Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Man United yapewa fursa ya kumsajili Victor Osimhen

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Victor Osimhen
Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester United wamepewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen mwezi Januari, huku Napoli wakiwa tayari kwa mkataba wa kubadilishana wachezaji kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Galatasaray. (TBR Football)

Everton wanajiandaa kumpa kipa wa England Jordan Pickford, 30, mkataba mpya ambao utamweka katika klabu hiyo kwa maisha yake yote yaliyosalia. (TBR Football)

Chelsea, Arsenal na Tottenham zote zimetuma maskauti kumtazama beki wa pembeni wa Club Brugge na Ubelgiji Maxim de Cuyper, 24. (Caughtoffside)

..

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Randal Kolo Muani

FC Zurich wamewasiliana na Arsenal kuuliza kuhusu upatikanaji wa mshambuliaji wa Uingereza Nathan Butler-Oyedeji, 21, mwezi Januari. (Football Insider),

Paris St-Germain huenda wakaipa Arsenal nafasi ya kumsajili fowadi wao wa nje wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 26. (Standard).

Bosi wa Brighton Under-18s Inigo Calderon, 42, yuko kwenye mazungumzo ya juu ili kuwa meneja mpya wa Bristol Rovers. (Sky Sports), nje

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Florian Wirtz

Bayern Munich ina matumaini ya kutaka kumnunua kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Florian Wirtz, 21, ambaye yuko kwenye majadiliano na Bayer Leverkusen kuhusu mkataba mpya. (Sky Germany),

Mkufunzi wa Leicester City Ruud van Nistelrooy anaweza kuegemea kwenye uhusiano wake na Manchester United ili kupata saini ya mkopo inayofaa Januari. (Football Insider)

Manchester United walianza kutafuta mrithi wa muda mrefu wa Erik ten Hag mara tu meneja wao wa zamani Mholanzi alipotia saini mkataba mpya msimu wa joto. (Telegraph – Subscription Required),

Imetafsiriwa na Seif Abdalla