Je, mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na mengine yanachangia moto wa nyikani unaosumbua dunia?

Chanzo cha picha, EPA
Hali ya hewa ya joto kali inazidi kushuhudiwa mara kwa mara na inazidi kuwa mbaya zaidi katika maeneo mengi kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Wanasayansi wanasema hali hii itaendelea kukithiri huku wanadamu wakiendelea kuzalisha gesi zinazoongeza joto kwenye sayari.
Katika taarifa hii tunaangazia njia nne za mabadiliko ya hali ya hewa zinazohusishwa na hali mbaya ya hewa.
Mawimbi ya joto kali kwa muda mrefu
Ongezeko dogo la jota hata liwe la wastani huwa na tofauti kubwa.
Hii ni kwa sababu usambazaji mzima wa viwango vya joto vya kila siku hubadilika na kufikia hadi viwango vya juu zaidi, na kufanya siku za joto ziwe z kali zaidi.

Wanasayansi hutumia uigaji wa kompyuta ili kubaini ikiwa matukio ya hali mbaya ya hewa yamechagiwa na ongezeko la joto linalosababishwa na shughuli za wanadamu.
Kwa mfano, wimbi la joto lililovunja rekodi kote Uhispania, Ureno na kaskazini-magharibi mwa Afrika mwezi wa Aprili lilipanda mara 100 zaidi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, kulingana na mtandao wa World Weather Attribution (WWA).
Ni mapema mno kusema kwa uhakika iwapo mawimbi ya joto yanayoendelea kushuhudiwa mwezi Julai 2023 katika sehemu tofauti za Ulaya, kusini-magharibi mwa Marekani na China yamechochewa zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa.
Lakini wataalam wanasema matukio ya aina hii yanawiana na kile kinachotarajiwa katika ulimwengu unaokabiliwa na ongezeko la joto - hasa yanapojumuishwa na mifumo ya hali ya hewa asilia kama vile mifumo ya shinikizo la juu na El Niño.
Nchini Uingereza, halijoto ilifikia 40C kwa mara ya kwanza kwenye rekodi mnamo Julai 2022. Hili lingekuwa "sio uwezekano mkubwa" bila mabadiliko ya hali ya hewa, WWA inasema.
Mawimbi ya joto pia yanazidi kuwa marefu na makali zaidi - ikiwa ni pamoja na nchini Uingereza.
Hii inaweza kutokea kwa njia ya "joto domes" - eneo la shinikizo la juu ambapo hewa ya moto inasukumwa chini na kunaswa mahali, na kusababisha joto kuongezeka juu ya maeneo makubwa.
Nadharia moja inapendekeza halijoto ya juu katika Arctic - ambayo imeongeza joto zaidi ya mara nne zaidi ya wastani wa kimataifa - inasababisha upepo mkali unaoitwa jet stream kupungua na kuongeza uwezekano wa kuba joto.

2. Kiangazi cha muda mrefu
Kadri binadamu anavyofanya shughuliza kilimo ndivyo mahitaji ya maji yanavyozidi kuongezeka.
Katika baadhi ya maeneo ya Afrika Mashariki, ukame unaoendelea umewaweka zaidi ya watu milioni 20 katika hatari ya kukosa chakula. Mabadiliko ya hali ya hewa yafanya ukame huu kuwa zaidi ya mara 100 zaidi, kulingana na WWA.

Chanzo cha picha, Getty Images
3. Kichocheo cha moto wa nyikani
Moto wa nyika huzuka kiasili katika sehemu tofauti duniani. Ni vigumu kubaini ikiwa mabadiliko ya hali ya hewa yamechangia moto wa nyika kwa sababu mambo mengine kama mabadiliko ya matumizi ya ardhi yanaweza kuhusishwa nayo.
Baadhi ya maeneo - kama vile Marekani magharibi - yameshuhudia ongezeko la eneo linaloteketezwa na moto wa nyika, lakini mienendo ya kimataifa ya moto wa nyika ni ngumu.
Lakini, wanasayansi wanasema mabadiliko ya hali ya hewa yanatoa mazingira yanayohitajika kwa moto wa kuzuka kwa urahisi zaidi.
Joto kali na la muda mrefu hukausha unyevu kutoka kwa ardhi na mimea.

Chanzo cha picha, JAVIER TORRES/AFP
Hali hizi za ukame ni kichocheo kama mafuta kwa moto, ambayo inaweza kuenea kwa kasi ya ajabu, hasa kukiwa na upepo mkali.
Alberta nchini Canada mioto ya nyikani "isiyo na kifani", na kulazimisha karibu watu 30,000 kuondoka makwao. Hii inafuatia moto mkali wa nyika nchini Chile na Australia mapema mwaka wa 2023.
Wanasayansi wanatarajia moto wa nyikani kuzuka mara kwa mara na mkali zaidi katika siku zijazo kutokana na athari za pamoja za matumizi ya ardhi na mabadiliko ya hali ya hewa.
4. Mvua kubwa
Kadiri hali ya joto inavyoendelea kushuhudiwa, ndivyo mvuke ardhini unakuwa mkubwa. Mvuke huo ukiwa mwingi unaunda mawingu ambayo huanguka yakiwa mazito.
Hii husababisha matone zaidi na mvua kubwa, wakati mwingine katika muda mfupi na katika eneo dogo.

Mnamo 2022, Pakistan ilipata mvua kupita kiasi miezi ya Julai na Agosti, na kusababisha mafuriko makubwa yaliyoathiri zaidi ya watu milioni 33.
"Inawezekana" mabadiliko ya hali ya hewa yalichangia mvua hiyo, kulingana na WWA, lakini mifumo ya hali ya hewa ya asili huenda pia ilichangia.
Mvua kubwa na mafuriko pia yamekumba maeneo mengine, ikijumuisha Afrika Magharibi kati ya Mei na Oktoba 2022, na New Zealand mnamo Februari 2023.
Wanasayansi hawawezi kusema kwa uhakika kwamba yalisababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, lakini mafuriko yanaendana na mabadiliko wanayotarajia katika ulimwengu unaokumbwa na joto.












