Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 12.05.2023

Manchester United wanahofia huenda wakakosa kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane msimu huu wa joto, huku Spurs wakidhamiria kumbakisha nahodha huyo wa England mwenye umri wa miaka 29 ingawa hivi karibuni atakuwa amesalia na mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake. (Mirror)

Rais wa La Liga Javier Tebas anasema kuondoka kwa kiungo wa kati wa Uhispania Sergio Busquets kutoka Barcelona ndio "mwanzo wa kuelekea" kwa klabu hiyo ya Uhispania kumsajili tena mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35, ambaye mkataba wake na Paris St-Germain unamalizika. katika majira ya joto. (Cadena COPE - kwa Kihispania)

Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 29, atarejea Chelsea kutoka Inter Milan ambako amekuwa kwa mkopo msimu wa joto na kufanya mazungumzo na mkufunzi mpya wa The Blues Mauricio Pochettino na pia kushiriki katika mazoezi ya kabla ya msimu kabla ya uamuzi kufikiwa kuhusu mustakabali wake. (Mirror)

Pochettino anataka Chelsea ianze upya mazungumzo ya kandarasi na kiungo wa Uingereza Mason Mount, 24, ambaye mkataba wake na The Blues unakamilika mwishoni mwa msimu ujao. (Standard)

Aston Villa wako kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Manuel Ugarte, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay mwenye umri wa miaka 22 akihusishwa pia na Chelsea na Liverpool. (Football transfers)

Wakala wa Ugarte anasema kuna vilabu kadhaa vinavyomtaka mchezaji huyo, ambaye anatarajia kuondoka Sporting Lisbon majira ya joto. (O Jogo - kwa Kireno)

Manchester United wanajiandaa kumnunua mlinda mlango wa Everton na England Jordan Pickford, 29, ikiwa kipa wa Uhispania David de Gea, 32, ataamua kuondoka katika klabu hiyo. (Mirror)

Manchester United wanavutiwa na mlinda lango wa Anderlecht na Uholanzi Bart Verbruggen, 20, baada ya hadhi ya De Gea katika klabu hiyo ya Old Trafford kuwa mashakani. (Manchester Evening News)

Kipa wa Argentina Emiliano Martinez anatarajiwa kuondoka Aston Villa msimu wa joto, huku Chelsea, Manchester United na Tottenham zikimwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Gaston Edul, TyC Sports)

Afisa Mkuu Mtendaji wa Inter Milan Giuseppe Marotta anahisi kocha Simone Inzaghi atasalia katika klabu hiyo na kuongeza kuwa kipa wa Cameroon Andre Onana, 27, ambaye amekuwa akihusishwa na Manchester United, anataka kusalia katika klabu hiyo ya Serie A. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Aston Villa wanataka kumnunua mshumbuliaji wa Real Madrid Marco Asensio, 27, kwa uhamisho wa bure wakati mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania utakapokamilika msimu wa joto. (Athletic- Usajili unahitajika)

Everton wanataka sana kumsajili beki wa Southampton wa Ghana Mohammed Salisu, 24, msimu huu. (Football Insider)

Newcastle United itakabiliwa na ushindani kutoka kwa Paris St-Germain katika azma yake ya kumsajili winga wa Bayer Leverkusen Moussa Diaby, huku klabu hiyo ya Ujerumani ikitaka angalau euro milioni 60 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, 23. (Sport Bild - in German).

Bayern Munich ingependa kuendelea kuwa na mlinzi wao Joao Cancelo aliyeko Manchester City kwa mkopo , huku Arsenal na Barcelona pia wakimnyatia mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 28. (90 Min)

Mlinzi wa Chelsea Muingereza Dujon Sterling, 23, anatarajiwa kuhamia klabu ya Rangers ya Scotland kwa uhamisho wa bure katika wiki chache zijazo. (Standard)

Norwich City wanatazamiwa kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Ashley Barnes wakati mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 na Burnley utakapokamilika msimu wa joto. (Football Insider)