Nchi 5 bora duniani kwa wageni kuishi ughaibuni

Mexico

Chanzo cha picha, Getty Image

Utafiti mpya juu ya mahali bora pa kuishi na kufanya kazi nje ya nchi umefichua nchi bora zaidi kwa wahamiaji ama wageni kuishi. Kuanzia Malaysia hadi Mexico, wakaazi wanaeleza kinachowafanya wapende kuishi kwenye makazi yao mpya.

Mtandao mkubwa zaidi wa wahamiaji duniani, Internations hivi majuzi uliweka wazi ripoti yake ya kila mwaka ya Expat Insider, ambayo inaorodhesha nchi zinazoongoza kwa kuzingatia vipengele 56 vya maisha ya wahamiaji kulingana na gharama ya maisha, makazi hadi upatikanaji wa mtandao wa kasi.

Zaidi ya wageni 12,000 wanaowakilisha mataifa 171 na wanaoishi katika nchi au maeneo 172 walishiriki, ambayo ilisababisha orodha isiyo na kifani na wakati mwingine ya kushangaza inayozunguka ulimwengu.

Tulizungumza na wakaazi wanaoishi katika baadhi ya nchi zilizo na nafasi za juu ili kuelewa ni mambo gani ya maisha huwasaidia watu kutoka nje ya nchi kujisikia nyumbani na kuwaruhusu kujenga maisha mapya huko.

Matokeo ymeziweka nchi hizi 5 kama nchi 5 bora za wahamiaji ama wageni kuishi na kujisikia nyumbani.

1. Mexico

Mexico

Mexico imeorodheshwa kama nchi namba moja katika utafiti wa mwaka huu. Nchi hii si ngeni katika utambuzi huo, baada ya kuwa tano bora kila mwaka tangu 2014. Nchi hiyo inashika nafasi ya kwanza kwa wageni kuzoa mazingira kwa haraka na kjihisi nyumbani. Kwa hakika, 75% ya wageni ama wahamiaji waliohojiwa walisema ni rahisi kupata marafiki wa ndani hapa, ikilinganishwa na 43% ya sehemu nyingine ulimwenguni.

"Watu hapa wana urafiki zaidi kuwahi kukutana nao," alisema mhamiaji kutoka Uholanzi Aemilius Dost, ambaye ameishi Mexico kwa mwaka mmoja na nusu na anamtandao unaoitwa Road to Unknown. "Ninafurahia sana muingiliano nilionao wakati nikinunua matunda na mboga mboga sokoni. Mtindo wa maisha hapa ni mzuri na rahisi kwa wengi kuukubali."

2. Hispania

Hispania

Chanzo cha picha, Getty Image

Hispania imeorodheshwa katika 10 bora kwa Ubora wa Maisha katika utafiti huu tangu 2014, kutokana na utamaduni wake na maisha ya usiku, fursa za burudani, na hali yake ya hewa ya wastani.

"Ingawa inatofautiana kwa kiasi kikubwa kutoka kusini hadi kaskazini mwa nchi, halijoto kwa ujumla ni nzuri na ya kupendeza," alisema mkazi Patricia Palacios, mwanzilishi mwenza wa España Guide, ambaye ameishi Hispania kwa muongo mmoja uliopita. Anasema hali ya hewa ni mojawapo ya kivutio cha kikubwa cha kuishi hapa.

Gharama ndogo za maisha imeendelea kuwa kivutio kwa wageni hapa ukilinganisha na nchi nyingine za Ulaya. Kwa mujibu wa Palacios, wenyeji huwa na tabia rahisi kuingilika, ya kirafiki na ya kukaribisha, hasa kwa wale wanaojaribu kujifunza lugha.

3. Panama

Panama

Chanzo cha picha, Alamy

Nchi hii ya Amerika ya Kati inashika nafasi ya tatu katika orodha kutokana na kupata alama za juu kwenye urahisi wa mgeni kupata utulivu, urahisi wa kupata marafiki, utamaduni ukaribisho. Upande wa hali ya hewa imeifanya kushika nafasi ya juu, nafasi ya 11 kwa jumla kwamba ni nchi yenye hali ya hewa nzuri na ya kuvutia.

"Panama ina hali ya hewa ya kupendeza kwa mwaka mzima, na mchanganyiko mzuri wa mvua na jua," alisema mgeni Sarah Bajc, mmiliki wa Camaroncito EcoResort & Beach. Nchi hiyo pia iko karibu zaidi kijiografia na Marekani, na hivyo kurahisisha mawasiliano ya simu na kutembelewa na familia na marafiki baada ya miaka yake 10 ya kuishi Asia.

4. Malaysia

Malaysia

Chanzo cha picha, Getty Image

Imeorodheshwa katika namba nne katika forodha ya ujumla, Malaysia ilipaa kwenye Ubora wa Maisha mwaka huu, huku wakazi wakiiweka pia kuwa nchi ya tatu katika upatikanaji wake wa fursa za usafiri. Nchi hii ya Kusini-mashariki mwa Asia pia ina alama nzuri katika urafiki wa ndani na upatikanaji wa fedha binafsi.

5. Bahrain

Bahrain

Chanzo cha picha, Getty Image

Hi ni nchi pekee ya Mashariki ya Kati katika 10 bora. Bahrain ilishika nafasi ya tisa na ilikuwa nchi iliyoboreshwa zaidi kwenye orodha hiyo mwaka 2022 na 2023, ikipanda nafasi 19. Ilipanda zaidi katika upande wa Fedha binafsi, kwani karibu nusu ya wageni waliohojiwa walikadiria wakisema gharama ya maisha ni nzuri zaidi kuliko 2022, na waliripoti kuridhika sana na hali zao za kifedha.