Kipi kingetokea iwapo taifa moja lingepunguza mwanga wa jua kupambana na mabadiliko ya tabia nchi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Iwapo mabadiliko ya hali ya hewa yangekuwa makali sana hadi nchi moja ikaamua kuvunja itifaki ya kimataifa ili kulinda watu wake! Hali hiyo imetokea katika Riwaya ya Kim Stanley Robinson ya 2020, "Ministry for the Future," ambapo nchi moja inakumbwa na joto kali na kusababisha maafa ya watu milioni 20. Viongozi wa nchi hiyo wanaamua kuchukua hatua kali ya kufifisha mionzi ya Jua.
Kwa miezi saba, ndege za nchi hiyo zilikuwa zikipuliza moshi mweupe mithili ya mlipuko wa volkano. Anga inakuwa nyeupe, jua linapotea na dunia inapoa. Ni mchanganyiko wa gesi ya dioksidi sulfuri na kemikali nyingine, huenea katika ulimwengu wa Kaskazini na kila mahala.
Hatua hiyo tata inavunja sheria za kimataifa, kama kitabu kinavyosimulia, na ina hatari ya kuvuruga mvua za masika - lakini kwa upande mwingine inapunguza kiwango cha joto duniani kwa "digrii moja, kwa miaka mitatu."
Lakini katika ulimwengu wa kweli, swali la ikiwa teknolojia kama hiyo inaweza kutumiwa kwa usalama, bado ni jambo lisilo na uhakika, huku kukiwa na hatari nyingi na mengi yasiyojuulikana.
Kwa hivyo ikiwa taifa litaamua kufifisha mwanga wa jua; ni matokeo gani ya kimazingira na ya kijiografia yanayoweza kuibuka? Je, kunaweza kuwa na matumizi salama ya teknolojia ya aina hiyo?
End of Unaweza pia kusoma
Kurudisha mionzi katika anga

Chanzo cha picha, Getty Images
Zaidi ya wanasayansi 440 walitia saini barua ya wazi ya kutaka makubaliano ya kutotumia teknolojia ya kuzuia mionzi ya jua kupiga dunia na kuirudisha mionzi hiyo katika anga la juu. Mfano wa jaribio hilo lililofanywa San Francisco huko Mexico mapema mwaka huu. Wanasayansi hao wanasema athari zake hazitabiriki.
Andreas Malm, profesa wa ikolojia ya binadamu katika Chuo Kikuu cha Lund nchini Sweden anakubali kwamba, "kutumia teknolojia hiyo ni kwamba biashara ya uwekezaji katika nishati ya mafuta na miundombinu yake itaendelea - na uzalishaji wa hewa chafu utaongezeka."
Kuhusu mbinu iliyoelezwa katika riwaya, Malm anasema, "kadiri ninavyosoma kitabu hiki, ndivyo ninavyoshawishika kwamba teknolojia hii inaweza kuleta madhara na uharibifu, mimi binafsi siwezi kuiunga mkono wala kuitetea."
Watafiti wengine wanapendekeza kuwa uhandisi wa jua unapaswa kuwa wa dharura ili kupunguza mabadiliko ya hali ya hewa. Nchini Marekani, Chuo cha Kitaifa cha Sayansi, Uhandisi na Tiba mwaka jana kilipendekeza mpango wa kitaifa wa utafiti kuhusu Urekebishaji wa Mionzi ya Jua [SRM].

