Kenya: Sanaa ya uchoraji yapata sura mpya

Train with grafitti
Presentational white space

Mabogi ya gari ya moshi yanayoonekana hayana kazi jijini la Nairobi, Kenya kuna jamii ya wachoraji inayojipambanua kuoonesha ubunifu wao.

Mita chache kutoka barabara yenye shughuli nyingi, utaona miti na manyasi lakini ukitupa macho upande wa reli ya zamani kuna mabogi yaliyozeeka ambayo utadhani hayana kazi.

Mabogi hayo yamekua nyumbani kwa kundi la wachoraji mahiri wa sanaa wanaofahamika kama Bombsquad, ama BSQ, kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Mabogi yalichorwa graffiti ni mali ya makavazi ya reli jijini Nairobi ambayo utafikiria yaliegeshwa nyuma ya ukumbi wake wa maonesho yake kw amiongo kadhaaaa.

Picture of traing with grafitti
Presentational white space

Mamlaka ya shirika hilo la reli imekubali kukodisha moja ya mabogi hayo kwa kundi la BSQ mkwaka jana, na bila kuchelea kundi hilo limebadilisha bogi hilo kuwa studio ya uchoraji.

Kundi hilo lilikua na wanachama watatu lakini sasa idadi yao imeongezeka hadi wanachama 15.

Vijana hao wanaonekana kila kona wakiendesha shughuli zao na wamebadilisha kabisa muonekano wa eneo hilo kutokana na michoro yao ya kuvutia.

Siku yoyote ukipita karibu na hapo utasikia muziki ukiimba kutoka kwa kijiredio kidogo na kando yake kun a kuna mchoraji anaendelea na kazi ima amesimama au amechuchumaa.

Artist working at an easel
Presentational white space

Brian Muasasia Wanyande mwenye umri wa miaka 26, ambaye jina lake la sanaa linafahamika kama Msale, ni mmoja wa aanzilishi wa BSQ.

Anachanganya upendo wake wa calligraphy na uchoraji kubuni mtindi tofauti wa tattoo, stika na and T-sheti.

"Hii tayari ni vuguvugu flani. Kwangu mimi, natazamia kati ya miaka mitano hadi saba ijayo, BSQ itabadilisha taswira ya sanaa ya uchoraji nchini Kenya," anasema.

Man standing in front of train with graffiti
Presentational white space

Kazi yake pamoja na ya wenzake katika kikundi hicho zinanunuliwa kwa wingi. Wauzaji bidhaa na wasanii wa muziki wanapendelea sana kutumia huduma zao.

Anahisi, BSQ inachanganya kwa ustadi uchoraji na sanaaa ya kupuliza rangi katika ukuta inayofahamika kama Graffitti

Pia nanasema mtindo wao zaidi "um,eegemea tamaduni ya kiafrika na wala sio ya kiigiza bali wanabuni wenyewe" hali ambayo inawapatia nafasi ya "kujieleza kama vijana wadogo wa kiafrika".

painting on train
Presentational white space

Kwa wale ambao wanafikiria sanaa ya uchoraji haina faida yoyote, Msale anawashauri wabadili shana hiyo.

Tangu baba yake alipofariki dunia akiwa mwanafuzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu amekuwa akijitegemea.

Alijifunza kuwa japo inategemea bidii yako mwenyewe unaweza kujikimu kupitia sanaaa ya Uchoraj.

"Kila wakati watu wanatafuta suluhisho la jambo fulani kupitia sanaa.

Haijalishi ni tatizo la iana gani, ni jukumu la mchoraji kubuni mbinu za kukabiliana na tatizo hilo bila kujikwaza," anasema.

Interior of the train carriage
Presentational white space

Ochieng Kenneth Otieno, 30, ambaye jina lake la sanaa ni Kaymist, pia ni mmoja wa waasisi wa BSQ.

Akiwaangalia wachoraji wote anaofanya kazi nao, anasemamengi yamebadilika tangu mwaka jana walipoanza kazi.

"Hatukujua kama watu wangelivutiwa na kazi yetu. Mambo yanabadilika kila siku kwasababu mahitaji yanabadilika kila uchao na hilo linatushangaza sana,"anasema.

Kaymist amejikita zidi katika sanaa ya kupaka rangi na anasema anashangazwa na jinsi watu wanavyokodolea macho baadhi ya kazi zake akitembea kati kati ya jiji la Nairobi

painting on wall
Presentational white space

"Unawasiliana bila kuzungumza na hilo ndilo jambo linalonivutia sana. Unaweza kuwahukumu. Wakati mwingine unaweza kukosea jambo fulani kuhusu hisia za watu."

Na hilo ndio jambo anajaribu kurekebisha upya.

Tofauti na wachoraji wengine katika BSQ, Kaymist hajasomea sanaa ya uchoraji kwa sababu wazazi wake hawakua na uwezo wa kumsomesha.

Lakini ameshikwa mkono na wenzake kama msanii wa Kenya Patrick Mukabi, ambaye amewapa motisha vijana wa rika lake

Sasa, Kaymist nae anawsshika mkono wachoraji wanaoibuka.

David Muchiri, 22, ni mmoja wa vijana anaowasaidia.

Man painting
Presentational white space

"Najaribu kufanya kitu tofauti kila siku," anasema.

"Najaribu kuja na mtindo mpya kutokana na kile ninachojifunza hapa."

Alex Mwangi, 25, ambaye anafahamika kama Lion's Art, anatabaamu huku akijaribu kuelezea kazi yake ya sasa.

Painting of chimpanzee wearing military uniform

"Niliona Sokwe mtu katika makavazi ya Nairobi na hapo wazo likanijia 'Je laiti sokwe mtu angelikua askari ingelikuaje?' Kwa hivyo nimempatia helmet na bandana."

Lion's Art anasema wanachama wa BSQ wanasaidiana. "Tunashauriana na kufanya kazi pamoja.

Hii inatusaidia kujifunz ambinu mpya na kupanua zaidi kazi zetu."

Portrait of a woman in pain

Allan Kioko,24, ambaye wazo lake kuhusu sanaa ya uchoraji ni Think kwa njia ya ubunifu anasema alianza sanaa ya uchoraji akiwa Chuo Kikuu.

Alianza na graphic design lakini aliachana nayo na kujikita zaidi katika ''uchoraji halisi".

Man drawing on a canvas
Presentational white space

Kwa Think, sanaa ya uchoraji ni kubwa sana: "Chochote unachofanya kwenye ubao, karatasi au kompyuta - unaweza kupeleka mtaani."

Azma ya kutaka kuwasiliana na hadhira kubwa inasaidia kuimarisha kazi ya BSQ.

Hili ni kundi ambalo linataka kuwashirikisha watu kazi yao badala ya kuwatenga.

"Nataka kuwapa nafasi vijana kujiendeleza," Mwanzilishi wa BSQMsale anasema. "Tunatengeneza mazingira ambapo watoto wanaweza kusema: 'Nataka kuwa mchoraji kama wale nilikutana nao BSQ.'"

Artist's palette
Presentational white space

Picha zote ni za BBC