Je sanaa ya Cuba inawasilisha vipi mapambano ya ukombozi wa Afrika?

An Ospaaal poster called After Emory Douglas, 1968 showing women in headscarves with babies and guns

Chanzo cha picha, Lázaro Abreu Padrón

Presentational white space

Maonyesho ya vipeperushi vya matangazo ya propaganda za Cuba huko London yanaonyesha msaada ambao Fidel Castro alitoa kwa harakati za ukombozi wa Afrika wakati wa vita baridi.

Kazi za sanaa zilizotengenezwa katika kampuni ya Castro ya mshikamano wa watu wa Asia, Afrika na Amerika ya Kusini (Ospaaal) ambayo ilianzishwa mwaka 1966 huko Havanna katika mkutano wa 'Tricontinental' kwa lengo la kupambana na ukoloni wa Marekani.

"Nchi nyingi za Afrika ziliwakilishwa kama wajumbe katika harakati za ukombozi. Vilevile Castro alisaidia kuwaunganisha baadhi ya viongozi haswa kutoka Guinea-Bissau," Olivia Ahmad, miongoni mwa wachoraji aliiambia BBC.

A Ospaaal poster entitled Day of solidarity with people of Guinea-Bissau and Cape Verde Islands, 1974, showing Amílcar Cabral

Chanzo cha picha, Olivio Martínez Viera

Maelezo ya picha, Amílcar Cabral akiwa anahamasisha mshikamano wa watu wa Guinea-Bissau na kisiwa cha Cape Verde, 1974
Presentational white space

Cabral aliongoza mapigano dhidi ya ukoloni wa Ureno huko Guinea-Bissau na kisiwa cha Cape Verde, lakini aliuwawa mwaka 1973, mwaka mmoja kabla Guinea-Bissau kupata uhuru.

Bi Ahmad anasema kuwa mkutano ule wa Tricontinental ulikuwa umepangwa kufanyika lakini haukufanyika hivyo ukachapishwa.

Hivyo machapisho yake kuwa kiungo muhimu cha taarifa na uwasilishi.

Mapinduzi ya Amerika Kusini yalijulikana zaidi, Ernesto "Che" Guevara, labda alikuwa mpambanaji zaidi katika harakati hizo.

"Lakini pia kuna viongozi wa kiafrika ambao wamekuwa wakikumbukwa kwa ushujaa wao "

An Ospaaal poster entitled Che Guevara, 1969, showing his face over a rainbow design

Chanzo cha picha, Alfredo G Rostgaard

Maelezo ya picha, Che Guevara imeonyeshwa kwenye bango la mwaka 1969
Presentational white space

Guevara aliipambania nchi ambayo inatambulika sasa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo mwaka 1965 ,kwa dhamira iliyoshindwa ya kuchochea uasi dhidi ya utawala wa kigeni wa miaka minne baada ya kuuawa kwa shujaa wa uhuru wa Kongo, Patrice Lumumba.

Lumumba aliuwawa miezi minne baada ya kuchaguliwa kuwa waziri mkuu wa kwanza kidemokrasia katika taifa lake, jambo ambalo lililaumiwa na wanaintelijensia wa Marekani na Uingereza.

An Ospaaal poster, entitled Day of Solidarity with the Congo, 1972, showing the face of Patrice Lumumba over a map of Africa

Chanzo cha picha, Alfredo Rostgaard

Maelezo ya picha, Patrice Lumumba , 1972
Presentational white space

"Michoro hiyo inavutia kwa sababu kwa sababu ya sanaa yake ya ushawishi ambao huwezi kutarajia kuuona, michoro hii ina muonekano wa kuwaenzi kwa furaha watu ambao walijitoa mhanga ili kuleta ukombozi," anasema bi Ahmad.

Maonyesho haya ya picha yaliobuniwa Cuba, yaliandaliwa na wabunifu 33 na wengi wao wakiwa wanawake.

Picha kuhusu Guinea-Bissau inamuonyesha mwanamke akiwa ameshikilia bunduki, huyo ni Berta Abelenda Fernandez, "ni miongoni mwa wanawake ambao walitumiwa katika picha nyingi za Ospaaal", Bi Ahmad alieleza.

An Ospaaal poster, entitled Day of Solidarity with the People of Guinea-Bissau and Cape Verde, 1968 showing a woman with a gun

Chanzo cha picha, Berta Abelénda Fernández

Maelezo ya picha, Siku ya mshikamano kwa watu wa taifa la Guinea-Bissau na Cape Verde, 1968
Presentational white space
The cover of the magazine Tricontinental 95 with the word Angola and a woman holding a machinegun

Chanzo cha picha, Ospaaal

Maelezo ya picha, Picha iliyopo kwenye kasha la jarida la 'Tricontinental' mwaka 1995
Presentational white space

Castro alijitoa sana katika taifa la Angola, sio kama kwenye operesheni ya siri ya Cuba barani Afrika ya mwaka 1960s, wakati ambao kulikuwa na fursa nyingi za kujinadi kimataifa kuhusu mshikamano na kuleta mabadiliko kidunia.

