Kwa nini hakuna suluhu ya haraka Man Utd?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Mashabiki wa Manchester United hawakuchukua muda mrefu kumtungia wimbo Ruben Amorim.

Ni rahisi sana, maneno mawili tu. "Ruben Amorim, Amorim, Ruben Amorim" kupitia wimbo wa KC na bendi ya Sunshine ya ‘Give it Up’.

Amorim naye aliwatambua mashabiki waliosafiri walipomwimbia baada ya kipenga cha mwisho cha sare ya 1-1 dhidi ya Ipswich.

Amorim alipochambua mchezo wake wa kwanza kama kocha mkuu na vyombo vya habari huko Portman Road, ilionekana wazi kuwa wimbo huo ndio kitu cha kipekee ambacho kitafanyika kwa haraka katika uwanja wa Old Trafford katika kipindi cha wiki chache zijazo.

Shabiki yeyote wa United anayetarajia suluhu ya haraka kwa matatizo ambayo yalimsumbua Erik ten Hag na kuwaacha wakiwa katika nusu ya mwisho ya jedwali la Ligi ya Premia, atasikitika.

Kulingana na Amorim, United italazimika "kupitia changamoto" anapoingiza mawazo yake mapya ndani ya wachezaji wake.

"Najua inakatisha tamaa kwa mashabiki lakini tunabadilisha mengi wakati huu wenye mechi nyingi," alisema. "Tutapata shida kwa muda mrefu. Tutajaribu kushinda mechi lakini hii itachukua muda.

"Tunapaswa kuchukua hatari kidogo kwa [sasa] na katika mwaka ujao tutakuwa bora [vinginevyo] mwaka ujao katika hatua kama hii tutakuwa hapa na matatizo sawa na tulionayo sasa."

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Reuben Amorim

'Hana fimbo ya kufanya miujiza'

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Baada ya kuona dakika nyingine 90 za kukatisha tamaa zikipita, itakuwa rahisi kufikiria kwamba hakuna kilichobadilika kutoka kwa muda wa ukufunzi wa Ten Hag.

Licha ya kuanza kwao kwa kasi, huku Marcus Rashford akifunga bao baada ya sekunde 81 tu, United walirudi kucheza katika mfumo ule ule wa zamani.

Licha ya wageni hao kubuni nafasi ambazo hawakuzitumia, walijipata njia panda wakati wenyeji Ipswich walipovamia lango lao.

Kufikia kipenga cha mwisho, malengo yaliyotarajiwa ya United (xG) yalisalia kuwa 0.90, yakiwa mabaya zaidi na ya tatu msimu huu. Ipswich ilikuwa 1.75, kikiwa kiwango cha juu zaidi cha msimu.

Bao la kusawazisha kutoka kwa Omari Hutchinson liliwanufaisha wenyeji lilipogonga kichwa cha Noussair Mazraoui na kupita juu ya Andre Onana.

Lakini kama haingekuwa uokoaji mara mbili wa Onana kumnyima Liam Delap kikosi cha Amorim kingeishia kushindwa.

"Tungepoteza iwapo si Onana," alisema Amorim. "Alituokoa mara mbili ."

Kiungo wa kati wa zamani wa England Jamie Redknapp aliiambia Sky Sports: "ndicho nilichotarajia, hana fimbo ya miujiza.

"Wachezaji ambao wamekukatisha tamaa mwaka jana hawatakuwa tofauti ghafla kwa sababu eti Amorim ameingia. Kutakuwa na mabadiliko mengi katika miezi sita ijayo."

Haiwezekani kubadilika ghafla

Amorim aliingia Portman akiwa amevalia koti kubwa , ambalo halijoto ya wastani zaidi haikuhitaji.

Kulikuwa na kusudi juu ya tabia yake. Kumbatio lake la kabla ya mechi na nambari tofauti Kieran McKenna lilikuwa la kupendeza na hakuna zaidi.

Na bao la kwanza la Rashford ndani ya dakika mbili likawa mwanzo mzuri. Haikuwa muda mrefu ingawa Amorim akawaita Diogo Dalot na Alejandro Garnacho wakati wa mapumziko mafupi ya kucheza ili kuelezea jinsi alitarajia mchanganyiko wao kufanya kazi.

Mara baada ya mazungumzo hayo kufanywa, alielezea kile alichotaka kwa Jonny Evans na Casemiro.

Neno la kujifunza kwenye kazi haliwezi kuwa linalofaa zaidi.

"Je, kwa kweli, kutokana na kile tulichoona msimu huu, tulitarajia hii kuwa timu ya Manchester United iliyobadilishwa?" alihoji Chris Sutton kwenye Radio 5 Live. "Ruben Amorim anataka kubadili mtindo lakini wachezaji wamekuwa hawapo kwenye majukumu ya kimataifa. Haiwezekani kwake kugeuza tu swichi."

