Kwa nini ni vigumu kutabiri matetemeko ya ardhi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Na Christal Hayes BBC News, Los Angeles Max Matza BBC News, Seattle
Maelfu ya watu wamefariki dunia na maelfu ya wengine kujeruhiwa vibaya huko Myanmar na nchi jirani ya Thailand na China kutokana na tetemeko kubwa la ardhi la ukubwa wa 7.7. Ni tetemeko la hivi karibuni kuathiria maelfu ya watu, ukiacha matetemeko zaidi ya 100,000 ambayo hutokea kila mwaka duniani.
Brent Dmitruk anajiita mtabiri wa matetemeko ya ardhi.
Mnamo katikati ya Oktoba, alieleza kwa wafuasi wake maelfu kadhaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba tetemeko la ardhi lingepiga sehemu ya magharibi kabisa ya California, kusini mwa mji mdogo wa pwani wa Eureka.
Miezi miwili baadaye, tetemeko la ukubwa wa 7.3 liligonga eneo hilo kaskazini mwa California - likiwaweka mamilioni ya watu chini ya tahadhari ya tsunami na kuongeza idadi ya wafuasi wa Bw. Dmitruk mtandaoni huku wakimgeukia kutaka kutabiri tetemeko lingine.
"Hivyo kwa watu wanaoshuku kile ninachofanya, je, unaweza kusema ni nimebahatisha? Inahitaji ujuzi wa hali ya juu kutambua ambapo matetemeko ya ardhi yatatokea," alisema kwenye sherehe za Mwaka Mpya (2025).
Lakini kuna tatizo moja: matetemeko ya ardhi hayawezi kutabiriwa, wanasayansi wanaochunguza matetemeko wanasema.
Ni hali hii ya kutokuwa na uhakika ndio inayofanya matetemeko ya ardhi kuwa ya kutisha na vigumu kurtabirika. Mamilioni ya watu wanaoishi kwenye pwani ya magharibi ya Kaskazini mwa Amerika wanaogopa kuwa "tetemeko" linaweza kutokea wakati wowote, likibadilisha mazingira na maisha ya wengi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Lucy Jones, mtaalamu wa Huduma ya Jiografia ya Marekani (USGS) kwa zaidi ya miongo mitatu na kuandika kitabu kiitwacho The Big Ones, ameweka nguvu nyingi kwenye utafiti wake kuhusu uwezekano wa matetemeko ya ardhi na kuboresha ustahimilivu wa kustahimili matukio kama hayo.
Kwa muda wote alioujihusisha na masuala ya matetemeko, Dr. Jones alisema kumekuwa na watu wanaotaka jibu la lini tetemeko wakiita "yule mkubwa" - neno linalomaanisha vitu tofauti kwenye maeneo tofauti - atatokea na kudai kwamba wamevumbua njia ya utabiri.
"Ni majibu ya kawaida ya binadamu kuwa na hofu," aliiambia BBC. "Ingawa hakuna nguvu yoyote ya kutabiri."
Pamoja na matetemeko ya ardhi 100,000 yanayohisiwa duniani kote kila mwaka, kwa mujibu wa Huduma ya Jiografia ya Marekani (USGS), ni rahisi kuelewa kwamba watu wanataka kuwa na tahadhari.
Eneo la Eureka - mji wa pwani kilomita 270 (434km) kaskazini mwa San Francisco, ambapo tetemeko la Desemba lilitokea, limeshuhudia matetemeko zaidi ya 700 ndani ya mwaka mmoja tu - ikiwa ni pamoja na zaidi ya 10 katika juma moja lililopita, data inaonyesha.
Eneo hili, ambalo ndilo Bw. Dmitruk alitabiri vyema kwamba tetemeko lingetokea, ni mojawapo ya "sehemu zenye shughuli nyingi za seismolojia" nchini Marekani, kwa mujibu wa USGS. Tishio lake linatokana na mikutano ya sehemu tatu za tectonic, eneo linalojulikana kama Mendocino Triple Junction.
Ni harakati za sehemu hizo kwa uhusiano wa kila moja - iwe juu, chini au kando - zinazozalisha mkazo kuongezeka. Wakati mkazo huo unapojitokeza, tetemeko linaweza kutokea.
Kufikiria kwamba tetemeko lingetokea hapa ni bahati nasibu rahisi, alisema Dr. Jones, ingawa tetemeko kubwa la ukubwa 7 kwa kipimo cha Ritcher ni nadra sana.
USGS inasema kumekuwa na matetemeko 11 ya ukubwa kama huo au mkubwa zaidi tangu mwaka 1900. Matano, ikiwa ni pamoja na lile Bw. Dmitruk alilopigia debe ama kutabiri kwenye mitandao ya kijamii, yalitokea katika eneo hilo hilo.
Ingawa utabiri ulikuwa sahihi, Dr. Jones aliiambia BBC kwamba ni vigumu kwa tetemeko lolote - ikiwa ni pamoja na yale makubwa ya kuathiria jamii - kutabiriwa kwa usahihi.
Kuna seti tata na "ya kubadilika" ya mambo ya kijiografia inayosababisha tetemeko, alisema Dr. Jones.
