Unaweza kumuita mpenzi wako wa zamani jina la Mende?

Chanzo cha picha, Getty Images
Bustani moja ya kutunza wanyama imekuja na wazo la ubunifu kwa ajili ya Siku ya Wapendanao: Jina la mende jina la mpenzi wako wa zamani ama ex wako kabla ya kulisha wanyama na wadudu walioko kwenye bustani hiyo.
Uchangishaji wa mtandaoni unaofanywa na San Antonio Zoo katika jimbo la Texas nchini Marekani umepata umaarufu sana, huku watu kutoka nchi 30 wakiwasilisha majina ya kuchukiza ya wapenzi wao wa zamani. Tazama video hii









