Shinzo Abe: Mfahamu Waziri Mkuu aliyehudumu kwa kipindi kirefu zaidi Japan

Chanzo cha picha, Reuters
Shinzo Abe Waziri mkuu wa Japan aliyehudumu kwa kipindi kirefu alikjulikana kwa sera yake ya kimataifa na mkakati wake wa kiuchumi ambao baadaye ulijulikana kama ‘Abenomics’.
Mzalendo wa kihafidhina kwa maelezo ya wengi, Abe mwenye umri wa miaka 67 aliongoza chama cha Liberal Democratic Party (LDP) kupata ushinda mara mbili.
Muda wake wa kwanza kama waziri mkuu ulikuwa mfupi - kwa zaidi ya mwaka mmoja kuanzia 2006 - na ulikumbwa na utata.
Lakini alirejea kwa kishindo mwaka 2012, na kukaa madarakani hadi 2020 alipojiuzulu kwa sababu za kiafya.
Japan ilikuwa katika mfumuko wa kiuchumi wakati alipoanza kuhudumu kwa awamu ya pili na sera yake ya kiuchumi, iliolenga kurahisisha fedha, kuwa kichocheo cha kifedha na mageuzi ya kimuundo – na kupewa sifa kwa kusaidia ukuajiwa uchumi uliokuwa unayumba kurudi mahala pake.
Pia alisaidia Japan kupona kutokana na tetemeko la ardhi na tsunami huko Tohoku mnamo 2011, ambalo liliua karibu watu 20,000 na kusababisha kuharibika kwa vinu vya nyuklia vya Fukushima.
Alijiuzulu mnamo 2020 baada ya wiki za uvumi, akifichua kwamba alikuwa ameugua ugonjwa wa koliti ya vidonda. Ugonjwa wa matumbo uliosababisha kujiuzulu kwake mnamo 2007.
Alirithiwa na mshirika wake wa karibu wa chama Yoshihide Suga, lakini bado alionekana kama mtu mwenye nguvu katika siasa za Japan.
Kupanda ngazi
Akiwa mtoto wa aliyekuwa waziri wa masuala ya kigeni Shintaro Abe na mjukuu wa aliyekuwa Waziri mkuu Nobusuke Kishi , Abe alitoka akatika familia ya kisiasa.
Lichaguliwa kwa mara ya kwanza katika bunge 1993 na ilipofikia 2005 aliteuliwa kuwa Waziri wakati Waziri mkuu Junichiro Koizumi alipomchangua katina wadhfa muhimu wa Waziri mkuu.
Kupanda kwake kulifikia kilele chake wakati alipoteuliwa kuwa waziri mkuu wa Japan aliye mchanga zaidi mwaka 2006.
Lakini mzusuru wa kashfa – ikiwemo serikali kupoteza rekodimalipo ya pensheni , na hivyobasi kuathiri madai milioni 50 wakati wa utawala wake.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hasara kubwa kwa LDP ilifuatia katika uchaguzi wa baraza la juu Julai 2007, na Septemba mwaka huo alipojiuzulu kutokana na maradhi ya matumbo.
Lakini mwaka wa 2012, Abe alirudi kama waziri mkuu, akisema kwamba alikuwa ameushinda ugonjwa huo kwa msaada wa dawa.
Baadaye alichaguliwa tena mwaka wa 2014 na 2017, na kuwa waziri mkuu aliyekaa muda mrefu zaidi nchini Japani.
Umaarufu wake ulishuka, lakini kwa kiasi kikubwa alibaki bila kupingwa kutokana na ushawishi wake katika LDP, ambacho kilirekebisha sheria zake ili kumruhusu kuhudumu kwa muhula wa tatu kama kiongozi wa chama.
Mzalendo mwenye utata
Abe alijulikana kwa msimamo wake wa kizungu juu ya ulinzi na sera ya kigeni, na kwa muda mrefu amekuwa akitafuta kurekebisha katiba ya Japan ya baada ya vita.
Wahafidhina wanaona katiba hiyo - ambayo iliandikwa na Marekani - kama ukumbusho wa kushindwa kwa aibu kwa wanajeshi wa Japan katika Vita vya Pili vya Dunia.
Maoni yake ya utaifa mara nyingi yameibua mvutano kati ya China na Korea Kusini, haswa baada ya ziara yake ya mwaka 2013 katika hekalu la Yasukuni la Tokyo, eneo lenye utata linalohusishwa na wanamgambo wa Japan kabla na wakati wa vita vya pili vya dunia.
Ziara yake ya mara kwa mara kwenye kaburi hilo pia ilikasirisha vikundi vya mrengo wa kushoto nchini Japan, ambao waliliona kama jaribio la Abe la kusahau yaliofanyiwa Wajapani wakati wa vita.