Wanasayansi wanajua kwa nini tetemeko hutokea - harakati za ghafla kwenye mistari ya makosa - lakini kutabiri tukio kama hilo ni jambo ambalo USGS wanasema haliwezi kufanyika na ni jambo ambalo "hatutaraji kujua jinsi ya kufanya hivyo katika siku zijazo." Anachokisema ni ngumu na kazi sana kutabiri tetemeko l;a ardhi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Shirika hilo linakiri kuwa linaweza kukadiria uwezekano wa matetemeko katika eneo fulani ndani ya kipindi cha miaka fulani - yani hicho ndicho kwa sasa wanachoweza kujivunia kufanya.
Rekodi za kijiografia zinaonyesha kwamba baadhi ya matetemeko makubwa zaidi, yanayojulikana hutokea kwa mzunguko fulani ikiwemo eneo la Cascadia na San Andreas huko Kusini mwa California, huku matetemeko yenye mshtuko makubwa yakitokea kila miaka 200-300. Wataalamu wamesema tetemeko linaweza kutokea wakati wowote katika kila eneo.
Dr. Jones anasema kuwa katika kipindi cha kazi yake, amepokea maelfu ya watu wakimjulisha kuhusu utabiri wa tetemeko kubwa - ikiwa ni pamoja na watu katika miaka ya 1990 waliotuma faksi ofisini kwake kwa matumaini ya kuwaonya.
"Wakati unapopokea utabiri kila wiki, mtu mmoja atakuwa na bahati, sivyo?" anasema akiwa na kicheko. "Lakini kisha hiyo kawaida ingeenda kwa vichwa vyao na kutabiri matetemeko 10 zaidi ambayo hayakuwa sahihi."
Kama ilivyokuwa kwa Bw. Dmitruk, ambaye hana ujuzi wa kisayansi. Amekuwa akitabiri kwa muda mrefu kwamba tetemeko kubwa litagonga Kusini-magharibi mwa Alaska, Japan au visiwa vya kando ya New Zealand, lenye ukubwa mkubwa hivyo alisema linaweza kusababisha usumbufu wa biashara ya kimataifa.
USGS inasema utabiri wa tetemeko lazima uwe na vipengele vitatu vilivyoainishwa - tarehe na saa, eneo la tetemeko na ukubwa - ili uwe na manufaa yoyote.
Lakini muda wa Bw. Dmitruk unabadilika kila wakati.
Wakati mmoja, alisema litakuwa kabla au baada ya kuapishwa kwa Rais wa Marekani Donald Trump.
Kisha alisema litatokea bila shaka kabla ya 2030.
Ingawa tetemeko kubwa bado halijatokea, Bw. Dmitruk alisema bado anaamini kuwa litakuja.
"Siamini ni bahati tu," alisema kwa BBC. "Si jambo la bahati."
Fikra hii ni ya kawaida kuhusu matetemeko ya ardhi, alisema Dr. Jones.
"Watu wengi wanaogopa matetemeko ya ardhi, na njia ya kukabiliana nayo ni kutabiri [lini] itatokea."
Jinsi unavyoweza kujiandaa kwa kutokuwa na uhakika wa tetemeko

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini ingawa huwezi kutabiri lini tetemeko la ardhi litatokea, haimaanishi kuwa haupaswi kujiandaa, wanasema wataalamu.
Kila mwaka, kwenye Alhamisi ya tatu ya Oktoba, mamilioni ya Wamarekani hushiriki kwenye zoezi kubwa zaidi la matetemeko duniani: The Great Shake Out.
Iliundwa na kikundi cha Kituo cha Matetemeko cha Kusini mwa California, kilichomjumuisha Dr. Jones.
Wakati wa zoezi hili, watu wanajifunza miongozo ya "Kutambaa , Kufunika, na Kushikilia": wanatambaa kwa magoti, wanajificha chini ya kitu imara kama dawati, na kushikilia kwa dakika moja.
Zoezi hili limekuwa maarufu sana tangu kuanzishwa kwake na sasa limeenea kwenye pwani ya maeneo ya matetemeko hadi majimbo mengine na nchi nyingine.
Ikiwa uko nje, watu wanashauriwa kufika kwenye eneo la wazi lililo mbali na miti, majengo au nguzo na waya za umeme. Karibu na bahari, watu wanajifundisha kukimbia kuelekea maeneo ya juu na miinuko baada ya tetemeko kutulia ili kujiandaa kwa uwezekano wa tsunami.
"Sasa, wakati ardhi haijatikisika, wakati sio hali ya mvutano mkubwa, ndiyo wakati bora wa mazoezi," alisema Brian Terbush, Meneja wa Programu ya Matetemeko na Volkeno kwa Idara ya Usimamizi wa Dharura ya Jimbo la Washington.
Mbali na mazoezi haya, wakazi wa majimbo ya Pwani ya Magharibi hutumia mfumo wa simu unaosimamiwa na USGS uitwao ShakeAlert.
Mfumo huu unafanya kazi kwa kugundua mawimbi ya shinikizo yanayotolewa na tetemeko la ardhi. Ingawa hauwezi kutabiri wakati tetemeko litatokea katika siku zijazo, hutoa onyo la sekunde ambazo zinaweza kuwaokoa maisha. Huu ndio ukaribu wa kutabiri matetemeko ya ardhi ambao umetengenezwa na kutegemewa hadi sasa. si zaidi ya hapo, kutabiri kikamilifu , kusema litatokea siku fulani, saa fulani na dakika fulani, ni vigumu kwa mujibu wa wataalamu.