Baada ya Angola kupata uhuru wake kutoka kwa wareno mwaka 1975, Castro alituma msaada wa kijeshi kwa kutuma wanajeshi wake 35,000 kusaidia na kusitisha chuki dhidi ya ubaguzi wa rangi huko Afrika kusini , jambo ambalo Marekani lilipanda katika utawala wake.

An Ospaaal entitled Day of Solidarity with Angola, 1972, with a patterned poster and face

Chanzo cha picha, José Lucio Martínez Pedro

Maelezo ya picha, Angola, 1972
Presentational white space

Inakadiriwa kuwa wacubani wapatao 4,300 waliuwawa katika migogoro ya Afrika, nusu yao waliuwawa nchini Angola peke yake katika mapigano yaliyoisha mwaka 2002.

Picha hizi zinabeba ujumbe wa mshikamano waukombozi .

Picha hizi wameweka maelezo ya lugha nne, kiingereza, kifaransa, kispaniola na kiarabu ili ziweze kuenea katika maeneo mngi zaidi ya Cuba pekee.

An Ospaal poster called International Week of Solidarity with the Peoples of Africa, 1970, showing the word Africa breaking through barbed wire

Chanzo cha picha, Gladys Acosta Ávila

Maelezo ya picha, Wiki ya kimataifa ya International Week of Solidarity with the Peoples of Africa, 1970
Presentational white space

Unaweza kusoma pia:

An Ospaaal poster called Day of World Solidarity with the Struggle of the People of Mozambique, 1973, showing a dagger being pushed into a hand

Chanzo cha picha, Olivio Martínez Viera

Maelezo ya picha, Harakati za watu wa Msumbiji, 1973
Presentational white space

Picha nyingi zimelenga mapambano dhidi ya watu wachache weupe nchi Afrika Kusini , mapambano ambayo yaliweza kutokomezwa mwaka 1994, wakati ambapo Nelson Mandela alipochaguliwa kuwa rais.

An Ospaaal poster entitled Day of Solidarity with the People of South Africa, 1968, showing a stylised design of a warrior with a spear and shield

Chanzo cha picha, Berta Abelénda Fernández

Maelezo ya picha, Afrika kusini , 1968
Presentational white space

Kitabu cha mapinduzi ya Cuba Marekani kilitoa fursa ya kuitangaza ndege ya Afrika kusini na kuijumuisha kwenye mkutano wa 'Tricontinental' wa mwezi Julai -Agosti mwaka 1968 ikitoa ahadi ya kutokomeza ubaguzi wa rangi ambao umesababisha kundi kubwa la waafrika waliopinga ubaguzi kuwekwa gerezani na maelfu ya waafrika wakiwa wanafanyishwa kazi kama watumwa katika migodi na maeneo mengine.

An Ospaaal poster entitled South Africa - Against Apartheid, 1982, showing a man with a bear chest and bleeding heart shaped like Africa

Chanzo cha picha, Rafael Morante Boyerizo

Maelezo ya picha, Afrika Kusinia - ubaguzi wa rangi, 1982
Presentational white space

Baada ya Mandela kufungwa gerezani mwaka 1964, ilikuwa ni kosa la jinai nchini Afrika kusini kwa mtu kumpiga picha au kuchapisha picha yake ya zamani . Picha ya mchoro huu ilitolewa mwaka 1989, mwaka mmoja kabla hajatolewa gerezani baada ya kufungwa kwa miaka 27.

An Ospaaal poster entitled Nelson Mandela, 1989 with the words: "Symbol of the anti-apartheid struggle"

Chanzo cha picha, Alberto Blanco González

Maelezo ya picha, Nelson Mandela, 1989
Presentational white space

Msanii aliyechora picha hiyo alikuwa anakaa Havana na alikuwa anajaribu kutumia uwakilishi wa watu kiuhalisia katika siasa.

An Ospaaal poster entitled Namibia Will Win! 1977 showing the child crying and the image of a fighter in one tear

Chanzo cha picha, Víctor Manuel Navarrete

Maelezo ya picha, Ushindi wa Namibia 1977
Presentational white space
An Ospaaal poster entitled Day of Solidarity with Zimbabwe, 1969. showing a statue holding a gun

Chanzo cha picha, Jesús Forjans Boade

Maelezo ya picha, Ukombozi wa Zimbabwe, 1969
Presentational white space

Dhana ya mshikamano kimataifa imebadilika na unaweza kuona ni kwa nini?

An Ospaaal poster entitled Long Live Free Zimbabwe, 1980 showing a woman holding up a banner with that phrase

Chanzo cha picha, Lázaro Abreu Padrón

Maelezo ya picha, Uhuru wa Zimbabwe, 1980
Presentational white space