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Februari mwaka huu, wanasayansi kadhaa walichapisha barua ya wazi , iliyoandaliwa na Sarah Doherty wa Chuo Kikuu cha Washington, wakisema kwamba utafiti zaidi unahitajika. Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa umebainisha " upungufu wa taarifa za kutosha juu ya athari zake. Umoja wa Ulaya umetaka mazungumzo ya kimataifa kuhusu hatari zake.
Miongoni mwa watetezi mashuhuri wa utafiti zaidi ni David Keith, mkuu idara ya mifumo ya hali ya hewa katika Chuo Kikuu cha Chicago. Keith anasisitiza kwamba uhandisi wa nishati utumike kusaidia ulimwengu kudumisha halijoto chini ya 1.5C, kiwango cha kabla ya viwanda.
Keith na wengine pia wanaeleza ongezeko la mabadiliko ya tabia nchi huathiri zaidi watu masikini - hasa wale walio katika ulimwengu wa Kusini. Ni wajibu kuchukua hatua za kupunguza madhara na ni wajibu kufanya utafiti juu ya uhandisi wa jua.
Haiwezekani kwa taifa la Kusini mwa Ulimwengu kutengeneza teknolojia iliyo elezwa katika riwaya, anasema Wake Smith, mtafiti wa hali ya hewa katika Idara ya Mazingira ya Chuo Kikuu cha Yale na mtaalam wa zamani wa sekta ya anga.
Kulingana na Smith, moshi mweupe utahitaji ndege kubwa ambazo kwa sasa hazipo ili zitoe mamilioni ya tani za kemikali angani karibu kilomita 20k (futi 66,000). Nchi pekee ambazo zinaweza kuunda ndege kama hizo, Smith anadai, ni Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi au Uchina, na uwezekano wa Ujerumani au Japan.
Athari za Kimazingira

Chanzo cha picha, Getty Images
Hata ikifika hatua nchi zikiendelea na kumudu jambo hilo, bado kuna hatari zingine nyingi za mazingira ambazo zinaweza kutokea. Utafiti mmoja umebainisha kuna uwezekano wa kupotea kwa barafu katika bahari ya Aktiki wakati wa kiangazi. Utafiti mwingine ukiashiria kupungua kwa kiasi kikubwa mvua ya monsuni.
Miongoni mwa athari zinazoweza kutokea zaidi ni uharibifu wa safu ya ozoni ya angahewa. Ripoti ya UNEP ya 2022 - teknolojia hiyo pia isingefanya chochote kuzuia kuongezeka kwa viwango vya CO2 kutoka katika asidi ya bahari .
Karen Rosenlof, mwanasayansi katika Maabara ya Kitaifa ya Sayansi ya Kemikali huko Marekani, anasema gesi kama sulfati, kaboni na metali, zote zina athari zake.
Mashaka na Matumaini

Chanzo cha picha, Getty Images
Licha ya uwepo wa maswali ya haki na usawa. Shuchi Talati wa The Alliance for Just Deliberation on Solar Geoengineering, shirika la Marekani, linaloeneza ufahamu na "kuhakikisha jumuiya na nchi zilizo katika mazingira magumu ya hali ya hewa - hasa katika ulimwengu wa kusini - zinapata habari, ujuzi na rasilimali kuhusu teknolojia.
Kwa sababu mataifa ya Kusini mwa Ulimwengu yana uwezo mdogo wa kuendeleza teknolojia kwa sababu ya kiwango kidogo cha teknolojia, na tayari yana uwakilishi mdogo katika mashirika ya kimataifa kama Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Kwa Lili Fuhr, mkurugenzi katika Kituo cha Sheria ya Kimataifa ya Mazingira, teknolojia "inahitaji mifumo ya utawala ya kisasa zaidi kuliko kitu chochote ambacho kimewahi kuwepo, mifumo itakayo fanya kazi kwa karne nyingi au milenia. "
Robinson aliiambia BBC kwamba ingawa majanga ya hali ya hewa yanaongezeka, ndivyo pia kasi ya kimataifa ya kuchukua hatua inaongezeka. "Maoni yangu ni kwamba janga hili lilishtua watu. Ulimwengu huu ni muhimu na tabia nchi inaweza kuvuruga ustaarabu wetu."
Robinson anaongeza. "Huenda tukalazimika kujaribu mbinu mbalimbali ili kupoza mambo, wakati uondoaji kaboni unaendelea. Nadharia hizi zipo kuchochea mijadala ili kuutayarisha umma. Na nadhani matumaini yaliyoenea ni kwamba ikiwa tutawahi kufanya mambo kama haya itakuwa kwa njia ya makubaliano ya kimataifa na makubaliano ya jumla."















