Familia moja iliyoiongoza Gabon kwa miaka 56. Je mapinduzi haya ndio mwisho wake?

f

Chanzo cha picha, AFP

Kwa hakika, kwa watu wengi ambao hawajamfahamu kiongozi mwingine nje ya familia ya Bongo, inazungumzwa kuwa kuna haja ya mabadiliko.

Sasa maafisa wa jeshi nchini Gabon wasema wamechukua mamlaka nchini Gabon na wametoa wito wa "utulivu" walipotangaza kuwa wamechukua madaraka mapema Jumatano asubuhi.

Walisema wameamua "kulinda amani kwa kukomesha utawala uliopo" mara baada ya baraza la uchaguzi kutangaza kuwa Rais Ali Bongo, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 14, ameshinda muhula wa tatu.

Kwenye mitaa ya mji mkuu wa Gabon, Libreville, wakazi wameonekana wakiwapigia makofi wanajeshi mitaani baada ya jeshi kutangaza kuchukua madaraka leo asubuhi.

Mmoja wa wanajeshi hao alisema kwenye chaneli ya televisheni ya Gabon 24: "Tumeamua kulinda amani kwa kukomesha utawala uliopo." Hii, aliongeza, ilikuwa chini ya "utawala usiowajibika, usiotabirika na kusababisha kuzorota kwa uwiano wa kijamii ambao unahatarisha nchi katika machafuko"

w
Maelezo ya picha, Mafisa wa jeshi la Gabon wakitangaza kwenye televisheni kuwa wamechukua mamlaka ya nchi

Ali Bongo alikua rais mwaka wa 2009 kufuatia kifo cha babake, Omar Bongo, ambaye alitawala taifa hilo la Afrika Magharibi kwa zaidi ya miaka 40.

Hatahivyo rais mwenyewe amekuwa akielezea mafanikio hususan katika uhifadhi wa mazingira na udhibiti wa maliasili pamoja na ujenzi wa bandari ya kibiashara ya Owendo kama mambo muhimu katika kipindi chake cha utawala.

Lakini wakosoaji wake wanasema hakuna mengi ambayo amefanya vinginevyo.

Ikiwa na uchumi unaotegemea mafuta, Gabon imeonekana kwa muda mrefu kuwa nchi yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi, lakini imekuwa ikikumbwa na ufisadi uliokithiri.

h

Utawala uliogubikwa na ufisadi

Mnamo 2022, Transparency International iliiorodhesha Gabon nafasi ya 124 kati ya nchi 180 kwenye orodha yake (index) kuhusu maoni ya Ufisadi.

Wananchi walisema wanakumbana na rushwa katika taratibu za msingi kabisa, ikiwemo katika mipango ya kuajiri watu katika nchi yenye uhaba mkubwa wa ajira.

Haki mara nyingi inaweza kupatikana kutoka kwa mahakama kwa ada ndogo pia, wengine walisema.

Familia hiyo ya Bongo imehusika katika mfululizo wa kashfa kubwa zikiwemo za hivi karibuni za Julai 2022, ambapo ndugu watano wa rais walishitakiwa katika uchunguzi wa Ufaransa wa ubadhirifu na utakatishaji fedha wa umma.

Wakati huo huo, theluthi moja ya watu milioni 2.5 wa Gabon wanaishi katika umaskini, na huduma za kimsingi za kijamii pia hazipo licha ya kuwa na pato la juu zaidi la ndani ya taifa (GDP)kwa kila mtu katika bara hilo.

Afya ya rais

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hali imekuwa mbaya zaidi kutokana na kutokuwa na uhakika wa afya ya rais.

Mnamo 2018, Bongo alipatwa na kiharusi wakati wa safari rasmi ya Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia.

Kiharusi hicho kilimzuia rais kuendelea katika wadhifa rasmi kwa miezi kadhaa na kusababisha kukosekana kwa utulivu wa kisiasa, na kilele chake ni jaribio la mapinduzi.

Pia hakuhudhuria hafla zozote za umma kwa miezi 10, na kujitokeza tena mnamo Agosti 2019.

Lakini alijitahidi kuondosha dhana kwamba alikuwa mgonjwa, asiyefaa kuongoza. Wakati wa kutawazwa kwa Mfalme Charles mnamo Mei alirekodiwa kwa kutumia fimbo ili kusonga mbele polepole hadi kwenye kiti chake.

Haraka kwa miezi michache na Bw Bongo anasemekana kuwa chini ya kizuizi cha nyumbani, huku wanajeshi wakitangaza mapinduzi kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka minne.

Bongo, hata hivyo, alibaki madarakani ingawa uwezo wake wa kimwili na kiakili wa kuongoza nchi umeendelewa kutiliwa shaka.

Wakati huo, janga la COVID-19 lilisababisha kushuka kwa uchumi kwa miaka miwili kwani sheria kali ya kutotoka nje ilizingatiwa miezi kadhaa baada ya vizuizi kuondolewa katika nchi zingine.

Kisha kulikuwa na vita nchini Ukraine, ambavyo vilizuka Februari 2022 na kuwa na athari kwa bei ya nishati na chakula, na kusababisha kuchanganyikiwa kwa umma.

Hilo, wachambuzi wa mambo wanadai, ni uthibitisho kwamba muhula wa mwisho wa Bongo haukuwa na tija.

Ali Bongo amekuwa akiongoza nchi kwa miaka 14, na rekodi yake katika mihula miwili ya uongozi sio nzuri sana.

Ndani ya jiji kuu Libreville kuna wilaya mbili ambazo hazina maji. Ni kwa sababu serikali haijawekeza vya kutosha katika miundombinu hii.

Tangu 2009, uhalali wa urais wa Bongo limekuwa suala la mjadala.

Alichaguliwa baada ya ghasia zilizofuata uchaguzi uliogubikwa na madai ya wizi.

Uchaguzi uliofuata pia ulikumbwa na dosari na tuhuma za udanganyifu mkubwa.

Matokeo yalipotangazwa, maandamano ya kupinga matokeo yalitawanywa kwa mabomu ya machozi na kisha milio ya risasi.

Wapinzani wa rais Bongo wanasema kuendelea kwa hali hiyo kunanufaisha chama tawala cha PDG ambacho kimekuwa madarakani kwa zaidi ya nusu karne na hakuna uwezekano wa kuachia madaraka kirahisi.

Hivyo walisema walitarajia uchaguzi mwingine wenye dosari.

w

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Raia wa Gabon wakilishangilia jeshi baada ya mapinduzi

Kutokuwa na uhakika katika uchaguzi uliopita

Wiki sita tu kabla ya uchaguzi, mamlaka iliamua kwamba uchaguzi wa wabunge na urais ungefanywa kwa kutumia karatasi moja ya kura badala ya tofauti kwa kila nafasi.

Katika nchi ambayo kipaumbele ni kumpigia kura rais na ambapo wagombea wa upinzani mara nyingi ni watu huru ambao husimama bila wagombea ubunge, wapiga kura mara nyingi huwa hawawachagui.

Kwa hiyo, uwezekano wa kuwa na wabunge huru ni mdogo sana nchini Gabon.

Ni dhahiri kuwa baadhi ya wananchi walikuwa wamechoshwa na utawala wa familia ya Bongo na kutokana na matukio yanayoendelea sasa nchini humo huenda ukawa ndio mwisho wa utawala wa zaidi ya miongo mitano ya familia hiyo.