Tetesi za soka Ulaya Alhamisi: Rashford akataa ofa za mikataba ya faida ya Saudia Arabia

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, 27, amekataa ofa tatu kutoka kwa vilabu vya Saudi Arabia zenye thamani ya hadi £35m kwa mwaka. (Mirror)
Hata hivyo, United inaweza kumtumia Rashford kuijaribu Napoli katika mpango wa kubadilishana mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 26. (Sun)
Borussia Dortmund na Paris St-Germain zinaonyesha nia mpya ya kumnunua mhitimu wa chuo cha soka cha Manchester United, Rashford. (Teamtalk)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United inaweza kuidhinisha mikataba mitatu ya mkopo mwezi Januari ili kuokoa fedha katika harakati zao za kutaka kumnunua mshambuliaji wa Sweden mwenye umri wa miaka 26 na mshambuliaji wa Sporting Viktor Gyokeres kwa pauni milioni 80. (i Sport)
Beki wa Manchester City na England Kyle Walker, 34, anasakwa na wachezaji watatu wa Saudi Arabia Al-Nassr , Al-Ahli na Al-Ittihad . (Sun)
Aston Villa wako kwenye mazungumzo na Borussia Dortmund kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Uholanzi Donyell Malen, 25, ambaye anathamanishwa na klabu hiyo ya Bundesliga kwa £25m. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool na Manchester City wanafikiria kuwasilisha ombi la Januari kwa Dani Olmo, 26, baada ya Barcelona kushindwa kumsajili kiungo huyo wa kati wa Uhispania. (Sky Sports Germany - in Germany)
Liverpool hawajawasiliana na AC Milan kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 25, licha ya ripoti nchini Italia kudai mkopo wa miezi sita pamoja na kwamba mkataba wa lazima wa kumnunua wa pauni milioni 41.5 unaweza kufanyika. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambulizi wa Ivory Coast Amad Diallo, 22, yuko mbioni kutia saini mkataba mpya na Manchester United . (Express)
Arsenal wanatazamia dili la kumnunua Evan Ferguson wa Brighton , 20, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Fulham na West Ham kumnunua mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland. (Sport)
Mshambulizi wa Athletic Bilbao Nico Williams, 22, pia analengwa na Arsenal na klabu hiyo ya Ligi ya Premia inaweza kuanzisha kipengele cha kutolewa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania kwa pauni milioni 48. (Football Transfer)
Tottenham na Wolves wanavutiwa na beki wa England mwenye umri wa miaka 26 Ben Godfrey baada ya Atalanta kutomtaka . (Rudy Galetti)

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Klabu ya MLS Charlotte FC inakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili fowadi wa Newcastle na Paraguay Miguel Almiron, 30, kwa £16m. (Sun)
Everton haitakaribisha ofa kwa mlinzi Jake O'Brien mwenye umri wa miaka 23 wa Jamhuri ya Ireland mwezi Januari. (Mirror)
Real Madrid wanamfuatilia beki wa kati wa Bournemouth na Uholanzi Dean Huijsen, 19, huku wakitafakari uhamisho wa Januari. (Sun)
Juventus wanaweza kutafuta mkataba wa mkopo kwa beki wa kushoto wa Manchester United na Uholanzi Tyrell Malacia, 25, hadi mwisho wa msimu. ( TuttoMercato - in Italy)
Ipswich Town na Everton wanatazamia uhamisho wa mkopo kwa winga wa Aston Villa Muingereza Jaden Philogene, 22. ( Athletic - Subscription required)
Tottenham inaongeza hamu ya kumnunua kipa wa England na Wolves Sam Johnstone, 31. (Mirror)
Tottenham wanaweza kumkosa beki wa kushoto wa Denmark Patrick Dorgu, 20, huku Lecce wakiongeza mahitaji yao ya uhamisho hadi zaidi ya £30m. (GiveMeSport)
Fiorentina wanajaribu kufikia makubaliano na Liverpool kumsajili winga wa Italia Federico Chiesa, 27, kwa £5.8m. ( TuttoMercato -In Italy)

Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa kati wa England Fikayo Tomori, 27, anataka kusalia AC Milan licha ya Juventus kumtaka . (Gazetta -in Italy)
Manchester United wanatafuta njia za kumtoa winga wa Brazil Antony mwezi Januari, huku Real Betis wakionyesha nia ya kutaka kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Caught Offside)
Tottenham, Leicester na Bayer Leverkusen wanashindania kumsajili mlinzi wa Udinese mwenye umri wa miaka 22 raia wa Denmark Thomas Kristensen. (Football Insider)
End of Unaweza pia kusoma:
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