Mtindo huo, kama ilivyotarajiwa, ulikuwa na mabeki watatu wa kati na mabeki wa pembeni. Hili ndilo "wazo" ambalo Amorim alimwambia kila mtu wangeona mara tu atakapoanza kazi.

Nafasi za Noussair Mazraoui na Amad zilikuwa za kushangaza katika suala la uteuzi. Beki wa upande wa kulia wa mabeki watatu ni nafasi ya nne kwa Mazraoui msimu huu.

'Haiwezekani kubadilisha timu mara moja'

Aliingia kwenye Barabara ya Portman akiwa amevalia koti kubwa sana, ambalo halijoto ya wastani ya eneo hilo haikuhitaji.

Kulikuwa na kusudi kuhusu hatua yake. Kumbatio lake la kabla ya mechi na mkufunzi mwenza Kieran McKenna lilikuwa zuri bila shaka.

Na bao la kwanza la Rashford ndani ya dakika mbili likawa mwanzo mzuri. Haikuchukua muda mrefu Amorim alipowaita mabeki Diogo Dalot na Alejandro Garnacho wakati wa mapumziko mafupi ya mechi ili kuwaelezea jinsi alivyotaka washirikiane.

Mara baada ya mazungumzo hayo kufanywa, alielezea kile alichotaka kwa Jonny Evans na Casemiro.

"Je, kwa kweli, kutokana na kile tulichokiona msimu huu, tulitarajia kuwa timu hii ya Manchester United itakuwa imebadilika?" alihoji Chris Sutton kwenye Radio 5 Live. "Ruben Amorim anataka kubadili mtindo lakini wachezaji wamekuwa hawapo kwasababu ya majukumu ya kimataifa. Haiwezekani kwake kugeuza mara moja."

Mtindo huo, kama ilivyotarajiwa, ulikuwa na mabeki watatu wa kati na mabeki wa pembeni. Hili ndilo "wazo" ambalo Amorim alimwambia kila mtu wangeona mara tu atakapoanza kazi.

Nafasi za Noussair Mazraoui na Amad zilikuwa za kushangaza katika suala la uteuzi. Beki wa upande wa kulia wa mabeki watatu ni nafasi ya nne ambayo Mazraoui amehudumia msimu huu.

Amad ni winga lakini alionekana kuwa mbadala bora kuliko Alejandro Garnacho katika safu ya beki wa pembeni, ambaye alipewa nafasi ya mbele zaidi.

Mbio za kasi za mchezaji huyo wa Ivory Coast na krosi zake zilimtengenezea bao Rashford na mwishoni mwa mchezo alikuwa akirudi nyuma ili kuwasaidia mabeki kwenye eneo la hatari kabla ya Mazraoui kumtaka arejee juu.

"Kwa muda wa siku tatu ameimarika sana katika safu ya ulinzi," alisema Amorim. "Mpinzani wake wakati wote alikuwa beki wa kushoto kwa hivyo alikuwa kama winga anayemfkabili. Alikuwa makini na alifanya kazi kubwa."

'Lazima tutafute muda'

Tatizo la Amorim ni rahisi. Hana muda wa kufanyia kazi mbinu yake mpya akiwa na kikosi chake kizima.

Hadi pengo la siku sita kati ya mechi ya Ligi ya Premia na Newcastle mnamo 30 Desemba na safari ya Liverpool mnamo Januari 5, United hawana mapumziko katikati ya wiki.

Iwapo wataishinda Tottenham katika robo fainali ya Kombe la EFL mwezi ujao, muda wa mechi za mfululizo katikati ya juma utaongezeka hadi Februari.

Inaongeza umakini wa kuwa katika nafasi ya nane bora - kwa sasa wako nafasi ya 15 - kwenye jedwali la Ligi ya Europa.

Bila hivyo - na isipokuwa watashindwa kufuzu hadi hatua ya muondoano - kutakuwa na wiki mbili za kati kupigania raundi ya mchujo.

Mpango wa awali wa Amorim wa kukabiliana na tatizo hili ni kuwafanyia wachezaji ambao hawachezi mazoezi mazuri siku inayofuata.

"Lazima tupate muda," alisema. "Njia pekee ya kufanya hivyo ni kama vijana ambao hawachezi wana mazoezi. Watu walio kwenye benchi wanataka kucheza hivyobasi wanahitaji kufanya mazoezi.

"Kwa ratiba hii, tunahitaji kuwazungusha wachezaji. Baadhi ya wachezaji watacheza siku inayofuata ambapo watalifanyia kazi wazo letu kisha watabadilisha msimamo wao."