Je, hii ndiyo nchi yenye mapinduzi mengi zaidi duniani?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Polisi walimkamata kiongozi wa mapinduzi saa chache baada ya wanajeshi kuivamia ikulu ya rais katika mji mkuu wa Bolivia, La Paz.

Bustani ya Murillo, medani ambazo ofisi muhimu za serikali ziko, zimejaa mamia ya askari na magari ya kivita.

Gari la kivita lilijaribu kuharibu lango la kuingilia katika ikulu ya rais. Baada ya hapo wanajeshi waliondoka kutoka kwenye mji huu wa Amerika ya Kusini.

Kuna sababu tatu kuu za shambulio hili.

g

Chanzo cha picha, MINISTRY OF GOVERNMENT OF BOLIVIA HANDOUT / GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Jenerali Zuniga aliongoza vikosi vilivyovamia uwanja wa medani ya Murillo siku ya Jumatano

1.Historia ya Uasi

Kwa saa chache, kumbukumbu za giza la idadi kubwa ya mapinduzi ya Bolivia na serikali zilizopinduliwa tangu miaka ya 1950 zilirejea akilini mwa wengi.

Kwa mujibu wa uchambuzi wa data za wanahistoria wa Marekani Jonathan Powell na Clayton Thain, Bolivia imepitia mapinduzi kadhaa katika kipindi cha miaka 74 iliyopita. Nusu yake yalizuiwa.

Powell ameiambia BBC kwamba Bolivia huenda ikawa na mapinduzi makubwa zaidi duniani. Hata hivyo, alisema, "Ni vigumu kupata taarifa za kuaminika kuhusu mapinduzi yanayosemekana kufanyika kabla ya mwaka 1950".

Wachambuzi waliiambia BBC kwamba wakati mapinduzi ya kijeshi yanapotofautishwa na uasi wa kijamii au kutwaliwa kwa madaraka kinyume na katiba, kuna utata kati ya mambo hayo mawili.

Kulingana na Fabrice Lehouk, mwanasayansi wa kisiasa kutoka Chuo Kikuu cha North Carolina nchini Marekani, kumekuwa na mapinduzi ya kijeshi ya 320 katika Amerika ya Kusini tangu 1900.

"mengi kati yake yana uhusiano na Ecuador, Argentina, Bolivia," Lehouk alisema.

Karibu nusu ya mapinduzi haya yamefanikiwa, Lehouc anasema. Zaidi ya nusu ya mapinduzi nchini Bolivia katika karne ya 20 yalifanikiwa kumpindua rais.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baada ya zoezi la uhamasishaji wa kijeshi kumalizika, biashara katika mji mkuu wa Bolivia, La Paz, ziliendelea kama kawaida
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa hivyo, ni nini kinachosababisha machafuko haya ya hivi karibuni?

Jenerali Juan Jose Zuniga alikuwa mkuu wa jeshi hadi alipoondolewa katika wadhifa wake siku ya Jumanne.

Rais Luis Arce alimng'oa Jenerali Zuniga katika wadhifa wake wa kijeshi baada ya kutishia kumkamata rais wa zamani wa Bolivia Evo Morales katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2025, ingawa haruhusiwi kugombea katika uchaguzi huo kwa mujibu wa katiba.

Jenerali huyo alielezea vitendo vyake kama "jaribio la kujenga upya demokrasia".

Zuniga alikamatwa sekunde chache baada ya kuviambia vyombo vya habari kuwa jeshi liliingilia kati ombi la rais.

Rais Louis Arce amelaani shambulio hilo na kulitaja kuwa "jaribio la mapinduzi". Alitoa wito kwa raia kwamba wote wanapaswa kuungana kwa ajili ya kuhifadhi demokrasia".

Mamia ya raia wa Bolivia waliingia mitaani kufanya maandamano kuiunga mkono serikali.

Wakati hali ya wasiwasi nchini humo ikizidi kuongezeka, kuna wasiwasi.

Hali mbaya ya kiuchumi na ushindani wa kisiasa kati ya Rais Arce na Morales wa zamani imesababisha maandamano mengi na mgawanyiko wa kidini nchini humo katika miezi michache iliyopita.

g

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Rais wa Bolivia Luis Arce

Ars dhidi ya Morales

Vita vya kuwania madaraka kati ya washirika wa zamani wa kisiasa Rais Arce na rais wa zamani Morales vinaonekana kuendelea kabla ya uchaguzi wa 2025.

Wote wawili ni wa chama kimoja cha kisiasa 'Movimiento al Socialismo' (MAS). jina lake la chama hicho likimaanisha : ni wakati wa ujamaa.

Licha ya Mahakama ya Katiba nchini humo kumtangaza kuwa hana sifa ya kugombea muhula wa nne Desemba mwaka jana, Morales alitangaza nia yake ya kuwania urais, jambo lililozua utata.

Tovuti ya mahakama inasema kuwa ukomo wa muda ni "hatua inayofaa kuhakikisha kuwa hawana nia ya kubaki madarakani milele".

