Ni mchezaji gani atahama katika dirisha la usajili wa Januari?

Chanzo cha picha, Getty Images
Dirisha la uhamisho wa Januari ni wakati mgumu sana kufanya biashara. Lakini ratiba iliyosheheni mechi, majeruhi, malipo au mvutano wa kusalia, hayo yote yamaanisha makocha kadhaa wa Ligi Kuu ya Engaland, huenda watahitaji kuingia sokoni msimu huu wa baridi.
Dirisha la uhamisho la Januari kwa vilabu vya Uingereza limefunguliwa Jumatano, Januari 1 na litafungwa Jumatatu, 3 Februari.
BBC Sport inangazia wachezaji watano wenye hadhi ya juu ambao mustakabali wao unaweza kuamuliwa mwezi ujao.
Trent Alexander - Arnold (Liverpool)
Vyanzo vya habari vilisema katika mkesha wa Mwaka Mpya kwamba Real Madrid inataka kumsajili, Alexander-Arnold wa Liverpool mwezi Januari, lakini Liverpool imekataa.
Vyombo vya habari vya Uhispania pia viliripoti kuwa Real walikuwa tayari kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwezi huu.
Alexander-Arnold ni mmoja wa wachezaji watatu muhimu wa Liverpool katika miezi sita ya mwisho ya mkataba wake.
Alisema Arnold mwezi Septemba kwamba mazungumzo juu ya mkataba mpya hayatafanyika hadharani, jambo ambalo limeongeza hali ya sintofahamu juu ya nini kinamkabili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye amekuwa Liverpool tangu umri wa miaka sita.
Huku Liverpool wakipewa nafasi kubwa ya kushinda Ligi ya Premia, na wakionekana kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa na katika nusu fainali ya Kombe la Carabao, kuna uwezekano wa Real kukataliwa kumsajili kwa sasa - lakini hilo litadumu kwa muda gani?
Mkataba wake ni hadi: Juni 2025.
Anahusishwa na: Real Madrid, Manchester City.
Marcus Rashford (Man Utd)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa sasa swali ni lini Marcus Rashford ataondoka Manchester United? Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 27 alisema katika mahojiano katikati ya Desemba kwamba "yuko tayari kwa changamoto mpya" huku kukiwa na sintofahamu juu ya mustakabali wake Old Trafford.
Rashford amefunga mabao 138 katika mechi 426 alizoichezea klabu hiyo tangu aanze kucheza kwa mara ya kwanza mwaka 2016, ametokea katika timu ya vijana ya United. Msimu wa 2022-23 ndio wenye mafanikio zaidi alipofunga magoli 30 katika mechi zote.
Hata hivyo, ameshuka kiwango kwa muda wa miezi 18 iliyopita na kuvutia ukosoaji kutoka kwa wachambuzi na mashabiki. Rashford ni mmoja wa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi United ambayo inaweza kuwa kikwazo kwa uhamisho wowote Januari hii.
Mkataba wake ni hadi: Juni 2028.
Anahusishwa na: Paris St-Germain, Barcelona na vilabu vya Saudi Pro-League Al-Ahli, Al-Ittihad na Al-Qadsiah
Martin Zubimendi (Real Sociedad)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa Real Sociedad Martin Zubimendi atakuwa mmoja wa wachezaji wa watakao vutia zaidi mwezi Januari.
Liverpool walikuwa karibu kumsajili kinda huyo mwenye umri wa miaka 25 katika dirisha lililopita, lakini timu yake ilimtaka abaki.
Zubimendi, ambaye aliisaidia Uhispania kushinda Euro 2024, inasemekana anauzwa kwa pauni milioni 51.7 katika mkataba wake. Akiwa na Sociedad hawezi kukosa ofa.
Mkataba wake ni hadi: Juni 2027
Anahusishwa na: Liverpool, Arsenal, Manchester City, Barcelona
Ben Chilwell (Chelsea)

Chanzo cha picha, Getty Images
Ana umri wa miaka 28, Ben Chilwell, anapaswa kuwa katika kiwango cha juu kabisa cha maisha yake ya soka huko Chelsea, lakini badala yake amejikuta akipoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza pale Stamford Bridge chini ya kocha Enzo Maresca.
Chilwell, ambaye alijiunga na Chelsea kwa pauni milioni 45 kutoka Leicester mwaka 2020, amecheza kwa dakika 45 tu za mchezo wa Kombe la Carabao dhidi ya Barrow msimu huu, na haukuweza kuhama klabu hiyo katika dirisha lililopita.
Maresca alisema Chilwell ni miongoni mwa wachezaji "wanaofikiria kuondoka" na klabu "itajaribu kutafuta suluhu." Beki huyo wa kushoto, ambaye ameichezea England mechi 21, kwa mshahara wake kuna uwezekano mkubwa wa kuhamishwa kwa mkopo.
Amepewa mkataba hadi: Juni 2027
Anahusishwa na: Juventus, Brentford, Manchester United, West Ham, Fenerbahce
Matheus Cunha (Wolves)

Chanzo cha picha, Getty Images
Msimu wa 2024-25 umemfanya Matheus Cunha aonekane, ni msimu wa mapambano kwa Wolves.
Cunha amehusika katika mabao 11 katika mechi 11 zilizopita za Ligi Kuu England, akifunga mabao saba na kusaidia manne. Pia ndiye mchezaji wa kwanza wa Wolves kufunga mabao 16 ya ligi kuu ndani ya mwaka mmoja tangu John Richards afunge mabao 18 mwaka 1980.
Mbrazil huyo, 25, alisajiliwa kutoka Atletico Madrid kwa mkataba wa pauni milioni 35.
Amepewa mkataba hadi: Juni 2027
Anahusishwa na: Liverpool, Arsenal, Manchester City, Manchester United na Newcastle
Nani mwingine anaweza kuhama Januari?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kocha wa Chelsea, Maresca amesema Carney Chukwuemeka anauzwa na kiungo mwenzake Cesare Casadei anatolewa kwa mkopo.
Jaribio la Barcelona lililoshindikana kumsajili mlinzi wa Uhispania, Dani Olmo limetia shaka mustakabali wake katika klabu hiyo ya La Liga.
Mshambulizi wa Newcastle, Alexander Isak amekuwa akihusishwa mara kwa mara na Arsenal.
Florian Wirtz wa Bayer Leverkusen na Bruno Guimaraes wa Newcastle wote wamehusishwa na Manchester City.
Januari itakuwa dirisha la kwanza la uhamisho kwa kocha wa Manchester United, Ruben Amorim na anaweza kutaka kuleta wachezaji kadhaa ili kufanya mabadiliko.
Mshambulizi wa Sporting, Viktor Gyokeres amekuwa akihusishwa kuhamia Arsenal na United.
Mshambuliaji wa Uholanzi, Joshua Zirkzee na winga Antony ni miongoni mwa wanaohusishwa kuondoka Old Trafford.
Mshambulizi wa Lille, Jonathan David mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu na ametajwa kuhusishwa na vilabu kadhaa vya Ligi Kuu England.
Mshambuliaji wa Paris St-Germain, Randal Kolo Muani pia anaonekana kutaka kuondoka.
Tottenham wanaweza kulazimika kuingia dirishani huku mabeki Micky van de Ven na Cristian Romero wakiwa nje ya uwanja kutokana na majeraha.
Crystal Palace wako sokoni kutafuta mfungaji mabao pamoja na Everton, ambao wamefunga mabao 15 pekee ya ligi hiyo, pungufu kuliko timu yoyote isipokuwa Southampton.