Chanzo cha picha, EPA
Mwaka 2015, alisukuma haki ya kujilinda kwa pamoja, akiiwezesha Japan kuhamasisha wanajeshi wa ng'ambo kujilinda na washirika wanaoshambuliwa.
Licha ya upinzani kutoka kwa majirani wa Japan na hata umma wa Japani, bunge la Japan liliidhinisha mabadiliko haya yenye utata.
Lengo lake kubwa la kurekebisha katiba ili kulitambua rasmi jeshi la Japan bado halijatimizwa, na linaendelea kuwa mada yenye mgawanyiko nchini humo.
Pia hakuweza kupata kurejeshwa kwa yale ambayo Japan inayataja kama Maeneo ya Kaskazini - msururu wa visiwa vinavyozozaniwa karibu na mkoa wa kaskazini wa Hokkaido ambavyo vinadaiwa na Japan na Urusi.
Uhusiano wa Abe na rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, ulisifiwa kwa kuilinda Japan dhidi ya kulemaza ushuru wa kibiashara unaoongozwa na Marekani, na kulazimika kutafuta pesa zaidi kusaidia uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini humo.
Kukabiliana na uchimi na Uviko
Sera ya bwana Abe ya Abenomics – ilionekana kama ilioisaidia kuimarisha uchumi wake wakati wa awamu yake ya kwanza kama waziri mkuu.
Hii ilijumuisha viwango hasi vya riba vya muda mfupi ambavyo vilifanya iwe nafuu kwa watumiaji na makampuni kukopa pesa na kutumia, kuongeza matumizi ya serikali katika miundombinu na motisha zaidi za kifedha kama vile mapumziko ya kodi, na mageuzi ambayo yalitaka kuongeza wanawake zaidi katika nguvu kazi. Na kuruhusu wahamiaji zaidi ili kupunguza shinikizo la kazi kwa lengo la kuimarisha ukuaji wa kiuchumi.
Lakini juhudi zake zilikabiliwa na changamoto kubwa wakati nchi ilipoingia tena katika mdororo katika majira ya kuchipua ya 2020. Hilo na hali zingine za kushuka kiuchumi ilizua maswali kuhusu ufanisi wa mbinu yake.

Chanzo cha picha, EPA
Umaarufu wa Abe uliguswa zaidi na wasiwasi juu ya kushughulikia kwake janga la Covid-19.
Wakosoaji wanaamini kuwa kampeni zake zilizolenga kukuza utalii wa ndani zilichangia kuibuka tena kwa maambukizo.
Pia wanasema ahadi nyingine za Abenomics - kama vile kuwawezesha wanawake katika nguvu kazi, kukabiliana na upendeleo na kubadilisha tamaduni zisizo za afya za kazi - hazijatekelezwa.
Kimataifa, amesifiwa kwa kushikilia Ushirikiano wa Trans-Pacific - makubaliano makubwa ya kibiashara kati ya nchi 11 - kwa pamoja, kufuatia kujiondoa kwa ghafla kwa Marekani chini ya utawala wa Bw Trump.
Kujiuzulu na kifo
Tangazo la kujiuzulu kwa Abe tarehe 28 Agosti lilisababisha mapambano ya ndani kati ya makundi ya LDP, kwa sababu alikataa kutaja mrithi.
Hatimaye alirithiwa na Yoshihide Suga, mwanasiasa mkongwe na mjumbe wa baraza la mawaziri wa muda mrefu.
Lakini Abe aliendelea kushikilia siasa za ndani nchini Japan, hata baada ya Suga kubadilishwa na waziri mkuu wa sasa Fumio Kishida.
Tarehe 8 Julai, Abe alikuwa katika mji wa kusini wa Nara akifanya kampeni kwa niaba ya mgombeaji wa bunge la juu la Japan.
Alikuwa akitoa hotuba alipopigwa risasi na mtu mwenye bunduki - mwenye umri wa miaka 41 ambaye anaaminika kuwa mwanachama wa zamani wa Kikosi cha Kujilinda, sawa na jeshi la wanamaji la Japan.
Abe alikuwa na fahamu alipopelekwa hospitalini, lakini alifariki baadaye kutokana na majeraha yake.












