollo-era landings

Na tangu wakati huo imepata mafanikio makubwa na kuanzisha setelaiti za kibiashara pamoja na kupata kandarasi ya kifahari ya kupeleka watu katika kituo cha anga za mbali.

Chombo kilichotengenezwa na kampuni hiyo sasa hivi kinafanyiwa majaribio katika kituo cha Boca Chica, kusini mwa Texas.

Mifano ya chombo hicho visivyobeba watu imezinduliwa kwa kimo cha kilomita 10 na zaidi kabla ya kurejeshwa chini katika jaribio la kutua salama ardhini.

Bob Behnken (L) and Doug Hurley (R)

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Bob Behnken (kushoto) na Doug Hurley (kulia) walikwenda kituo cha anga za mbali mwisho wa Mei

Hatahivyo, majaribio ya mwisho ya vyombo hivyo yaliishia kulipuka ama karibu au kwenye njia baada ya kurejea.

"Kuna nyakati za kufurahisha kwa Nasa hasa na timu ya Artemis," amesema Lisa Watson-Morgan, meneja wa mpango wa mfumo wa kupeleka mwanadamu kwenye mwezi wa kituo cha utafiti wa roketi na vyombo vya anga za mbali cha Marshall huko Huntsville.

"Wakati wa mpango wa Apollo, tulithibitisha kuwa inawezekana kufanya yasiyowezekana: kupeleka binadamu kwenye mwezi. Kwa kuchukua hatua ya ushirikiano na kuimarisha utaalam wa kiufundi na uwezo wa Nasa ambao ulishaimarika, kwa mara nyengine tutarejesha wanaanga wa Marekani tena, na safari hii kuchunguza maeneo mapya kwa kipindi kirefu zaidi."