Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Newcastle kumuuza Isak ikiwa haitafuzu klabu bingwa Ulaya

Isak

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Isak
Muda wa kusoma: Dakika 2

Newcastle itakuwa tayari kumuachia Alexander Isak kuondoka kwa £83.3m (100m euros) katika dirisha kubwa lijalo kama haitafuzu michuano ya Klabu bingwa Ulaya, huku Barcelona, Liverpool, Arsenal na Chelsea miongoni mwa vilabu vinavyomuania mhambuliaji huyo Msweden mwenye umri wa miaka 25. (Sport - in Spanish), external

Atletico Madrid inamtamka kiungo mnigeria wa Leicester, mwenye umri wa miaka 28, Wilfred Ndidi. (Caught Offside), external

Ndindi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wilfred Ndindi

Everton itamfukuzia mlinzi wa kati mfaransa wa Burnley, Maxime Esteve (22), iwapoa mlinzi wake muingereza Jarrad Branthwaite, 22, ataondoka katika katika dirisha kubwa la majira ya joto. (Sun - subscription required), external

Chelsea imekuwa ikiwafuatilia kwa karibu mapacha wa Middlesbrough's Anton na Bailey Palmer wenye miaka 16, huku Tottenham, Aston Villa na Brighton pia zikionyesha nia viungo hao wanaochezea timu ya taifa ya Uingereza ya chini ya miaka 17. (TBR Football).

Everton wanatarajia kufufua tena nia yao ya kumsaka winga mfaransa wa Lyon Rayan Cherki, baada ya kumtaka katika dirisha lililopita la Januari. (Football Insider).

Cherki

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rayan Cherki

Klabu kadhaa za ligi kuu England zinamfuatilia mshambuliaji kinda wa Ireland anayechezea Shamrock Rovers, Michael Noonan, 16, amaye amekuwa mfungaji bora wa pili kinda kwenye historia ya michuano vilabu ya UEFA, alipofunga dhidi ya Molde kwenye michuano ya Conference League alhamis iliyopita. (Times - subscription required), external

Real Madrid inajaribu kuachana na ligi kuu ya Hispania ili kwenda kushiriki ligi nyingine kuonyesha kupinga uongozi wa rais wa La Liga,Javier Tebas kwa kile wanachodai uwepo wa maamuzi ya upendeleo. (Sport - in Spanish)