Hata hivyo, tangazo la Morales lilikuwa changamoto kwa Arce, ambaye anataka kuwa rais tena.

Kufuatia madai kwamba alijaribu kuiba matokeo ya urais katika uchaguzi wa 2019, Morales alilazimika kujiuzulu urais na kukimbia nchi kufuatia uingiliaji kati wa wakuu wa jeshi.

Hata hivyo, amekanusha madai hayo ya wizi.

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jeanine Anez ahukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa uchochezi

Jeanine Anez alihudumu kama rais wa mpito kuanzia mwaka 2019 hadi 2020. Hata hivyo, alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela baada ya kutuhumiwa kwa mapinduzi ya kumuondoa Morales madarakani.

Ars alishinda uchaguzi ujao.

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Licha ya kuenguliwa na mahakama, Morales anatarajiwa kuwania muhula wa nne kama rais

Morales alitishia "mgogoro wa kijamii" nchini Bolivia ikiwa mpango wa kuondolewa kwake utaendelea. Alidai kuwa rais wa sasa anajaribu kumzuia asiende kwenye uchaguzi.

Morales alikuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo. Alikuwa rais kuanzia mwaka 2006 hadi 2019. Licha ya umaarufu wake, anajulikana kama kiongozi mwenye utata.

Morales alionya kwamba Rais Arce na Jenerali Zuniga walikuwa wakipanga 'mpango wa giza' dhidi yake.

Morales alitoa wito kwa raia wa Bolivia kujitokeza kulinda demokrasia wakati wa uhamasishaji wa kijeshi. Unapendekeza kwamba serikali ya Ars inapaswa kubaki madarakani kwa muda mfupi, badala ya jeshi kuchukua serikali.

Rais Ars alimteua Mkuu wa Jeshi mnamo 2022. Wote wawili walikuwa wakosoaji wa Morales.

Akizungumza katika mahojiano ya televisheni siku ya Jumatatu, Zuniga alisema atamzuia rais wa zamani Morales "hata kama inamaanisha kukanyaga katiba".

Lakini wakati wa kukamatwa kwake siku ya Jumatano, rais alimshutumu Arce kwa kupanga mapinduzi hayo ili "kuongeza umaarufu wake".

Zuniga hajatoa ushahidi wowote wa kuunga mkono madai yake. Ukweli halisi katika suala hili bado haujajitokeza.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

3. Tishio kwa 'Muujiza wa Kiuchumi'

Mvutano nchini Bolivia unakuja wakati kukiwa na hali ngumu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Bolivia inaendelea kuwa uchumi unaokua kwa kasi na utulivu na mfumuko wa bei wa chini, ingawa nchi jirani katika Amerika ya Kusini zinapambana na mfumuko wa bei sugu.

Hata hivyo, Bolivia pia ina kiwango cha juu cha umaskini katika Amerika ya Kusini.

Kadri sarafu ya Bolivia inavyopungua, watu hulipa dola za Marekani kwa ununuzi wa bidhaa.

Hata hivyo, wachumi wanaonya kwamba kushuka kwa thamani ya sarafu ya Marekani kunatishia "Muujiza wa Uchumi wa Bolivia".

Ukosefu wa dola ya Marekani unaumiza mauzo ya nje na uagizaji. Wananchi wa Bolivia wanalazimika kuchukua mifuko yao hata kununua mahitaji muhimu kama vile mchele na nyanya.

Mchumi wa Bolivia Jaime Dunn anasema kuwa uraia wa Morales wa sekta ya hydrocarbon mwaka 2006 umepunguza uzalishaji wa gesi asilia nchini humo na kusababisha uhaba wa dola za Marekani.

Serikali za Morales na Arce zilitumia dola za Marekani kufadhili mipango ya kijamii kama vile mpango wa ununuzi wa mafuta.

"Hali hii imesababisha mgogoro nchini. Ingawa mapato yamepungua, matumizi ni ya juu sana. "Tangu mwaka 2014, mapato yanayotokana na gesi asilia yametosha kufidia madeni ya ndani na nje ya nchi," alieleza Dunn.

Kwa mujibu wa Rais Arce, Bolivia inaagiza asilimia 56 ya mafuta ya petroli na asilimia 86 ya dizeli.

Sasa, wataalam wanaonya kuwa hakuna akiba ya dola ya kutosha kuagiza mafuta muhimu. Maandamano pia yanazidi kuongezeka nchini humo.

Jaribio la mapinduzi siku ya Jumatano lililaaniwa na ulimwengu.

Wachambuzi wanasema hatua ya Jumatano inaonekana kuwa yalikuwa ni mapinduzi ya haraka badala ya kunyakua mamlaka yote.

Huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika mwaka 2025, bado inasubiriwa kuona iwapo uwezo wa kuondoa jaribio la mapinduzi utaongeza uungwaji mkono wa wananchi kwa serikali, au kuudhoofisha katika mapambano haya ya kuwania madaraka.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Seif Abdalla